Rais Magufuli atoa dola 20,000 kusaidia matibabu ya Ruge Mutahaba mkurugenzi wa CMG

Haya mzee ngoja niishike vizuri....Hivi Clouds Media hawana Bima ya Afya kwa wafanyakazi wao?Hivi Ruge yuko Mahututi kwa ile sumu alopewa?Hivi Ruge ametangaza kwamba anaomba mchango wa matibabu.Hivi unajua dola 20,000 ni sawa na milion 50 so angefanya tu kukipa hata kijiji kimoja kutimiza ahadi yake ya kampani badala ya kumpa yote hio mtu mmoja.Hamuoni kama mnaposhangilia upuuzi kama huu na ninyi mnazidi kupuuzwa?
Acha roho mbaya
Mimi pia simpendi magufuli ila hapa hajafanya kosa
 
Wenye matatizo ya kusaidiwa nchi hii ni wengi, kila siku ukiangalia taarifa ya habari watu wanaomba msaada wa kupelekwa india. Awasaidie wote basi, kwa sababu sababu hizo anazotoa sio fedha zake ni fedha zetu ,yeye pale ikulu hakuna biashara yoyote anayoifanya . Kwa hiyo awasaidie wote akiona tangazo kwenye matv ajitokeze kusaidia .halafu kinachonishangaza ni hiki cha kumsaidia mtu halafu unamtangaza,huo msaada hauna baraka za Mungu
 
Pole sana kamanda hela ni yake usimpangie....na yeye ndio mmiliki wa hela zote nchini hahahaha nakuona tumbo linavyo kuuma na jaziba juu... Umwa na wewe uchangiwe kama unaona wivu
Hela ni zake au za wananchi..hivi una akili kweli wewe bwana mdogo??
 
Rais Magufuli ametoa usd 20,000 karibia sh 50 milioni za Tanzania kuchangia mfuko wa matibabu ya mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group.Sebastian Maganga wa CMG amesema hali ya Ruge inaendelea vizuri na amewataka watanzania wenye mapenzi mema kumuombea katika sala zao.Pia Maganga amemshukuru sana Rais Magufuli kwa upendo aliouonyesha.Source Clouds 360
Watanzania wangapi wanaumwa na wanaitaji misaada?kunawatu wanaumwa na pesa za kula na matibabu hawana hizo pesa raisi angezipeleka muhimbili angesaidia watu wengi zaidi
 
Pole sana kamanda hela ni yake usimpangie....na yeye ndio mmiliki wa hela zote nchini hahahaha nakuona tumbo linavyo kuuma na jaziba juu... Umwa na wewe uchangiwe kama unaona wivu
Rais hamiliki hela acha ujinga pesa ni za nchi

By the way yuko sahihi kutoa msaada huo
 
Wenye matatizo ya kusaidiwa nchi hii ni wengi, kila siku ukiangalia taarifa ya habari watu wanaomba msaada wa kupelekwa india. Awasaidie wote basi, kwa sababu sababu hizo anazotoa sio fedha zake ni fedha zetu ,yeye pale ikulu hakuna biashara yoyote anayoifanya . Kwa hiyo awasaidie wote akiona tangazo kwenye matv ajitokeze kusaidia .halafu kinachonishangaza ni hiki cha kumsaidia mtu halafu unamtangaza,huo msaada hauna baraka za Mungu
Mbwiga nani katangaza?!
 
Sawa anaweza kuwa anaumwa kweli, hivi ni kweli Ruge amekosa pesa ya matibabu??? Kuna watanzania wanakufa kwa kukosa ata laki mbili hii ni aina nyingine ya kushindwa kuangalia vitu kwa umakini.

Ata angeamua kuchangia siyo lazima atangaze maana wapo ambao ata hawawezi kulipia malipo mhimbili wamezuiliwa kuondoka.
Je kama inaitajika mill 200
Then magufuli katoa 50 the rest katoa ruge mwenyewe ?
 
Back
Top Bottom