mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 815
- 733
Spika wa Bunge Job Ndugai ametangaza mabadiliko ya ratiba ya shughuli za Bunge ambapo Bajeti Kuu ya Serikali itasomwa June 11, 2020 na shughuli za Bunge zitamalizika June 19, 2020 .
"Tunamaliza shughuli za Bunge June 19,2020 ambapo panapo majaliwa Rais anaweza kuja kutufungia Bunge la 11 rasmi"-NDUGAI
Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania
SHUGHULI za Bunge la 11 nchini Tanzania, zinatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 19 Juni 2020 kwa Rais John Magufuli kulihutubia. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 18 Mei, 2020, na Spika Job Ndugai, wakati anazungumza na wanahabari jijini Dodoma kuhusu maazimio ya kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge, kuhusu tathimini ya shughuli za mhimili huo.
Lakini Spika Ndugai amesema mabadiliko ya ratiba hiyo, yametokana na mabadiliko katika vikao vya mabunge ya nchi za Afrika Mashariki.
Amesema, nchi za Afrika Mashariki zina desturi ya kusoma bajeti zao siku moja, mawaziri wa fedha wa nchi husika wamekubaliana kusoma bajeti zao tarehe 11 Juni, 2020.
Hivyo, Bbunge la Tanzania limeamua kughairisha kuhitimisha Bunge mwezi tarehe 29 Mei, 2020 ili liende sambamba na nchi hizo.
“Ratiba ya mwanzo haikuwa inaonyesha hivyo, badiliko ni kutokana na kwamba tuna tamaduni ya bajeti za bunge la nchi za Afrika Mashariki kusomwa pamoja. Lakini kutokana na janga la Corona, mawaziri wa fedha wamekubaliana tarehe 11 Juni isomwe bajeti, “ amesema Spika Ndugai.

Awali, uongozi wa bunge ulitangaza kwamba, shughuli za mhimili huo uliozinduliwa tarehe 20 Novemba 2015 na Rais Magufuli zitafikia tamati tarehe 29 Mei 2020.“Pia niwajulishe, tumemaliza muda si mrefu kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge, ambapo tulikuwa tunatahimini shughuli zetu. Tumekubaliana tumalize shughuli za bunge la 11 tarehe 19 Juni 2020, panapo majaliwa Rais Magufuli anaweza kuja kufunga rasmi,” amesema Spika Ndugai.