Rais Magufuli hajawahi kupangiwa na hatapangiwa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila
0768239284

Jana baada ya Balozi Dkt Bashiru kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu kiongozi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Kijazi aliyefariki kumekuwa na maneno mengi. Watanzania wamekuwa na mijadala mikubwa ya nani atakuwa mrithi wa Mhe Balozi Bashiru.

Karibu mitandao yote ya kijamii ambayo mimi ninaisoma kuna mijadala hiyo. Watu kwenye kujenga hoja na uhalali wa kile wanachokianini wametoa na orodha ya majina ambayo wanaamini yatatoa Katibu Mkuu.

Sikutaka kuwa sehemu ya mjadala huo ambao hauna mantiki kwa kuwa vigezo vya mteuaji si lazima vikafanana na uhalisia wa matamanio yetu.

Ninachoweza kusema na kukisimamia ni kuwa Mhe Rais hapangiwi. Anavyo vigezo vyake ambavyo huviweka katika kuwapata wasaidizi wake na si kelele zetu za kubashiri mitandaoni.

Wakati Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM hakuna aliyekuwa akimdhania, na pengine watabiri wote hamkuwahi kumtabiria. Lakini wakati jana Balozi Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hakuna aliyekuwa amemuweka kwenye orodha ya utabiri kuwa angeweza kuteuliwa kuchukua hii nafasi.

Kwa mantiki hiyo, hata hizi orodha mnazotembea nazo kuwa huyu anafaa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa JPM atakuja na surprise ili aendelee kuwathibitishia kuwa hategemei utabiri na presha kupata wasaidizi wake.

Ni jambo jema kuombeana heri, lakini JPM anajaribu kujenga nchi katika hali ya kuondoa uswaiba na ujamaa. Hataki kuleta watu ambao tayari wana makundi, anataka watu ambao hawana makundi na wanakuwa wapya. Ukiangalia safu ya CCM hasa sekretariati pale juu alianza na watu wapya kabisa ambao wengi hatukuwategemea. Kwa mantiki hiyo orodha zote mnazojaribu kutabiri hata kama alikuwa anazifikiria ataziweka benchi.
 
Teuzi za surprise zinafuatiwa na tumbuatumbua ambazo hazijawahi shuhudiwa katika awamu zilizomtangulia.

Labda angeenda sambamba na matarajio ya walio wengi uenda kutumbuana kusingekuwepo kwa kiwango kikubwa kihiyvo.
 
Fanya kazi ili upate ridhiki yako kwa jasho lako.

Huku kujipendekeza pendekeza utakuja kuolewa mara mbili.
 
Back
Top Bottom