Majighu2015
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,936
- 3,958
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekwenda Papua New Guinea kumwakilisha tena Rais, John Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 30.
Hii ni mara ya pili kwa Makamu wa Rais kumwakilisha Rais Magufuli, awali ilikuwa Desemba 4, mwaka jana alipokwenda Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa nchi za Afrika na China.
Samia aliondoka jana kuelekea nchini humo, ambako atahudhuria mkutano wa Papua New Guinea utakaotanguliwa na mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za ACP.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais jana kwa vyombo vya habari, ilisema mkutano wa mawaziri utafanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Peter O’Neil.
Makamu wa Rais amefuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushi na wanatarajiwa kurudi nchini Juni 3, mwaka huu.
“Maeneo ya mjadala ni pamoja na kukuza usawa na maendeleo endelevu kwa ajili ya wananchi wa nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya nchi za ACP katika utawala bora na maendeleo, pia masuala ya amani, usalama na utulivu wa kisiasa kama sharti mojawapo kwa maendeleo,” ilieleza taarifa hiyo.
ACP inajumuisha nchi wanachama 79, kati ya hizo, nchi 48 ni za kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, 16 kutoka Caribbean na 15 kutoka Pacific.
Source:Mwananchi
Mytake:
Ni kwamba presidaa wetu kabanwa sana na shughuli za ndani mpaka atume wawakilishi kwenye karibu kila mkutano/mwaliko au kuna jambo limejificha hatulijui?? Mm nafikiri ni vyema raisi ahudhurie hii mikutano unless kuna sababu maalumu.