Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Habari waungwana, leo Rais John Magufuli anaapisha watu kadhaa na miongoni ni teuzi iliyozua rapsha ya wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo ambayo ilimuondoa Nape Nnauye kwenye nafasi yake huku timing ikileta mjadala. Nafasi hio inachukuliwa na aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, Dkt Harisson Mwakyembe huku Palamaganda Kabudi akiiziba nafasi yake anapotoka.

Pia Leo anaapishwa katibu mkuu wa Ikulu ila kwa sasa wanaoapishwa ni mabalozi mbalimbali wanaowakisha nchi zao.
===========

Mawaziri Dkt Harisson Mwakyembe na Palamaganda Kabudi wameshaapa, wanaoapa kwa sasa ni mabalozi wanaonda kuwakilisha katika nchi mbalimbali.
======

Anaeongea kwa sasa ni Rais Magufuli na kuwapongeza wote walioteuliwa. Amewaambia wasitegemee mazuri sana kwa kazi huwa zina lawama hasa kwa Tanzania ambapo kuna grupu la watu wao siku zote ni kulalamika.

Amedai Mwakyembe mitandao ilisema asingekuja kuapishwa pia wapo walioposti kuwa Kinana angeongea leo ilhali yeye kamtuma India kwa matibabu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…