Rais Magufuli atashinda tuzo ya Mo Ibrahimu miaka 10 ijayo

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,201
3,322
Wanabodi
Salaam;

Kasi aliyoanza nayo Rais wa awamu ya 5, kama ataendelea nayo na kuyafanya kwa vitendo yale anayoyaahidi kwa hakika ataitwa tuzo ambayo imekosa mshindi kwa sasa.

Viongozi wengi wa Africa wameshindwa kudhibiti ufisadi, rushwa na utawala bora. Kama atatenda sawa na kauli zake, naamini atakuwa mshindi ajaye wa tuzo hiyo ya mamilioni ya dollar.

Natamani sana afanikiwe ingawa hakupata kura yangu lkn hii nchi ni yetu sote. Kama atasimamia yale ambayo tumekuwa tukiyapigania hatuna sababu ya kumpinga.

Haya ni maoni yangu binafsi na matarajio yangu kwake.

Nawasilisha.
 
Mna kivimbisha sana kichwa cha huyu mtu mpaka mtakipasua bure! Tuzo za MO hazitolewi kwa mtu eti kwa sababu katimiza wajibu wake, ni zaidi ya hapo. Jee hayo ya zaidi ya hapo ni yepi mmeona kayafanya?
 
Wala kutumbua majipu si moja ya vigezo!
 
Mna kivimbisha sana kichwa cha huyu mtu mpaka mtakipasua bure! Tuzo za MO hazitolewi kwa mtu eti kwa sababu katimiza wajibu wake, ni zaidi ya hapo. Jee hayo ya zaidi ya hapo ni yepi mmeona kayafanya?
Mkuu Chakaza wengine kwa kufanya hivi tunadhani itampa nguvu zaidi ya kuyatenda na kuyasimamia yale anayoamini.
Ni kweli ile tuzo vigezo vyake ni zaidi ya kukuza uchumi,utawala bora nk. Lkn pia huwezi kuipata kwa kuyaacha hayo..! Miaka 10 ni mingi sana,hii ni nchi yetu sote hata wale tunaotaka mabadiliko,lkn kwa sasa uchaguzi umeisha huyu ndiye tuliyenae na nnaamini km tutakuwa wazima,atakuwepo kwa miaka 10! Acha tumuongezee nguvu.
 
Last edited by a moderator:
Na zaidi ya hapo ufisadi rushwa wezi matumizi mabaya fedha za Serikali.Isitoshe hanunuliki na wala Haongeki aliwapa LIVE Wafanyabiashara Ikulu.Vyama vyote vya Siasa vyake habagui wala hachagui .Mnataka nini Jopo la MO limeanza kumwangalia .Ilianza Msumbuji zaidi ya miaka kupita Tanzania hiyo ni JPM
 
Mkuu Chakaza wengine kwa kufanya hivi tunadhani itampa nguvu zaidi ya kuyatenda na kuyasimamia yale anayoamini.
Ni kweli ile tuzo vigezo vyake ni zaidi ya kukuza uchumi,utawala bora nk. Lkn pia huwezi kuipata kwa kuyaacha hayo..! Miaka 10 ni mingi sana,hii ni nchi yetu sote hata wale tunaotaka mabadiliko,lkn kwa sasa uchaguzi umeisha huyu ndiye tuliyenae na nnaamini km tutakuwa wazima,atakuwepo kwa miaka 10! Acha tumuongezee nguvu.
Mkuu magole tutamsaidia na kumwongeza nguvu kwa kumwambia ukweli tupu. Akifanya vizuri tumpongeze kwa kiasi kinachostahili na akikosea na kuvurunda tumpe za uso mpaka aione ofisi ile sio ya mzaha. Makosa yaliyofanyika kwa mtangulizi wake ya kumvisha kilemba cha ukoka leo tunaona madhara yake.
afanye kazi yake kwa bidii maana ameiomba mwenyewe na sisi tumempa. Pia kwa kazi hiyo ni kama tiketi ya maisha ya uhakika na familia yake mpaka mwisho wa maisha yake hata baada ya kustaafu sasa kwa nini naye ailetee dharau? Lazima awajibike vema na ataona akipendwa na kila raia mwema.
 
Last edited by a moderator:
Magufuli anaweza kuja kupata hiyo tuzo ya Mo Ibrahim iwapo Kikwete hatamuwekea kiwingu cha kung'ang'ania kuwa mwenyekiti wa ccm mpaka 2017!!! Akimuachia uenyekiti mapema hapo atakuwa na nafasi ya kutimiza yale aliyoahidi ama sivyo itakuwa ngumu sana kushinda.
Hivyo basi kikwazo cha Magufuli kupata tuzo ya Mo Ibrahim ni kuendelea kwa DHAIFU kuwa Kiongozi wa ccm!!
 
Wanabodi
Salaam;

Kasi aliyoanza nayo Rais wa awamu ya 5, kama ataendelea nayo na kuyafanya kwa vitendo yale anayoyaahidi kwa hakika ataitwa tuzo ambayo imekosa mshindi kwa sasa.

Viongozi wengi wa Africa wameshindwa kudhibiti ufisadi, rushwa na utawala bora. Kama atatenda sawa na kauli zake, naamini atakuwa mshindi ajaye wa tuzo hiyo ya mamilioni ya dollar.

Natamani sana afanikiwe ingawa hakupata kura yangu lkn hii nchi ni yetu sote. Kama atasimamia yale ambayo tumekuwa tukiyapigania hatuna sababu ya kumpinga.

Haya ni maoni yangu binafsi na matarajio yangu kwake.

Hii ni ndoto ya mchana.
 
Back
Top Bottom