OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,075
- 114,599
Kama tunavyokumbuka rais Magufuli alianza kwa kuyapuuza tena majukwaani mafanikio ya Awamu ya nne. Kuupuzwa huko kuliitikiwa na baadhi ya Mawaziri na viongozi wengine wa kisiasa ikiwepo Mh.January Makamba, Mh.Paul Makonda, Mh.Mwakyembe na wengine. Mheshimiwa Magufuli. Mbele ya rais mstaafu Jakaya Kikwete na mbele ya wahudhuriaji wa uzinduzi wa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam rais Magufuli alisema Kikwete alimwachia hewa nyingi ''ukigeuka huku barabara hewa, kule wanafunzi hewa, pale watumishi hewa, kila kitu ni hewa''- Nilipata uchungu kwa jinsi uso wa Kikwete ulivyobadilika.
Lakini sasa mda umejibu...........ni mwaka na ushei umepita bado rais anazungumza mambo yale yale kana kwamba maeshika madaraka jana. Ni mwendo wa matamko na Opereshini zisizo na hatma yeyote. Huku muhimili wa bunge ukivunjiwa heshima na muhimili ambao mizizi yake imejichimbia sana. Hata hivyo serikali imefanya vyema katika kamatakamata ya viongozi wa upinzani.
Baadhi ya mafanikio ya Awamu ya Nne ambayo kwa kiwango fulani taifa lilipiga hatua, tofauti na sasa taifa linapiga hatua kurudi nyuma;-

- Utoaji wa Mikopo wanafunzi wa elimu ya juu
- Ongezeko angalau la mishahara ya watumishi wa umma. Capacity building kwa watumishi wa umma mfano utoaji wa semina na fedha za mafunzo
- Ujenzi wa Miundombinu mikubwa mfano barabara za lami, barabara za mwendo kasi, daraja la Kigamboni
- Kuheshimu separation of power kwa mihimili ya nchi Bunge, Mahakama na Serikali
- Sera za Mambo ya nje inayoeleweka iliyofanya heshima ya Tanzania kuwa kubwa kimataifa
- Umoja na Utengamano miongoni mwa Wananchi. Angalau vyama pinzani na tawala viliweza kukutana na kutafuta maridhiano. Rais aliheshimu matamko ya wapinzani wake kisiasa
- Bunge kuonekana live huku wananchi wakipata nafasi ya kuona uwakilishi wa wabunge wao.