Rais Magufuli anatuongoza kwenye njia sahihi kama sisi Waafrika

big IQ

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
491
890
Rais Magufuli anatuongoza kwenye njia sahihi kama waafrika. Anatuongoza kwenye njia ya kujitambua na kujiamini, tuna namna yetu ya kujiongoza kabla ya watu weupe hata kabla ya ma missionary pamoja na waarabu wa kwanza. Watu weupe wameleta utaratibu wao wa maisha kiasi kwamba desturi zetu za mwanzo zimegeuka ushirikina, dhambi na ushamba!

Hatuna Uhuru, sasa tunapogombea Uhuru wetu wa kweli bila kuingiliwa tunakwazwa na ukoloni wa kiuchumi. Sikuhizi hatupigani mabomu. Sayansi na technologia ndio silaha kubwa kwenye Karne hii. (Ubaya vita vya mataifa makubwa havitutengi sisi, lazima tuathirike).

Ni juu yetu kuamua kucheza ngoma moja na kuendelea kuwa watumwa wajinga au kucheza ngoma iliopo kwa namna yetu na kuwa watumwa wanaojielewa walio tayari kwa UHURU WA KWELI. Roma haijaiemgwa kwa siku moja,Wala hajajengwa kwa jasho tuu,Machozi na Damu pia yalihusika,muhimu kujua tupo kwenye vita. (MUHIMU KUJUA TUPO KWENYE VITA).Na namwamini Meko anapotupeleka nipo tayari kumfata kiongozi wangu mwenye maono ya Kiafrica.

Leo hii Raisi asipoenda magharibi ni mgonjwa wa moyo (mmesahau maneno yenu miaka 7 iliyopita?).

Leo hii Raisi asipoongea kiingereza fasihi anasemwa(huu ndio Uhuru?).

Leo hii Raisi akiwa na doupt na chanjo zinazotoka nje tunatukana kana kwamba aliewakata mikono mababu zetu kwenye mashamba ya mkonge sio hao wazungu.(huu ndio uzalendo?).

To cut it clear hakuna chanjo itakayopokelewa wala hakuna lockdown. HIVYO NDIVYO MNAVYOONGOZWA,FULLSTOP.
 
Naunga hoja
IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Wewe una uhuru wa kupenda / kuona kitu fulani kipo sahihi, vilevile wape fursa / nafasi wengine wanaoona kwamba unapotoka / upo nje ya mstari.

Tofauti na hapo ni dictatorship.
 
Wewe una uhuru wa kupenda / kuona kitu fulani kipo sahihi..., vilevile wape fursa / nafasi wengine wanaoona kwamba unapotoka / upo nje ya mstari...

Tofauti na hapo ni dictatorship....
Maendeleo hayaji kwa kubaki njiapanda huku mnashauriana,it takes a hero to lead you all through one right way no matter what
 
Maendeleo hayaji kwa kubaki njiapanda huku mnashauriana,it takes a hero to lead you all through one right way no matter what
What is to lead ?, Kufikiri kwa niaba yako ?, kwamba kila anachosema ni sawa ?

Nchi haiendeshwi na mtu / bali misingi huyo mtu ni kuhakikisha misingi hio inatekelezwa..., Na hilo ni kwa kushirikiana na wadau pamoja na wataalamu..., sio my way or the high way...
 
Asante mleta mada....kipimo cha utu wetu, Uhuru wetu, imani yetu, nk eti lazima kikubaliwe kwanza na wazungu ndio tuamini kuwa tupo sahihi! Wakati wenyewe wazungu wapo wanajiuliza wapi walikosea hadi kuwa hivi walivyo (mifano ipo mingi) sisi tunatafuta sababu za kutaka kuwa kama wao....

Bwana Andrew Cuomo gavana wa New York wengi tulimfahamu wakati wa mlipuko wa covid-19, kwa umakini wake aliounyesha katika mapambano makali ya mlipuko, ilifika hatua wamarekani walihoji kama jamaa anataka kuwa rais wa Marekani kwababu ya bidii yake!

Utamaduni wa wenzetu tunaotaka kufanana nao ili tuwe "bora" wameanza kumuibulia visa, anatokea mama mtu mzima anasema Cuomo alitaka kunibusu....kwa akili zangu za asili najiuliza muda wote ulikuwa wapi hadi unakuja kushtaki leo?
 
What is to lead ?, Kufikiri kwa niaba yako ?, kwamba kila anachosema ni sawa ?

Nchi haiendeshwi na mtu / bali misingi huyo mtu ni kuhakikisha misingi hio inatekelezwa..., Na hilo ni kwa kushirikiana na wadau pamoja na wataalamu..., sio my way or the high way...
Misingi unayoizungumzia ni ipi?and why?wadau unaowazungumzia ni wapi and why?
 
Usipotembea mwenyewe tutakuburuza,ila tutafika wote kama watanzania

Unamaana kwa kubaka.

Serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali zinawajibu wa kukidhi matakwa ya watu.

Si kulazimisha au kubaka watu.
 
Asante mleta mada....kipimo cha utu wetu, Uhuru wetu, imani yetu, nk eti lazima kikubaliwe kwanza na wazungu ndio tuamini kuwa tupo sahihi! Wakati wenyewe wazungu wapo wanajiuliza wapi walikosea hadi kuwa hivi walivyo (mifani ipo mingi) sisi tunatafuta sababu za kutaka kuwa kama wao....
IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Misingi unayoizungumzia ni ipi?and why?wadau unaowazungumzia ni wapi and why?
Misingi ni yoyote ambayo jamii husika imejiwekea (mfano kwa sasa kuna separation of power (mihimili tofauti) kutokuingiliana hili linasaidia check and balances na mtu mmoja kutokuvuka mipaka...

Misingi tuliyojiwekea watanzania mpaka hivi sasa ni kuwa sisi sote ni ndugu, hakuna ukabila, udini wala uchama sio wa kututenganisha..., hivi sasa imekuwa sifa kupeleka kila kitu ulipozaliwa eti utazikwa huko (inaleta precedent ya kila atakayekuja kujenga kwao na watu kuchagua wa kwao ili ajenge kwao)...

In short kwa muda mfupi sana tumevunja misingi ambayo watanzania tulikuwa tunajivunia na ambayo ilikuja kwa gharama kubwa sana (umimi na ukwetu; sisi na wao; tumefanya hawajafanya) yaani kiongozi ni wa Chama na sio wa Walipa Kodi ambao hao ni Watanzania...

Wadau ni wataalamu na wahusika wote huwezi kufanya vitu bila kuwauliza wataalamu ambao hao ndio kazi zao (hilo jambo ndio maisha yao) kwamba tunafanyaje..., na mipango yote lazima iwe long term sio mashindano ya kwamba nimefanya hiki na kile...., Na mipango hio lazima iangalie factors zote (economic, social na environmental)....

In short kujenga kila mtu anaweza kujenga ila ukivunja misingi itachukua generations kuweza kuirudisha.
 
Back
Top Bottom