Rais Magufuli azidi kupotoshwa na Wasaidizi wake

Nilifikiri una jipya kumbe yaleyale yanayoongelewa kila siku.

Bado wengine tupo nyuma yake kwa sana tu, na anatufurahisha.
 
Rais JPM a.k.a Catepillar amezidi kuporoka kwa ummarufu baada ya kuonekana kwamba kila jambo analoshauriwa na Wasaidizi wake hulitekeleza bila ya kulipima kabla ya utekelezaji!
Mpaka sasa kuna makosa mengi ambayo JPM ameyafanya kiasi cha Watanzania wengi kuanza kujenga chuki na hasira zidi yake na serikali yake. Nitaeleza machache kati ya hayo!

Swala sukari:Kama kuna jambo ambalo limempunguzia heshima na umaarufu ilikuwa kupiga marufuku uingizaji wa sukari toka nje kwa kisingizio cha kulinda viwanda vya ndani!Amri hiyo imesababisha mtikisiko na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo muhimu kipindi chote cha mwezi mtukufu kiasi cha bei kufikia 6000/- kwa kilo.
Bunge la Bajeti 2016/7: Bunge la Bajeti lilkiongozwa na Naibu wa Spika Ackson Tulia alilivuruga Bunge kwa kuliendesha kama vile ni taasisi au chombo cha mtu binafsi.Nina hakika Magufuli ni shahidi wa kila kilichokuwa kikitendeka Bungeni na sina hakika kama alihoji kuhusu hali hiyo.Yawezekana alikuwa akidanganywa au kushauriwa vibaya kuwa ati Tulia ndiyo mbabe wa Wapinzani na kuwa amewanyosha kwa timua timua ya Wabunge wa UKAWA! Nakumbuka baada ya kuapishwa JPM alijitanabaisha atatumikia watu wote waliompigia kura na wale wa UKAWA lakini kinachofanyika ni kinyume chake.Swali la kujiuliza hapa ni IKO WAPI DEMOKRASIA ndani ya Bunge letu?

Kupiga marufuku mikutano ya kisiasa: Nina hakika kuna mahifidhina ndani ya CCM waliomshauri JPM kuwa akipiga marufuku mikutano ya kisiasa ya Upinzani basi ataiongoza Tanzania kwa raha mustarehe. Huu ni udhauri mbaya na kama JPM hataufanyia kazi utamgharimu kwenye utawala wake.

Kuchukua Wataalamu toka Rwanda: Juzi Watanzania wsmeshuhudia Rais Paul Kagame wa Rwanda skitembelea Tanzania na kuwa na mazungumzo na JPM kuhsu Rwanda kuleta wataalamu wa IT toka Rwanda kutengeneza mtandao wa ukusanyaji Kodi na wengine kuhsu uendeshaji wa ATC! Sina hakika kama Magufuli ana uelewa wa kutosha kuhsu mambo ya IT kiasi cha kuwaponda Watanzania waliobobea kwenye IT wakiwa wamesomea vyuo vikuu vya ndani na nje! Sina hakika kama JPM anajua kuna kitu kinaitwa Mkongo wa Taifa(NICTBB) unaosimamiwa na Serikali yenyewe kupitia Kampuni ya TTCL na kwamba mkongo wa Taifa umeiunganisha Rwanda kwa kutumia Wataalamu wa Kitanzania toka TTCL!
Je, Magufuli amewahi kuwaita Wahandisi wa IT wa Kitanzania na kuwauliza kama hawawezi kufanya hizo kazi za IT kiasi cha kutafuta Wanyarwanda?Badala yake yeye analaumu tu kuwa ati Watanzania wanapenda rushwa! This is not fair at all!
Acha waendelee kumpotosha tu. Si waliimba wananchi tuisoma namba. Unadhani tutaisoma namba vp bila ya kupotoshwa
 
Nafahanu ndio ila computer engineer kuna IT ndani yake,ila IT sio computer engineer .namaanisha mtu wa computer engineering anaweza kufanya kazi za IT
Sio kweli icho ni kipande kidogo sana IT ni zaidi ya computer enginering
Hapo tunadeal zaidi na software
 
Tukiwaambia hawa jamaa wanakurupukaga kuna majitu yanabisha ... Hilo la kuleta wataalamu kutoka rwanda kwetu ni fedheha tena fedheha kimataifa...na kuna miprofesa inapiga makofi kusupport upuuz.. Cjui ndo huo uprofesa wa godfather.. Tanzania tunadhalilika sasa kwa maamuzi ya wakurupukaji
Mimi nafurahi sana kwa jinsi magu anavyo tupelekesha ili tupate akili na mara ifikapo 2020 tuwe na uchaguzi wa kutufaa
 
kuna computer engineering au computer engineer kwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu hakuna tofauti ya IT na computer science so computer engineer ni mhandisi na anafanya kazi za IT
Kuna tofauti mzee kati ya it na comp science tena sana ebu jaribu kusoma online uone utofauti kati ya hayo yote mambo matatu uliyoyataja
 
Juzi kwenye mabango yenu mmesema hashauriki, leo mnasema anatekeleza ushauri bila kupimayou people ni lazima mtakuwa na Bipolar disorder.
 
Ukitaka kujua na kupanua ubongo basi angalia vizuri ile video ya mkutano wa pale BOT na Pro Ndullu, jaribu kuwaangalia wale mabwana kwenye nyuso zao na utapata walichokuwa wanakifikiria
 
Hiyo ya kutafuta wataalamu wa IT Rwanda ni sawa na kwenda kutafuta migodi ya Tanzanite Kenya
 
Sio kweli icho ni kipande kidogo sana IT ni zaidi ya computer enginering
Hapo tunadeal zaidi na software
Sio kwel cmp engr. Asomi database labda ungeniambia cmp science kidg ningekuelewa yani wote apo anasoma somo kwa undani kuhusu computer ni computer science ila anaweza akawa ajui kuitumia more deep computer science ana deal na programming languages yani software design zaid na kutumia kidg na IT anajua kutumia zaid na anagusa karibu kila kitu ndo mana anaweza kuwa ndo mkuu wa kitengo kwenye departments ila wanaojenga system ni computer science mara nyingi ila kama ukiwa mjanja IT unaweza kufanya kaz ya mtu wa computer science coz vyote basics unazo kama networks au programming
 
Back
Top Bottom