Rais Magufuli atoa siku 7 anataka majibu ni kwa namna gani dawa zitaongezwa katika hospitali ya Masumbwe, Mbogwe na maeneo mengine

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo wampe majibu ya kwa nini Mkoa wa Geita wanapunjwa madawa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo akizindua vituo vya afya vya Masumbwe na Mbogwe mkoani Geita ambapo alisema mwaka 2015 bajeti ya madawa mkoa wa Geita ilikuwa bilioni 2.35 mwaka 2020 ilikuwa bilioni 2.75.

Amesema anataka majibu ni kwa namna gani dawa zitaongezwa katika hospitali ya Masumbwe, Mbogwe na maeneo mengine.

"Inawezekana kuna upunjaji wa mgawo wa madawa katika Mkoa huu ikiwemo Masumbwe, bajeti ya madawa imeongezeka lakini madawa yanayotolewa hapa ni kidogo, Waziri wa Afya na wa TAMISEMI mnaopanga bajeti ya madawa mkakae ndani ya siku saba mlete jibu, "amesisitiza

Aidha Rais Magufuli amewashukuru wana Masumbwe na Mbogwe kwa kumpigia kura nyingi.

"Nawashukuru wana Masumbwe na wana Mbogwe kwa kura nyingi sana mlizonipa na kuniwezesha kuwa Rais, mlinipa mimi mkampa na Maganga awe Mbunge wa jimbo hili na mkawapa kura nyingi sana madiwani wa CCM asanteni sana"-
 
Nawashukuru wana Masumbwe na wana Mbogwe kwa kura nyingi sana mlizonipa na kuniwezesha kuwa Rais, mlinipa mimi mkampa na Maganga awe Mbunge wa jimbo hili na mkawapa kura nyingi sana madiwani wa CCM asanteni sana"-
Anamdanganya nani huyu?
 
kuna mikoa naona haitokaa itembelewe hadi mwisho wa muhula huu

Je nayo inafikiriwa katika uboreshwaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi?
 
Siasa kitu kibaya sana,unaagiza mwenyewe budget ichotwe ipelemwe kwenye stigglers halafu unawataka uliowaagiza mwenyewe wachote pesa kupeleka kwenye ujenzi wa stigglers wajieleze kwanini dawa hazitoshi.

Yani yote ni kutaka uonekane wewe mwema sana wengine si wema wakati ukweli tatizo ni wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom