MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 385
Mwaka 2015 hasa katika kuelekea katika uchaguzi mkuu, tuliona Mh. Edward Lowassa akitembelewa na wageni katika makundi mbalimbali. Tuliona makundi ya vijana waliojiita “Wazalendo”, makundi ya Viongozi wa dini, Makundi ya wafugaji na wakulima, na makundi mengineyo.
Ni makundi yaliyodai kuwa yanakwenda kwake kwa lengo la kumsalimia mpendwa wao huyo, lakini pia kumshawishi kuchukua fomu za kugombea katika nafasi ya Urais wa JMT kupitia CCM. Ni makundi yaliyotushangaza wengi kwa namna ambavyo yalikuwa yakipishana mlangoni, na kuitawala kalenda ya mheshimiwa Eddo kwa kiasi kikubwa.
Yaliibuka madai kutoka kwa watu mbalimbali kwamba makundi hayo yaliandaliwa na kugharamiwa na “mtembelewaji”, lakini wengine tulikataa na kusema hayo makundi yaliashiria upendo mkubwa wa Watanzania kwa Mzee wetu huyo. Lakini cha kushngaza tangu aangushwe katika uchaguzi ule wa Mwaka 2015, hao wageni hawaendi tena kwake kwa lengo la kwanza ambalo ni kumsalimia. Ni kama amekuwa adui yao sasa, maana urafiki wao haupo kwa kiasi kile tulichoshuhudia kipindi hicho. Hali hii inatufanya sasa tuamini kwamba huo mchezo aliucheza Mzee mwenywewe ili kuweza ku-win mawazo ya watu wengi kwamba anapendwa sana, ambapo kwa kiasi chake alifanikiwa; maana alipata kura nyingi though hazikutosha. Mh. Rais Magufuli hajakataza watu kutembelewa na wageni nyumbani kwao, hivyo makundi yale bado yana nafasi ya kwenda kumsalimia mpendwa wao kama upendo walionao kwake ulikuwa ni real.
Otherwise tunasubiri kwa shauku kubwa movie nyingine hapo 2020, ambayo wengi wanadai kwamba Eddo anaiandaa kimya kimya kwa sasa na ambayo ni tamu zaidi ile movie ya Mafuriko ya 2015.