Rais Magufuli awataka Watanzania kutumia mvua zinazoendelea kujenga Uchumi wa Taifa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,649
2,000
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kutumia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Nchini kujenga Uchumi wa Taifa.

Akiwa Muleba Mkoani Kagera, Rais Magufuli Taifa limeingia katika Uchumi wa Kati, na ni lazima liendelee kupanda na kwenda kwenye Uchumi wa juu zaidi, huku akiwataka Watanzania kujipanga katika suala hilo.

Aidha, Rais pia amesema anatarajia kuwepo Mkoani humo kwa zaidi ya siku tatu/nne ambapo baadhi ya miradi ya Maendeleo itazinduliwa, pia mkataba wa mabilioni utasainiwa na kuwezesha Wananchi wapate Ajira.


437FBF87-17B1-4DA3-93E8-C5D34DFD6A27.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Muleba wakati akiwa njiani kuelekea Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 17 Januari 2021
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom