Rais Magufuli awataka wakandarasi kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Ndugu wanaJF,

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) uliofanyika jijini DSM

Pix1.jpg


“Nawatolea mfano idara ya mahakama, imetangaza kujenga mahakama za mwanzo na za wilaya, kwenye bajeti wana shilingi bilioni 24, makadirio ya kitaalam yanaonyesha kila jego lisizidi milioni 200, wakandarasi wazalendo walipoomba katika nyaraka zao wametaka jengo lijengwe kwa bilioni 1, sasa nakuuliza Mheshimiwa Mwenyekiti na ndugu wkandarasi, hata kama upendeleo, upendeleo huo utapasua moyo”.


index.jpeg
indgex.jpeg
 
Serikali itunge sheria ya "faida elekezi"; itakayoweka kiwango cha juu cha faida.
1.Kwanza sheria huyo ifafanue neno "faida"
2. Pili ihalalishe kitu kinachoitwa faida
3. Sheria hiyo itamke kwamba ni mrufuku kuuza bidhaa/huduma au kitu chochote kwa faida inayozidi asilimia 200 au 400 (200 to 400%) ya gharama halali za bidhaa/huduma husika.
4. Itowe na adhabu elekezi kwa atakayevunja sheria hiyo.
FAIDA ZA SHERIA HII.
1. Itaongeza uwazi katika process ya yabuni (tenda) kwasababu wakandarasi watashindanishwa kwenye kuonyesha faida iliyo chini ya faida elekezi.
2. Itapunguza rushwa katika utaratibu wa kupata mzabuni.
3. Itarahisisha ulipaji wa kodi bila kushutishwa.
 
kodi ni nyingi sana kwa wakandarasi
pia malipo wanachelewesha mno yaani kama mtu kakopa benk lazima afilisike
bado makato ya retention sijui
 
Serikali itunge sheria ya "faida elekezi"; itakayoweka kiwango cha juu cha faida.
1.Kwanza sheria huyo ifafanue neno "faida"
2. Ili ihalalishe kitu kinachoitwa faida
3. Sheria hiyo itamke kwamba ni mrufuku kuuza bidhaa/huduma au kitu chochote kwa faida inayozidi asilimia 200 (200%) ya gharama halali za bidhaa/huduma husika.
4. Itowe na adhabu elekezi kwa atakayevunja sheria hiyo.
FAIDA ZA SHERIA HII.
1. Itaongeza uwazi katika process ya tenda kwasababu wakandarasi watashindanishwa kwenye kuonyesha faida iliyo chini ya faida elekezi.
2. Itapunguza rushwa katika utaratibu wa kupata mzabuni.
3. Itarahisisha ukulipaji wa kodi bila kushutishwa.
wazo zuri,ila unafkr wabunge wa c.c.m wataupitisha waraka huo na rais kuusaini uwe sheria!!?
 
Taarifa ya ikulu inasema Raisi Magufuli amesema Serikali yake....... halafu bungeni wabunge wa ccm wanakanusha mweeee
Mkuu, tofautisha maneno ya kisiasa na maneno ya kisheria.

Tatizo unataka kuyafanya maneno ya kisiasa kuwa maneno ya kisheria.

Sheria hazina siasa lakini siasa wakati mwingine hazina sheria.

Rejea Katiba ya nchi 1977 ili upate majibu yake kuhusu Muundo wa serikali na nani mwenye mamlaka ya kuunda serikali baada ya Uchaguzi Mkuu. Achana na maneno ya wanasiasa.
 
Huyu Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu anapaswa kujua namna ya kuandika press release.Ukiangalia habari zake ni kama anaandika gazeti.Ni vyema habari ikawa fupi na yenye ujumbe uliokamilika.Press release nyingi anazoandika mtaalamu huyu ni ndefu kama kurasa za gazetI
Pammoja na hayo ila core issue ni gharama kubwa ya wakandarasi wazawa kulinganisha na bei halisi.Shida ya kula bila kunawa inalitafuna taifa letu.ni aibu kuona hao waitwao local contrctors hawajui kupanga na kuweka makadirio kulingana na kazi yenyewe
 
Wazo la rais ni agizo kwa watendaji, wakandarasi wazawa mpo tayari? Kutoka bilion 1 mpaka mil 200 kwa jengo!
 
Taarifa ya ikulu inasema Raisi Magufuli amesema Serikali yake....... halafu bungeni wabunge wa ccm wanakanusha mweeee

Mnaangali makosa tu...ni wazi kuwa ikiwa watu mnakazania kuangalia makosa tu, mtayapata...sometimes you have to be positive in your contributions ...mmekazana CCM, CCM, CCM.....kwani hamuwezi kufikiri tofauti?????????
 
Huyu Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu anapaswa kujua namna ya kuandika press release.Ukiangalia habari zake ni kama anaandika gazeti.Ni vyema habari ikawa fupi na yenye ujumbe uliokamilika.Press release nyingi anazoandika mtaalamu huyu ni ndefu kama kurasa za gazetI
Mmeanza tena mgao mmeshapata!
 
Jengo la bilioni moja!??
Akija mchina akitaja kiwango cha chini,akipewa kazi lawama

Ni shida tu. Hata makandarasi wazalendo nao ni majipu. Kwanza hata wanapopewa kazi, hawa ndio wanaongoza kujenga miradi chini ya kiwango. Wanapenda kulalamika tu, hakuna lolote la maana. Nafuu tuendelee na Wachina wetu.
 
Kama zabuni zimepatikana kwa njia ya rushwa Na aliyekupatia anataka 10%.Lazima ifike hiyo bei.Kuhusu wakandarasi wachina Wao hawana shida wanajenga kutokana na hela yako.Wachina wanaweza kujenga hata kwa million 50 kwa ramani hiyo ya million 200 kupunguza material.Kupanga ni kuchagua.
 
Contractor wapo humu watakuja, ila Rais Kuna sehemu huwa anapotoka, thamani ya mradi huangaliwa kwenye BOQ na spex zake, mfano mahakama wanahitaji air conditioner,fire alarm na nk,lazima izidi M200 na umbali baina ya mkoa na mko
 
Taarifa ya ikulu inasema Raisi Magufuli amesema Serikali yake....... halafu bungeni wabunge wa ccm wanakanusha mweeee
Nami nimeona kipande kinachosema serikali na sio serikali ya ccm kwani kura aliomba yeye, Urais ni taasis sasa hawa maccm kuiita serika ya ccm wanatoa wapi haya maneno.
 
Back
Top Bottom