Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla. DC wa Tunduru, Juma Homera ateuliwa kuwa RC mpya

Nimeelewa kwa nini kwenye misiba wengine wanalia sana. Kumbe ni wanalizwa na mengi nje ya msiba,, njombe here we come
Njombe ni suala la muda tu, mkuu wa mkoa akae mkao wa kutumbuliwa. Wakati wa ziara yake Njombe, alipomtumbua OCD na kumrejesha hapo hapo, alimstahi sana Ole Sendekea.Sababu zinazomfanya afeli ni
1. Mauaji ya kishirikina ya watoto
2. Kuchelewa kukamilika kwa kituo kikuu cha mabasi
 
Awamu hii tutaona mengi, kwangu Mimi Makalla ni kiongozi makini saana tena mwanadiplomasia, yupo makini sana kwenye maamzi yake. Lakini Leo kapigwa chini, daaa hii ni shida!
Anafanya Maandalizi ya Kurudisha Jimbo Lake
 
Walikuwa wanaotesha mikoa kama uyoga na kuwaongezea mzigo walipa kodi. Mikoa kati ya 6 mpaka 10 inaweza kuunganishwa ili kupunguza gharama au kuwa na magavana watano au sita tu to take of the whole country.

Katavi wanamuonea bure mkoa karibu 60% ni hifadhi sehemu za biashara ni chache mno.
Mkoa hauna hata lami ya kuingia mkoani
Bora akapumzike tuu kuliko hizi presha
 
Aaaaaaaaah! Hivi Jiwe amewahi kufika Katavi? Kule wamejaa wafugaji na wakulima tu. Sasa unaweza kuwagawia vitambulisho wafugaji na wakulima? Mfano, mmasai utampa kitambulisho cha ujasiriamali?
Wale wasaidizi wake wapeleka taarifa wameshamdanganya sultani wao na huwa hawasemi mambo kama hayo maana sultan nae hashauriki
 
nahisi ni kutokana na wana Mbeya siku ile ya malumbano ya hoja ya ITV kumsifu Makalla na kumponda Chalamila.

si unajua kina hamnazo kama Bashite, Happy & Chala ndiyo dizaini ninayoitaka?

Hiyo ndio sababu halisi. Kumbuka pia kuwa Makala hakulazimisha ushindi kwenye chaguzi za marudio za madiwani na ccm ikapata inachostahili.
 
Jamaa aliyeteuliwa haki ya Mungu ataogesha hadi watoto na tutamuona kwenye matv....Ni type ya kina Bashite, Hapi, Olesabaya, Chalamila yani ni mulemule. Naona Jiwe kapiga kona kali kwa Ole Sendeka kaenda kutua Katavi. Naona Ole kaachwa achwa ili machungu ya kufiwa na kaka yake yapoe kwanza ila kiuhalisia ananing'inia ile kishenzi.
 
Back
Top Bottom