Rais Magufuli amuapisha waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Tizeba

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles John Tizeba (Mb) kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba kulia pamoja na kaka yake Mhandisi Adrian Tizeba mara baada ya kumalizika kwa tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Mhandisi Adrian Tizeba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mwanza amerejea rasmi Chama cha Mapinduzi CCM.
 
xMchemba.jpg.pagespeed.ic.eHEDlFrrxp.webp


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akipeana mkono na Rais Magufuli muda mchache baada ya kuapishwa.

Jumamosi iliyopita Rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
xMchembaa.jpg.pagespeed.ic.SulVWoi8xt.webp


Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
.
 
Tunataka demokrasia huru......."kitisho kikuu cha uhuru ni kukosekana kwa ukosoaji"
 
Rais awaapisha Waziri wa Mambo ya ndani na Waziri wa Kilimo na Mifugo na Uvuvi, june 2016,
Raisi Magufuli amemwapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa mambo ya ndani nafasi ambayo ilikua wazi baada ya Raisi kutengeua uteuzi wa aliyekua waziri wa mambo ya ndani mh. Kitwangwa kawa kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa.
 
Hongereni sana Tizeba na Mwigulu mkachape kazi kwa kuwa utendaji wenu tunaujua hamtatuangusha.
 
Back
Top Bottom