Naangalia suala la upungufu a ukosefu wa madawati na vyumba vya madarasa kwa shule ya msingi jimboni Ubungo kwa jicho la 3.
Basically Mhe. Rais katoa agizo na bila shaka utekelezaji wake utafanyika kwa haraka sana.
Binafsi naangalia tatizo la shule kwenye jicho la wawekezaji wa Tanzania wenye shauku/njaa ya kugeuza matatizo yaliyopo Tanzania kama fursa ya kuzalisha.
Ili kuwekeza na kupata cheti cha uwekezaji toka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC; mwekezaji tarajiwa anatakuwa kuwa na yafuatayo
1. Application Letter (hili linawezekana)
2. Filled application form (hili linawezekana)
3. Business Plan (hili linawezekana kwa serious investor)
4. Memart (hili linawezekana)
5. Certificate of Incorporation (hili linawezekana)
6.Tin certificate (hili linawezekana)
7. Evidence of Land (hili linawezekana na tulijadili)
8. Bank statement (hili linawezekana na tulijadili)
9. Board Resolution (hili linawezekana)
10.Payment slip of 1100 USD (hili linawezekana na tulijadili)
Katika mchango kutoka kwa mmoja wa wachangiaji Nd. Magembe alisisitiza umuhimu wa kuwa na
Investment Brokers,
Investment consultants
Investment advisors
Imagine mtu/Mtazania anaweza kuwa solution ya kupata fedha nje ya Tanzania kwa mikipo ya uwekezaji wa riba nafuu.
Na huo uwekezaji ukifanikiwa kama ni wa kiwanda cha maji; (TRA inavuna hela kwenye kila chupa ya maji inayozalishwa) na huenda thamani ya ushuru kwa kila chupa tu thamani ya fedha ni kubwa kuliko USD 1100 au malipo ya kukodi ardhi ambako kungefinya/unapunguza mtaji.
In essence, biashara ya sasa kama mbavyo kwenye mpira wa miguu kuna mawakala wa wachezaji ambao wanafanikisha deals za usajili; ndivyo biashara kubwa zinafanyika.
Kuna waiver inahitajika ila mambo mengine yasonge; kero za kutembeza bakuli kuomba budget support kutoka wizara ya fedha ungepungua kama tunaongeza tax base.
Kero ya kupanda mara kwa mara kwa sukari na mafuta ya kula kama tung'amua Tanzania hapa hapa tuna watu wana IQ ya uwekezaji ila what they need is just signature na certification toka serikalini ili kufanya uwekezaji uwe.
Uchumi mzuri ni uchumi jumuishi ambao ifikie wakati billionaire wanaozalishwa ndani vutu kama madawati ni sehemu ya CSR.
Vitu kama matundu ya choo ni sehemu ya CSR.
Ila kwa upande mwingine TRA akiwa na urafiki na wawekezaji kwa kuelewa changamoto wanazopitia na kukubali kuwasikiza local investors.
Tanzania ya neema itajengwa na local investors wenye vision ya kuleta suluhu kwenye kuzalisha zaidi ndani vitu ambavyo tuna import na ikiwezekana kuongeza export kwenye mataifa 8 yanayoizunguka Tanzania.
Say leo nikihitaji kuwekeza kwenye kuzalisha Sukari, kwanini TIC wasini-guarantee kupata hati ya shamba then ntalipa in the period of 10 years;
Kwanini nihitaji heka 100,000 say kuzalisha mafuta ya kula; kwanini TIC wasiwe sehemu ya kuomba waiver ili uzalishaji wa mafuta ya kula ukuanza then nilipie kodi ya ardhi.
Tukifikiria as innovators, kw model ya Reverse Innovation toka kwa Vijay Govindarajan kuna lots of milestone can be achieved in relatively short time.
Juzi juzi tumezindua referral hospital Chato na Uhuru hospital Dodoma,
Kila mwaka tuna import dawa worth 900bil; je MSD nikiwaomba wanipe purchase Order as a guarantee ili nipate mkopo TIB kwa kuzalisha surgical bandage au surgical cotton au chochote ambacho kutatumika kwenye mifumo ya manunuzi ya madawa na vifaa tiba; mifumo imejiandaa kwenye kuja na inclusive systems in ensuring tuna breed new investors??
Kila la kheri wakubwa.
Tanzania tukiamua; tutafika mbali sana