Rais Magufuli atengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo

Siyo lazima kila ukishawishiwa ukubali ushawishi, kwa hadhi ya kazi na uwakilishi aliokuwa nao katika ngazi ya Kimataifa bado alikuwa ni kama Mbunge tena ngazi ya Kimataifa. Lakini hata kama Mhe. JK alimshawishi kwa awamu ya kwanza, awamu ya pili ili kulinda hadhi yake alipaswa kuacha kugombea ili ateuliwe tena. Aidha, hata kama angeshinda au kuteuliwa, yeye kama Mtalaam aliyebobea katika Sekta ya Madini, baada ya kukabidhiwa Wizara, alipaswa kung,amua upungusu uliopo na kumshauri Mhe. Rais haraka sana bila kusubiri Tume. Inafahamika kabisa kuwa huo upungufu haukuanzia kipindi chake, lakini yeye ina maana alikuwa hajui ilhali Wapinzani walikuwa wakiusema sana ? Mbona Mhe. Rais yeye alikuwa anaufahamu ila kwa kuwa hakuwa na maamuzi ikiwa inashindikana, ndo maana baada ya kuona Mawaziri hawachukui hatua, kaamua kuchukua hatua mwenyewe ya kwanza ikiwa ni kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu. Acha kutetea watu wazembe, wenye majivuno wanaondekeza kupiga makokofi Bungeni na kusema Ndiooooooooo. Hapa Tumpe Hongera Mhe. JPM.
Umenena vema ila umemaliza kwa hisia,unasema rais hakuwa na maamuzi ...sawa...waziri yeye maamuzi anayapata wapi???Tukirudi nyuma JPM alikuwepo ktk cabinet kwa miaka 20 na prof kwa miaka kama minne hivi...kwa hiyo mkuu ana uelewa mkubwa Zaidi ya haya mambo toka zama hizo ingawa itasemwa hakuwa katika wizara husika ila ndio kimsingi waliohusika kupitisha na kubariki yote hayo!!!Kuna mambo lazima uyaingie strategically na sio kwa pupa...!!!
 
Back
Top Bottom