Mambo manne aliyoyafanya Rais Magufuli katika muhula wake wa awali yaliyonifurahisha

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,486
51,063
Kuna mambo mengi sana ya msingi ambayo sikubaliani na aina ya utawala wa rais Magufuli. Mathalani sikubalini na matendo yake ya kuminya haki za msingi za wananchi kujichagulia viongozi wao kwa ridhaa zao, kwa mfano yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 kisha yaliyofanywa kwenye uchaguzi mkuu ambapo kuba uporaji wa waziwazi wa maamuzi ya wananchi ni mfano mmoja wapo wa mambo ambayo kiukweli sikubaliani nayo na ninaamini kuwa mtanzania yeyote anayeheshimu katiba ambaye anatambua kuwa mamlaka yote nchini yanapaswa kutoka kwa wananchi na Siyo TISS kushirikiana na NEC na Polisi kutuwekea viongozi wakiwemo wabunge na madiwani wa mfukoni. Hili halikubaliki.

Lakini pia sikubaliani na uonevu na siasa za manunuzi ya watu, matendo haya hayajengi nchi bali yanasimika rushwa kwenye kiini cha maamuzi ya nchi yetu, kwa sababu wanaohongwa ili kubadili political alliance wao wataendelea kuamini katika fedha kama namna ya kupata mamlaka katika nchi na si kupitia wananchi kwenye sanduku la kura.

Waliopata fursa za uongozi kupitia rushwa kamwe hawawezi kupambana na ufisadi na rushwa. Kwa hiyo haya mambo ya kuhongahnga vyeo atharo yake tutaanza kuiona muda mfupi sana ujao, kwa maana tumetaasisisha rushwa kwenye uongozi wa nchi.

Hata hivyo wahenga walisema hata saa mbovu huwa inasema kweli angalau mara moja kwa siku

kuna mambo makuu matatu ambayo utawala wa Magufuli ulinifurahisha sana kwenye awamu yake ya kwanza ya uongozi, haya yaligusa maisha ya watu, na ni mambo mazuri
nitayataja : Sitotaja mambo kama REA, Barabara n. k kwa sababu hayo mambo yalikuwa pia yanafanyika kwa kasi tu katika serikali ya awamu ya nne, nitataja ya kwake binafsi

1. Kuwaondolea wananchi service charge kwenye umeme
Alipoingia madarakani, Magufuli alikura umeme unanuliwa kwa bei ghali sana, na miongoni mwa vitu vilivyokuwa vinafanya bei iwe kubwa na mzigo kwa wananchi ni hiyo service charge. Katika vitu vya mwanzo alivyoviondoa ni hiyo, binafsi nilishangilia sana. Niliwaambia wenzangu kuwa yes sasa tumepata rais (Hii ilikuwa ni kabla ya mambo ya ajabuajabu ya watu kupotezwapotezwa)

2. Kupiga marufuku viroba
Katika mambo makubwa ambayo Magufuli alilisaudia Taifa ni kwenye hili suala, Taifa iliuwa linaangamia hivihivi mbele ya macho yetu, vijana walianza kuwa kama mazombi, wanalewa pombe kali sana za viroba, wengine ni waendesha vyombo vya moto kama pikipiki, ajali za pikipiki zilikuwa ni nyingi sababu ya viroba. Lakini Baada ya kupigwa marufuku angalau leo tuna vijana wenye akili zao wapo wanahustle lakini angalau wakiwa sober. Bila kupiga vita viroba, matukio ya ukwapuaji njiani, ajali za pikipiki, ukabaji, ubakaji vingeendelea kutisha zaidi

3. Suala la kupiga Marufuku mifuko ya plastiki
Kama kuna kitu inabidi tumshukuru Magufuli ni hiki. Hii nchi ilikuwa inageuka kuwa jalala, nahisi pengibe elimu yake ya Kemia ilimsaidia kuliona hili kuwa ni tatizo la msingi, kwa sababu mifuko ya plastic haidecompose, inaweza kukaa ardhini hata miaka 100 iko vilevile. Pia mito yetu ilikuwa mhanga mwingine, ungeenda kwenye mito, ilijaa maplastic hadi ikawa mizito kutiririka na matokeo yake kutuama na kuharibika flow yake, Hebu tazama mto msimbazi, ule mto hadi miaka ya 1995 ulikuwa bado uko vizuri, lakini hebu tazama hali yake ilikuwaje baada ya kukithiri kwa plastic ilikuwa ni balaa kubwa, mto ksisha khabar yake!
Namuomba Magufuli akaze sana kwenye ishu ya mifuko ya plastic na asiishie hapo tu, atafute namna ya kudeal na chupa za plastic, hizi nazo ni balaa kubwa kabisa kwa mazingira

4. Kudhibiti ujambazi
Uongo mbaya, ujambazi umepungua sana kwenye awamu hii ya utawala. Kabla yaMagufuli kuingia madarakani, watu walipofwa sana mali zao na majambazi yalikuwa yanapiga show bila wasiwasi sana. Lakini kwenye awamu ya kwanza ya utawaa wa Magufuli mambo haya ya ujambazi yalithibitiwa sana

Kitu gani kilinifanya niuchukie utawala wa Magufuli?

Mpaka mwishoni mwa mwaka 2016 usingeniambia kitu juu ya JPM, Ila turning point ilikuwa.

1. Ukatili, Ukatili ulionitisha kabisa mpaka nikakinai ni KUVUNJIWA NYUMBA wananchi wa Ubungo-Mbezi licha ya kuwepo kwa stop order ya mahakama, lile zoezi, vild vilio vya wananchi, nikikumbuka yale magreda yaliyokuwa yakipita kwa ukatili mkubwa huku wananchi wakiangalia na hawawezi kufanya chochote huku kukiwa na Polisi wameshika mitutu wanawaangalia kwa jicho kali wasilete fyoko, halafu baadae akaleta kauli kuwa watu wa mwanza wasivunjiwe kisa walimpa kura, Aisee hii kitu ilinichefua vibaya mno, Iliniumiza mno. Hapo hapo nikamuangalia Magufuli kwa jicho baya sana, sikupenda ukatili ule kwa kweli.

2.Kisha baadae au kabla yake yakatokea matukio mengi hapo ya wasiojulikana
kupigwa risasi Lissu, kutekwa Mo, Roma Mkatoliki, Azory Gwanda

3. Pia ajira zilizoonekana kukaa kidini ilinipiss off vibaya sana
Ukweli lazima usemwe Magufuli kwenye awamu yake ya kwanza Waislamu aliwasideline sana kwenye teuzi zake. Pindi ulikuwa ukiangalia zile teuzi kianzia kwa mawaziri, manaibu waziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, MaRAS, MaDAS, wakurugenzi wa mashirika ya umma, Mabalozi n. k unsona kabisa kuna udini uliokubuhu. Sijui huenda akalirekebisha hili safari hii, lakini ni mambo yaliyonipiss off vibaya sana kwenye muhuoa wake wa kwanza

4. Kutoheshimu katiba ya nchi
Jinsi alivyopiga marufuku vyama vya siasa kufanya shughuli zao halali kwa mujibu wa sheria. Kutumia mahakama kama komoa, yaani wewe ukiuwa mwiba kwa serikali yake, au ukimchukiza basi kesi ya kutakatisha fedha na uhujumu uchumi unayo. Wengi wamewekwa ndani muda mrefu sana kwa makosa yenye dhamana. Hili la kutheshimu katiba na kuonea watu kupitia mahakama pia lilinichukiza sana.

Anyway hebu tuone, Jiwe ni unpredictable huenda akatushangaza au akatuduwaza!
 
Back
Top Bottom