Rais Magufuli atua Songwe na ndege rasmi ya Rais

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,177
October 4, 2019
Songwe International Airport.

Mh. Rais Magufuli awasili mkoani Songwe kwa kutumia ndege aina ya Gulfstream G550 jet, ndege hii ni rasmi kwa matumizi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye uwezo wa kubeba abiria 18 imesajiliwa kwa namba 5H-ONE . Katika ziara zake zingine za ndani ya Tanzania Mh. Rais alikuwa anatumia ndege kubwa aina ya Airbus a220-300 iliyokodishwa kwa Air Tanzania yenye uwezo wa kubeba abiria 130 - 160 .

Video : NDEGE RASMI YA RAIS WA TANZANIA Gulfstream G550 Jet ikitua ktk uwanja wa Songwe international Airport

Source : Millard Ayo
Uwanjani hapo Mh. Rais alipokewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, Naibu Spika Bi. Tulia Ackson na Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi.

Katika ziara hiyo Mh. Rais anatazamiwa kuzindua miradi kadhaa katika mkoa huo uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
 
Hongera Rais wa vyama vyote CCM, ACT, CDM, CUF, TLP, CHAUMA, nk..

Naona vyama vingine wameingia mitini ni CCM tu pekee ndio wametokea, Maendeleo hayana chama..
 
October 4, 2019
Songwe International Airport.
NDEGE RASMI YA RAIS WA TANZANIA Gulfstream G550 Jet, hii yenye uwezo wa kubeba abiria 18 imesajiliwa kwa namba 5H-ONE. Mh. Rais Magufuli aliwasili mkoani Songwe kwa kutumia ndege aina ya Gulfstream G550, kuanza ziara rasmi ya kikazi. Katika ziara zake zingine za ndani ya Tanzania Mh. Rais alikuwa anatumia ndege kubwa aina ya Airbus a220-300 iliyokodishwa kwa Air Tanzania yenye uwezo was kubeba abiria 130 - 160 .

Source : Millard Ayo
Uwanjani hapo Mh. Rais alipokewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, Naibu Spika Bi. Tulia Ackson na Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi.
Katika ziara hiyo Mh. Rais anatazamiwa kuzindua miradi kadhaa katika mkoa huo uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Kusini si salama kwa ATCL makaburu wana mkono mrefu.
 
Katika kutembetembea kwangu duniani rais anapokelewa na watu wachache sana kwenye uwanja wa ndege kwenye nchi yake na anaenda kukuta upokezi mwingi kule anakoenda kuhutubia. Sikutegemea hata kuona vikundi vya ngoma hapa. Pamoja na kwamba Raisi anafanya mambo mazuri lakini kwa hapa kupokelewa na umati huu wote tunarudi kule kwa mwalimu Nyerere. Lakini labda ndivyo ilivyo kwa kila anakotembelea.
 
October 4, 2019
Songwe International Airport.

NDEGE RASMI YA RAIS WA TANZANIA Gulfstream G550 Jet, hii yenye uwezo wa kubeba abiria 18 imesajiliwa kwa namba 5H-ONE. Mh. Rais Magufuli aliwasili mkoani Songwe kwa kutumia ndege aina ya Gulfstream G550, kuanza ziara rasmi ya kikazi. Katika ziara zake zingine za ndani ya Tanzania Mh. Rais alikuwa anatumia ndege kubwa aina ya Airbus a220-300 iliyokodishwa kwa Air Tanzania yenye uwezo was kubeba abiria 130 - 160 .

Source : Millard Ayo
Uwanjani hapo Mh. Rais alipokewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, Naibu Spika Bi. Tulia Ackson na Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi.

Katika ziara hiyo Mh. Rais anatazamiwa kuzindua miradi kadhaa katika mkoa huo uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Anaogopa kupanda airbus baada ya engine zake kuanza kuharibika
 
Back
Top Bottom