MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
VIDEO:
Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
Rais ameongea na ''vijana wa kijiwe'' kuhusu hali ya maisha na matarajio yao katika utawala wake.
''Vijana wa kijiwe'' wamemshukuru sana kwa kuwatembelea na ''kupiga story'' lakini pia wameshangaa sana kwa sababu hawakutegemea kama angeweza kuwatembelea tena baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Mmoja wa vijana alisikika akisema, ''Rais tumekumiss''. Rais alijibu na kusema, ''hata mimi nimewamiss mno''.
Wamemuomba asiache kuwatembelea kila anapopata nafasi ya kufika Chato ili waendelee kumueleza hali halisi ya maisha na mafanikio yao kama walivyokuwa wanafanya kabla hajachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Rais amewaambia serikali yake inafanya kila linalowezekana ili kuwajengea mazingira bora zaidi ya kupata kipato halali lakini pia waendelee kuchapa kazi halali.