Rais Magufuli, hivi huyu jamaa wa NEMC anazungumzia nini?

Kumbe ndiyo hivyo! Ndiyo maana ufanisi wa kazi uko so law. Mimi nimekuwa nashangaa kwanini mambo yanajirudia tena na tena na tena. Sababu ndiyo hiyo! Asante mkuu kwa kufungua macho. Duuh!

Hapa lazima sheria ya watumishi serikalini ibadilishwe.
Tatizo sio kubadilisha sheria tatizo liko hapa....MAFAO NA MABORESHO YA MALIPO YA WATUMISHI!!

Nyongeza za misharaha hazijaongezwa karibu miaka sita, sasa huo ufanisi utatokea wapi?

Sheria ni mbwembwe tu boresha mazingira ya watumishi uone kama hali haijabadilika!!
 
Kwani si ni yeye mwenyewe hua anasema serikali ya Magufuli?

Wewe ulitaka watu wapeleke kero zao wapi wkt inajulikana serikali ni ya kwake?
"---serikali ni ya kwake," na huenda nyinyi wenyewe mnaamini ni "wa kwake"!
 
Kwa sababu Magufuli ni Rais wa nchi na watumishi wote wa serikali wako chini yake. Yeye ndiye anaye dictate utekelezaji wa sera zote za usalama, amani, maendeleo na maisha bora ya wananchi wake.

Sasa kama nyie vidampa mlio pewa majukumu hamtaki kuwajibika basi yeye ana mamlaka kisheria kuwafukuza na kuwaweka watumishi wengine. Kwani nyie mmeuthibitishia umma kuwa ni malooser. Hawezi kazi na hamna utaalam na uelewa wowote ule?
Eeenh, hii ndio sababu?
Kwa hiyo nawe unataka uteuliwe kwa kuimba jina lake hata lisipostahili? Na wewe unajiita 'mtaalam', 'msomi'!
'Sycophants' wakubwa nyie.
 
Binafsi nimetoa mawazo yangu kutokana na hiyo clip uliyoweka. Mimi siyo part ya system na wala sifanyi kazi serikalini. Nimeandika kama independent party.

Kwa mtizamo wangu ni kwamba serikali haijawahi kuwekeza kwenye sewage system infrastructure nchini kwa ujumla. nakumbuka mwanzoni mwa 2000 kulikuwa na mradi mdogo Kijitonyama chini ya World Bank lakini sijui mafanikio yake.

NEMC siyo kazi yao kuweka hizo infrastructure ni kazi ya serikali na idara zake. Ingekuwa ni nchi za wenzetu hizi kazi zingekuwa chini ya manispaa lakini kwa Tanzania ni miradi ya serikali kuu. System ya Tanzania iko complicated na haiwezi kuwa na mafanikio makubwa hata kama kuna juhudi kubwa inafanyika. Labda NEMC wajaribu kwanza kuwaelimisha watu kamla ya kuanza kuwarundikia makesi na fine kibao.

Mimi naamini kuwa underground water sehemu nyingi za makazi Tanzania hasa Dar ziko contaminated both Chemically and Biologically .... Research zinatakiwa kuthibitisha hilo!! Michicha na mbogamboga nyingi Dar zinalimwa kandokando ya mifereji ambayo huko huko ndiko watu wanaflush uchafu wote. Sasa fikiria the microbiological and chemical quality ya hizo mboga mboga sehemu kama kwenye Bonde la Msimbazi.
Asante sana Mr. Zero hoja yako nimeipenda sana. Nami nimeonelea niongezee mawazo yangu tena juu ya hii mada.

Nashindwa kuelewa kwa nini Rais wetu na serikali yake bado hajaona umuhimu wa nchi kuwa na sewage System au mfumo wa maji taka kwa kisawhili. Hivyo asipofanya yeye sasa hivi anafikiri Rais gani mwingine atakuja afanye hicho kitu?

Nashangaa yeye kila wakati anapiga kelele kuhusu nchi ya viwanda na uchumi wa kati wakati ambapo anasahau kuwa ili wadau wengi waweze kuwekeza katika nchi, usafi wa mazingira nao pia una matter sana.

Sidhani kama smart people wako willing kuwekeza kwenye nchi ambayo wakazi wake ambao ni pontental workers na potential buyers wadhoofu wa maradhi na hawana uhakika wa kuishi mda mrefu.

Wajerumani wana msemo wao; "Prevention ist besser als Heilung" yaani prenvention is better than cure. Hapa ina maanisha kuwa kabla ya mtu kuamua kuwekeza kwenye mahospitali mengi kwa ajili ya kutibu magonjwa ni busara kuwekeza katika mambo ambayo hayata wezesha hayo magonjwa kutokea.

Mazingira machafu tuliyo nayo yanamfanya hata mwekezaji mwenyewe kujiuliza na kuangalia kama hata weza athirika na maradhi endapo ataamumua kuwekeza kwenye nchi ambayo hali ya mazingira sio ya kupendezesha, kwani izingatiwe kuwa mwekezaji ni mfanya biashara na mda mwingi anakuwa na contact na watu. Sasa kama hao watu ambao yeye ana contact nao wanaishi kwenye mazingira machafu na hicho kiwanda au biashara yake iko kwenye sehemu chafu sidhani kama itampendeza kuwekeza huko.

Nchi zilizo endelea au zinazotaka kuendelea kiuchumi haziwezi piga hiyo hatua bila kuzingatia mambo ya mazingira. Na hatuwezi tukaanza kuzungumzia mazingira bila sewage System, tutakuwa tuna jidanganya sisi wenyewe. Sewage System hasa kwenye maeneo yenye wakazi wengi ni mgongo wa uchumi na msingi wa maisha bora kwa wakazi hao.

Kama ambavyo umekwish elezea Mr. Zero Sewage System kwenye nchi za wenzetu zilizo endelea basically ni shughuli ya manispaa ya jiji lakini hapa kwetu kwa ajili ya complications za mambo ya kiutawala yalivyo, serikali kuu ndiyo inahusika na uratibu wa mfumo huo lakini serikali kuu iko kimya kana kwamba hili swala hawalioni, hawali sikii na haliwahusu.

Cha kushangaza ni kwamba Rais wetu ana kimbilia kuwekeza katika mambo ambayo yataongeza kuleta mazingira mabaya zaidi badala ya kupanga miradi hiyo ya maendeleo kwa mfano; miundo mbinu ya barabara za mitaa na meingineyo yangeweza kufanyika sambamba na mfumo wa maji taka.

Kama yeye anavyo wahangaika wamachinga na wafanya biashara kupata nyezo bora za kufanya biashara zao bila bughuzi, basi atambue kuwa wakazi wa jiji nao pia wanastahili kuwa na mazingira boreshi kwa maendeleo yao.

Na kama haitoshi sewage systema kwa undani wake inatoa directly ajira nyingi zaidi kuliko hata mtambo wa Stieglers Gorge na SGR na revenue inapata juu, kwani huduma za mradi wa maji taka disposal wakazi wanalipia kama umeme na maji, haitolewi bure.

Wajerumani wakitaka kuanzisha makazi mapya, wenyewe wanaita "Siedlung" (settlememt), kwanza wanafanya mahesabu ya kujua wakazi wangapi wanaishi kwenye hiyo settlement na matumizi yao ya maji taka yatakuwa kiasi gani? Na wakisha jua haya yote wanaanza na matayarisho ya kuweka mfumo wa kusafirisha maji taka kwenda wastewater treatment plants, wenyewe wanaita "Kläreanlangen" kabla hayaja mwagwa mitoni au baharini.

Ieleweke pia kuwa hii mitaro na mabomba ya maji taka hairuhusu maji taka kuzama ardhini ili kukutana na ground water.

Na barabara kwao mara nyingi ni za lami kwa ajili ya magari, njia za waendesha baiskeli na pavements kwa ajili ya watembea kwa miguu. Hiyo ni lazima kwa sababu kwao afya ya watu wao ni kitu muhimu sana kuliko kueneza mahospitali kila kona.

Sasa huyo msomi wetu wa NEMC badala ya kuibana serikali kuu ili ichukue hatua za kutekeleza huu mfumo wa maji taka nchini, yeye badala yake anawatafuta wanyonge tusio weza kujitetea na kutupa mafaini ambayo sisi sio wasababishaji. Pamojabna kuwa wanajua fika kuwa wana wajibu wa kuishtaki na kuipa pressure serikali kuu ili itekeleze majukumu yake.

Haya mambo kwa ujumla yalitakiwa yaanze wakati ule ambapo Tanzania ilikuwa bado haina watu wengi na Dar es salaam ulikuwa mji ambao bado haujawa complicated kama sasa. Mwalim Nyerere na watendaji wake walitakiwa watuwekee sisi msingi wa kuuendeleza huu mfumo badala yake jamaa alikomaa sana na ukombozi wa Afrika kiasi kwamba alisahau kuwa wananchi wake wana hitaji maendeleo yao ya kipekee na kinamna yake.

Nafikiri haya mambo ya kupigania ukombozi wa uhuru wa nchi za Afrika na sera za maendeleo wakati wa ujamaa zimetufanya sisi tuwe na trauma ambayo inatuwia vigumu kujikwamua. Pamoja na neema yote hii ambayo mungu wetu ametujalia, tunashidwa kuitumia kikamilifu kiasi kwamba ikatusaidia sisi wote kuwa na maisha bora.

Mr. Zero haina haja ya kufanya juhudi yoyote kubwa badala yake ni uamuzi tu ndiyo unatakiwa kufanyika kama hela zipo.

Mimi naona jambo la mfumo wa maji taka sio kitu ambacho Rais Magufuli amekipa kipau mbele kikubwa sana kwa sababu nafikiri yeye anapenda kuona vitu vizuri na rahisi kuvitekeleza ambavyo vina mpa matokeo ya haraka.

Swala la mfumo wa maji taka tukiangalia kwa undani, kama ulivyo sema Mr. Zero, ni kitu ambacho kiko complicated sana. Na utekelezaji wake utasababisha watu wengi kuumia kwa kubomolewa nyumba zao au makazi yao kuwa completelly displaced.

Lakini hata hivyo ili kuondoa maafa ambayo sisi na vizazi vyetu vijavyo yatatukumba hapo baadae ni afadhali tuka amua hivi sasa kuyatekeleza hayo kuliko kuwaachia vizazi vyetu vikapata shida ya kuyatatua. Watatulaumu sana.

Kama kwetu ni swala tata basi kwa hao wenzetu wajao litakuwa tata zaidi, kwani hatujui uharibifu wote huo wa mazingira ambao sisi tumeufanya na tunaendelea kuufanya utakuja kuwa na athari gani kwao? Wasomi wetu wa NEMC nina uhakika wanalijua, lakini wanaona heri wanyamaze maadam tuna angamia wote.

Ushauri wangu kwa Rais Magufuli ningemwomba ajitose tu sasa. Hana jinsi. Kwa vile watanzania wame anza kumwelewa sasa nia yake, wata vumilia hata kama wengi wetu tuta athirika na bomoa bomoa.

Pendekezo langu kubwa ni kuwa hivi sasa watu wa mazingira na serikali kuu ianze kampeni kabambe ya kuwaelimisha wananchi mitaani, mitandaoni na mashuleni juu ya umuhimu wa swala hili na hatua ambayo serikali inapaswa kuchukua na maafa au hasara ambayo wananchi waishio mijini yanaweza kuwakuta.

Zaidi ya hayo ni uboreshwaji wa bonde la Msimbazi kwa maneno mengine Jawangani. Bonde lote la msimbazi linatakiwa lichimbwe ili liwe bahari mpaka Surrender. Pembeni ziwekwe nyufa za barabara kuzunguka bonde lote na majengo ya maana ya makazi, starehe, mahoteli na kadhalika pia upandaji wa miti. Hai leti maana kama Surrender kutawaka lakini ukija kangwani giza na maji machafu na harufu mbaya. Jangwani panatakiwa pawe kioo cha Bongo.

Kabla ya maji taka kumwagwa kwenye bonde la Msimbazi kunatakiwa kwenye midomo yote mikubwa ya mito ya maji taka kuwekwa wastewater treatment plants kwa ajili ya kuyasafisha hayo maji.

Maboresho haya yataifanya jiji letu la Dar es salaam lipendeze sana na kuwa katika sura mpya. Bonde la Msimbazi litakuwa tourist attraction na hapo jina la Msimbazi litapata hadhi linalo stahili.
SmartSelect_20190911-103446_Drive.jpeg
 
Tatizo hapa ni neno septic tank! Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa hicho ndiyo aina ya choo kinachoweza kujengwa na mtu yo yote tena kwa gharama nafuu mjini. Kama mtu hawezi kujenga choo cha namna hii ahamie kijijini akajenge choo cha shimo!
Lengo la Septic Tank nini? Septic tank sio choo bali ni Facility. Soma definition Wikipedia:

A septic tank is an underground chamber made of concrete, fiberglass, or plastic through which domestic wastewater (sewage) flows for basic treatment.

Settling and anaerobic processes reduce solids and organics, but the treatment efficiency is only moderate (referred to as "primary treatment"). Septic tank systems are a type of simple onsite sewage facility (OSSF).

They can be used in areas that are not connected to a sewerage system, such as rural areas.

The treated liquid effluent is commonly disposed in a septic drain field, which provides further treatment.

Nonetheless, groundwater pollution may occur and can be a problem.

Sasa mijini kwenye densely populated areas kama Dar es salaam (angalia picha) utapata wapi nafasi ya kusambaza maji taka (Drainfield)? Kasome kwanza mambo ya dimensions halafu njoo na Argument yako tena.
SmartSelect_20190920-005940_Gallery.jpeg
SmartSelect_20190920-010313_Google.jpeg
 
Kwa hiyo kwako Magufuli ndio mtaalam wa mambo hayo?
Mbona watu mmekuwa kama majuha vile?

Unamtaarifu Magufuli afanye nini? Kila kitu 'Magufuli, Magufuli...' Hata kufikiri mnamtegemea Magufuli...!
Mkienda chooni...Magufuli; hata vitandani kwenu na wake zenu, mtakuwa mnalia... Magufuli, Magufuli!!
Baelese Baelewe, sio kila kitu ni Magufuli

P
 
Baelese Baelewe, sio kila kitu ni Magufuli

P
Mr. Mayalla tofauti yako na watu kama mimi ni kuwa wewe ukienda Ulaya na ukiyaona maendeleo ya wazungu una yastaajabu na kuya furahia na kuamini kwamba wao ndiyo Mungu wanaweza kila kitu. Sisi hatuta wafikia.

Mimi nikienda Ulaya na nikiyaona maendeleo ya Wazungu nina staajabu na kuya furahia, lakini nitajiuliza imekuwaje wao wameweza na sisi tuna shindwa wapi?

Sitapenda leo kuanalyse taarifa na michango yako mingi unayotoa mitandaoni ila tu itoshe kukufahamisha kuwa Magufuli is the head of state na tumeshuhudia kuwa sisi watanzania tulikuwa tumepalarize. Tulifikiri tukikaa kwenye mjadala mingi ya kisiasa basi maendeleo yatakuja yenyewe, wakati kumbe kulikuwa na watu ambao ni wajanja wakitupiga.

Kwa hali hiyo sioni kama kuna ubishi ambao kwa mtu mwenye akili timamu atashindwa kuyaona matendo na nguvu ambazo Rais Magufuli anazitunia kwenye kuhakikisha kuwa nchi yake na wananchi wenzake kwa pamoja tunapiga hatua ya maendeleo. Watu wa katiba hii Magufuli wakipatikana watatu zu kwa mfululizo basi ujue kuwa tutafika tu.

Ndiyo tuna mlilia kila kitu Magufuli kwa sababu imethibitika kuwa yeye ni kiongozi bora sio tu Tanzania bali katika bara zima la Afrika na ni msimamizi mzuri sana na wa dhati wa mali za umma.

Ndiyo maana sisi wazalendo tumeona tutumie hii nafasi kushirikiana naye katika vita tunayo pambana ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini ambao tumejitakia kwa kudhani kila kitu ni siasa na katiba tu.

Huko nyuma hii nchi ilikuwa yenu majournalist wababaishaji, mliweza pindisha mambo kwa matakwa yenu, lakini sasa tumeirudisha nchi yetu mikononi mwetu. Wazalendo tunataka maendeleo ya kweli, hatutaki longo longo za kukufanya wewe na majournalist wenzako fake mpate Story za kutuonyesha sisi ni mazezeta.

Nyie wengi wenu sio majournalist kama mnavyo jipa bali ni wanasiasa wa upande fulani.
 

Rais Magufuli huyu mzee anaelewa kweli anachokieleza au anabwabwaja tu maneno bila kujua nini anachokisema? Hiyo elimu yake imemwelimisha hayo anayo yatoa?

Anatueleza sisi juu ya septic tanks kana kwamba watanzania wanajua what the septic tanks are? Katika mazingira kama hayo kwenye picha hayo ma septic tanks wakazi wa mijini watayaweka wapi?

Septic tanks kwanza gharama yake sidhani kama watu wa uswahilini wanaweza ku afford. Zaidi ya hayo yanahitaji eneo kubwa kwa ajili ya kusambaza maji taka ardhini

Dar inahitaji investiment kubwa sana ya Sewage System. Haya mambo ya water treatment ya mtu mmoja mmoja kwa mjini ni kudanganyana tu. Hii System ina-work kwenye isolated Houses.View attachment 1210060

Septic tank ni ya kukufanyia taka ngumu si waste water na baadhi ya maeneo ya Dar hizi septic tank zipo,Mtoa mada mambo usiyoyaelewa uliza si kujifanya mjuaji
 
Lengo la Septic Tank nini? Septic tank sio choo bali ni Facility. Soma definition Wikipedia:

A septic tank is an underground chamber made of concrete, fiberglass, or plastic through which domestic wastewater (sewage) flows for basic treatment.

Settling and anaerobic processes reduce solids and organics, but the treatment efficiency is only moderate (referred to as "primary treatment"). Septic tank systems are a type of simple onsite sewage facility (OSSF).

They can be used in areas that are not connected to a sewerage system, such as rural areas.

The treated liquid effluent is commonly disposed in a septic drain field, which provides further treatment.

Nonetheless, groundwater pollution may occur and can be a problem.

Sasa mijini kwenye densely populated areas kama Dar es salaam (angalia picha) utapata wapi nafasi ya kusambaza maji taka (Drainfield)? Kasome kwanza mambo ya dimensions halafu njoo na Argument yako tena.View attachment 1211812View attachment 1211813
Kwani choo siyo facility?
 
Kwani choo siyo facility?
Sawa lakini hapa tuna zungumzia Facility ambayo ina special function for the environment. Choo kwa mtindo wetu wa ujenzi wa kushiba shimo na kumaliza kila kitu, sio busara kwa mazingira.

Lengo hapa ni kutaka kukidhi mazingira mazuri ambayo yatatuwezesha sisi kuto pata maradhi mara kwa mara ambayo tunaweza tuka jiepusha nayo.
 
Kwani choo siyo facility?
Sawa, lakini hapa tuna zungumzia Facility ambayo ina special function for the environment. Choo kwa mtindo wetu wa ujenzi wa kuchimba shimo na kumaliza kila kitu, sio ujenzi rafiki kwa mazingira.

Lengo hapa ni kutaka kukidhi mazingira mazuri na rafiki kwetu ambayo yatatuwezesha sisi kuto pata maradhi mara kwa mara ambayo tunaweza tuka jiepusha nayo.

Waulize watu wa mazingira NEMC wakupe data za ground water za jiji la Dar es salaam ili ujionee parcentage za bacteria na toxic elements ambazo ziko humo ndani.

Unajua kwa nini hawako transparent? Waambie waweke data zao wazi.
 
JF of GT ni raha tupu watu wanajifanya wanabusara, wanajali na wakomakini, hebu tumchukue mmojammoja atupeleke nyumba anayoishi kabla ya kumuomba atupeleke kijijini kwake kwa babake, mjadala huu hautautaka uendelee.
Tujue tunaweza kujenga choo bora cha gharama ndogo sana ambacho haja kubwa na mkojo havichanganyiki na tukaishia kupata mbolea nzuri na kuzalisha mbogamboga majumbani kwetu.
 
Sawa, lakini hapa tuna zungumzia Facility ambayo ina special function for the environment. Choo kwa mtindo wetu wa ujenzi wa kuchimba shimo na kumaliza kila kitu, sio ujenzi rafiki kwa mazingira.

Lengo hapa ni kutaka kukidhi mazingira mazuri na rafiki kwetu ambayo yatatuwezesha sisi kuto pata maradhi mara kwa mara ambayo tunaweza tuka jiepusha nayo.

Waulize watu wa mazingira NEMC wakupe data za ground water za jiji la Dar es salaam ili ujionee parcentage za bacteria na toxic elements ambazo ziko humo ndani.

Unajua kwa nini hawako transparent? Waambie waweke data zao wazi.
Kwa kukusaidia walio na data za water quality Dar es Salaam ni Bonde la Wami Ruvu ambao ndiyo wenye mamlaka kisheria kusimamia rasilimali za maji. Hivyo ukitaka data watembelee katika ofisi zao Morogoro ambapo ndiyo makao makuu na ofisi ndogo ipo Ubungo.
 
Kwa kukusaidia walio na data za water quality Dar es Salaam ni Bonde la Wami Ruvu ambao ndiyo wenye mamlaka kisheria kusimamia rasilimali za maji. Hivyo ukitaka data watembelee katika ofisi zao Morogoro ambapo ndiyo makao makuu na ofisi ndogo ipo Ubungo.
Asante mkuu kwa msaada wako. Nitajaribu kufuatili.

Swali moja ambalo ningeomba kukuuliza kama haita kukwaza, ina maana NEMC hawana mamlaka hayo ya kutoa au kuhifadhi ground water data quality za DSM?

Mimi nilifikiri mtu yeyote anaweza pata kila kitu kwenye Home page yao!
Natoa Mfano hapa wa;

"Hessisches Landesamt für Naturschutz, Umwelt und Geologie"

yaani kwa kiingereza;

"State Office for Nature Conservation, Environment and Geology of the State Hessen" nchini Ujerumani na napata Report nzima bure.

Duuh! Bado tuna njia ndeeeeefu mpaka kufikia huko!View attachment Stickstoffumsatz_Bert_Juli_2019.pdf
 
Asante mkuu kwa msaada wako. Nitajaribu kufuatili.

Swali moja ambalo ningeomba kukuuliza kama haita kukwaza, ina maana NEMC hawana mamlaka hayo ya kutoa au kuhifadhi ground water data quality za DSM?

Mimi nilifikiri mtu yeyote anaweza pata kila kitu kwenye Home page yao!
Natoa Mfano hapa wa;

"Hessisches Landesamt für Naturschutz, Umwelt und Geologie"

yaani kwa kiingereza;

"State Office for Nature Conservation, Environment and Geology of the State Hessen" nchini Ujerumani na napata Report nzima bure.

Duuh! Bado tuna njia ndeeeeefu mpaka kufikia huko!View attachment 1212073
Unapotaka kujua jambo fuata utaratibu wa kisheria wa nchi husika. Tanzania mwenye mamlaka ya kulinda, kuhifadhi, na kugawa maji kwa matumizi mbalimbali ni wizara ya maji kupitia ofisi za maji za mabonde. Nemc chini ya ofisi ya makamu wa Rais inawajibika na usimamizi wa mazingira! Mazingira hapa inahusu mifumo yote ya asili kama maji, ardhi, hewa, sauti, mwanga, harufu nk.

Hivyo kwa maelezo hayo utagundua kuwa nemc wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara ya maji katika masuala ya maji na maeneo asili ya maji kama mito, mabwawa, maziwa(lakes), maji ardhi (groundwater) nk.

Kujibu swali lako nemc utapata data za groundwater zinazohusiana na mazingira.
 
Unapotaka kujua jambo fuata utaratibu wa kisheria wa nchi husika. Tanzania mwenye mamlaka ya kulinda, kuhifadhi, na kugawa maji kwa matumizi mbalimbali ni wizara ya maji kupitia ofisi za maji za mabonde. Nemc chini ya ofisi ya makamu wa Rais inawajibika na usimamizi wa mazingira! Mazingira hapa inahusu mifumo yote ya asili kama maji, ardhi, hewa, sauti, mwanga, harufu nk.

Hivyo kwa maelezo hayo utagundua kuwa nemc wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara ya maji katika masuala ya maji na maeneo asili ya maji kama mito, mabwawa, maziwa(lakes), maji ardhi (groundwater) nk.

Kujibu swali lako nemc utapata data za groundwater zinazohusiana na mazingira.
Thank you so much for your information! Asante sana!
 
Back
Top Bottom