Rais Magufuli anachezeshwa Mchezo wa "Buy Time"

IZENGOB

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
323
317
WARAKA KWA MJOMBA MAGUFULI
Anaandika Bundala Izengo
Kwanza pole na kazi nzito za kulijenga taifa lililo na changamoto lukuki,Ndugu Raisi hongera kwa kubeba sera nzito na ngumu kuliko zote ya "Tanzania ya viwanda" uchumi wa viwanda unawezekana hasa katika nchi iliyobarikiwa Raslimali kama Tanzania.

Juzi nimesikia sauti yako ukitoa onyo kali kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwa makini na habari wanazozitoa ukisahau kabisa kuwa gazeti hutoa habari inayozingatia mahitaji ya msomaji siku hiyo. Ulikwenda mbali sana ukaviasa vyombo vya habari kushirikiana kwa pamoja kuunga mkono sera ya taifa ya "TANZANIA YA VIWANDA" hapa ndipo kwenye hoja yangu siku ya leo.

Nimeamua kutumia busara ya taaluma yangu na vidole vyangu kukuandikia haya Mjomba,
Sera ya Tanzania ya viwanda haieleweki pa kuanzia kwani hata wewe hujawahi kuweka wazi kuwa sera hiyo inaanzia wapi Mfano.Rasilimali watu,Kuvutia wawekezaji wa nje na ndani, kutengeneza miundombinu,kuanzisha sekta ya viwanda yenye kujifungamanisha na mazao ya kilimo. Hili nadhani ndio tatizo hata waandishi wanashindwa waanzie wapi kwani sera hii umeibeba kwa ujumla mno.

Mwaka 2015 wakati mkichuana majukwaani na yule bwana mwenye nywele nyeupe,nilikuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana hasa vipaumbele vyenu ambapo mwenzio alionyesha wazi kuwa katika sera ya Viwanda angezigeuza kambi za JKT kuwa VETA ili vijana wasome uzalendo na taaluma ya uhandisi na ufundi kwani hii ndio injini ya Tanzania ya Viwanda.

Mjomba ukumbuke kuwa tangu mwaka 1992 ni miaka 25 sasa sera ya viwanda tuliizika rasmi hivyo itakuwa ni vigumu kuifufua bila ya kuwa na mipango madhubuti ya kutengeneza rasilimali watu na rasilimali vitu(secta ya viwanda yenye kufungamanisha na bidhaa za kilimo) la sivyo sera hiyo itabaki kuwa wimbo wenye tumaini tupu maskioni mwa watanzania.

Wakati nikiandika haya nasikitishwa na jinsi serikali yako imeamua kupoteza muda kufuatilia mambo madogo ambayo hayana tija katika sera yako hata kidogo.Bila ya wewe kutambua umejikuta ukicheza ngoma ya maadui zako iitwayo "Buy Time"(nunua muda) ukisahau kabisa kuhusu sera yako ambapo bado una nafasi kubwa ya kutengeneza maajabu katika sera hii.

Mjomba kuna ulazima gani ya kukimbizana na hawa wanaokuimba vibaya na wanaokuandika vibaya katika mitandao ya kijamii?Je muda huo ungeutumia kuongea na Dangote au matajiri wengine dunia kuwashawishi waje kuwekeza hapa nchini kwa masharti nafuu?Askari wanaotumika kukamata hawa watu na wengine kuwasafirisha kutoka mikoani mpaka Dar ungewatuma kuzuia magendo yanayofanyika huko pembezoni mwa mipaka yetu si ingekuwa bora zaidi kuliko wanavyotumika hivi sasa na ukizingatia wanatumia kodi zetu?
Kumbuka kuwa tumeshaingia mwaka 2017 na 2018 kuna chaguzi ndogo za serikali ya mtaa zitafanyika jua ya kuwa hawa maadui zako wnaendelea kucheza mchezo wa "Buy Time".Mjomba nakukumbusha tu mimi sio mchochezi Mjomba.
 
Aliambiwa kagame kuwa sera ya viwanda itawezekana kama atapiga marifuku harakati za vyama vya Upinzani
 
...Mjomba kuna ulazima gani ya kukimbizana na hawa wanaokuimba vibaya na wanaokuandika vibaya katika mitandao ya kijamii?...
Mjomba wako leo amekuumbua. Tafuta kingine cha kufanya.
 
Mshauri wa mjomba ni yule tall wa kigali ambaye anaongoza watu mil 5 sijui huku yeye anaongoza mil 50
 
Hii sera ilikua ya kuombea kura. Hauwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuinganisha na kilimo,nishati na miundombinu.
 
Kila mtu anaweza Namba, lakini siyo Kila mtu anaweza Hesabu. mkuu watu yeye anaweza Namba, kwenye swala la Hesabu ni kilaza wa kiwango cha Bashite Kolomije.
 
Back
Top Bottom