Rais Magufuli avuruga wengi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
STAILI ya Rais John Magufuli kutimua watumishi wa umma kwa ‘munkari’ inawavuruga watu wengi ambapo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya, anaandika Regina Mkonde.

Kabla ya LHRC kuonya, Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea uraas kupitia Chadema na kuungwa mkono na Ukawa pia Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini walionya staili hiyo na kushauri taratibu za kisheria za utumishi wa umma zifuatwe.

Helen Kijo Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ameikumbusha serikali kufuata sheria za utumishi wa umma katika kuwawajibisha watumishi wanaotuhumiwa kufanya makosa.

Bisimba ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2015 uliofanyika jijini Dar es Salaam, MwanaHALISI Online lilishuhudia.

“Inafahamika kwamba, Rais John Pombe Magufuli ameikuta nchi sehemu mbaya na anahitaji kuirekebisha.

“Ila ni vema akafuata taratibu za kisheria wakati anapotaka kumtumbua mfanyakazi aliyeajiriwa na serikali ambayo ndiyo anayoiongoza,” amesema Bisimba.

Anaeleza kuwa, Rais hakuchukua uamuzi wa busara kwa kumsimamisha kazi Wilson Kabwe, aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam mbele ya hadhara na kwamba, alitakiwa kufanya uamuzi huo kwa kufuata sheria.

“Makonda (Paul Makonda) hakuwa na sababu za kumsema Kabwe mbele ya hadhara, alitakiwa afuate utaratibu, si maanishi kuwa namtetea Kabwe, bali kutokana na agizo la rais alilotoa la kusimamishwa na kufanyiwa uchunguzi, je atakapobainika kuwa ni msafi ataweza kumsafisha?” anahoji.

Bisimba amewataka Watanzania waache unafiki kwamba, wapo baadhi ya wanasheria wanaojua taratibu za kumsimaisha kazi mtumishi wa umma lakini walishindwa kumshauri badala yake waliacha aendelee na uamuzi wake.

“Mfano jana alikuwa anauliza wananchi, nimtumbue nisimtumbue, mbele ya hadhara, huyo aliyekuwa anamfanyia hivyo ni mtumishi aliyeajiriwa na serikali, isitoshe Kabwe ninavyomjua ni mgonjwa, je angepata matatizo ingekuaje?” anauliza.

Bisimba pia ametolea mfano wa hatua iliyochukuliwa wakati wa kufukuzwa kazi Anne Kilango Malecela, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwamba, aliju akwamba amefukuzwa kazi baada ya kupigiwa simu akiwa ofisini.

“Kilango alitumbuliwa wakati alipokuwa ofisini, alipigiwa simu ili kujibu baadhi ya maswali juu ya kufukuzwa kwake, cha kustajaabisha hakuwa na taarifa kama alifukuzwa kazi na rais,” amesema.

Amesema kuwa, mfumo wa utumishi mbaya ulianzishwa na serikali baada ya kuuondoa mfumo wa ujamaa na kuuweka mfumo wa ubepari.

Kwa upande wa sheria anasema, zipo nzuri ila nyingi kati ya hizo zinahitaji maboresho na kwamba, inahitajika Katiba Mpya ili ifanyike marekebisho ya sheria zilizoachwa na mkoloni.

Aidha, ripoti iliyotolewa leo inaonesha kuwa, uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015 ulikuwa huru japo kulikuwa na wasiwasi wa kutokuwa na haki kutokana na madai ya kuibiwa kura.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa, kwa mujibu wa uangalizi uliofanywa na LHRC umebaini kuwa, elimu ya uraia haikutolewa vizuri, watu wenye ulemavu walipata shida kufika maeneo ya kampeni na kutumika kwa vifaa vya serikali wakati wa kampeni hasa magari pamoja na uchelewashaji wa kutangaza matokeo katika vituo mbalimbali.
 
Hivi bado Kuna watu wanaoamini kuwa suluhisho la matatizo yetu ni kurudisha ujamaa??

Wafanyakazi wanakuwa wabadhirifu kutokana na mishahara midogo isiyokidhi mahitaji pamoja na tamaa za viongoz kujilimbikizia Mali....wenyewe wanasema usipokula wenzio watakula.........


Tatizo kubwa ni system mbovu na kuwa na katiba yenye mlengo wa chama kimoja cha Siasa......hayo mengine ni ziada Tu...
 
Former President Jerry Rawlings has admitted that some of the Military Officers who were extra-judicially killed in the 1979 uprising were innocent.

The former Military leader told students in the Volta region where he spoke as the Guest of honour at the closing ceremony of the regional camp of the International Youth Fellowship at the Adidome Senior High School that: “We had no choice. We thought let two go. Acheampong and a certain Utuka, very corrupt Generals. They were sacrificed. It was not enough. Ladies and gentlemen, 10 days later, we had to sacrifice another six and some of the Commanders were innocent good people but it had to be done because the rage in the country was too high, too much”.
Source: African Spotlight
 
Nimeskia clip ya mwl.jk Nyerere(RIP)ni kama alijua kuna mtumbuaji sinayo hapa kama kuna mtu anayo aweke tuskilize
 
Kwa issue ya Wilson Kebwe, Bi Simba ana hoja lakini kwa Anne Kilango hapana. Anne Kilango sio mtumishi bali kateuliwa na rais kwa hiyo she was serving at the pleasure of the president. Vyeo vinavyongukia kwenye kundi la Anne Kilango wanaweza kuondolea bila hata ya kutoa sababu. Ndivyo ilivyo duniani kote.

Na huyo Kebwe ni kitu gani hakijulikani kuhusu utendaji wake?
 
Utumbuaji uendelee lakini mbwembwe na kubeza so vizuri hasa unaposubiri taratibu za kisheria
 
"isitoshe Kabwe ninavyomjua ni mgonjwa.."

Nawahurumia wasio julikana sijui nani atawatetea
 
Shauri yake kama ni mgonjwa anaibaje? Au hajui sheria za mikataba ? WATUMBULIWE TU MAANA HAKUNA NAMNA NYENGINE
 
namuunga mkono bisimba hekima no kitu muhimu sana raid hakupaswa kufanya vile yeye ni MTU wa mwisho ila kwa Jana ameonyesha upungufu kwa kuwauliza watu kuwa eti wanaotaka nitumbue wanyoshe vidole naona so busara no bora kufuata taratibu za kiutumishi zifuatwe
 
Mbona Mwaka jana wakati Kabwe analalamikiwa Bungeni Huyo Bisimba hakujitokeza?

Mh. Rais mimi ni UKAWA ila Nakuunga Mkono, maana haya ndio tuliyokuwa tunayataka wapinzani, sasa nashangaa hata baadhi ya wapinzani wanapinga, nadhani wapinzania kwa sasa hatujui nini tunachosimamia.
Ushasema wapinzani kwahiyo sie lazima tutafute lolote lile la kupinga ili tuonekane tupo tofauti,maana hivyo ndio tunaamini tutachukua nchi.
 
Back
Top Bottom