Rais Magufuli amteua Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)

asante kwa kunielewesha, ila pia bado ni majanga, yule jamaa angepewa nafasi kule kwa wasanii ingemfaa zaidi, huku kwenye elimu hapamfai
Hahaah kwa wasanii wapi?? Wasanii wenzake...!!
 
Hyo n nafas ya picha hakuna effect yoyote kwa udsm coz mkandala ndo anaratibu mambobyote ya chuo yeye atakuwa ceremonial head..
 
naona haya ni majanga tuu, mtu ambaye nchi ilimshinda anapewa taasisi nyeti

Yeye sio mtendaji mkuu wa chuo jamani, angalia Mkapa ni Chancellor wa UDOM, Msuya D ni ARDHI, Mwandosya M yuko MUST nk, hivyo hakuna kosa. Sema ni kama JK alijibakizia hiyo nafasi maana iko wazi tangu kufariki kwa Balozi Flugence Rwezaura about three years ago lakini JK hakuteua mtu mwingine hadi anaondoka Ikulu hivi majuzi.
 
tatizo jk hafai popote mkuu, yani hili janga tuuu
Kwa nafasi aliyopewa ni ya kisiasa zaidi, hana impact sana.........yeye zaidi siku ya graduation kutoa hizo degree labda na ushauri tu.
 
Nijuavyo mkuu wa chuo kikuu cha taifa(udsm) miaka yote anakuwaga Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania!Imekuwaje sasa?au utaratibu ulishabadilika kitambo?
 
Bavicha kweli akili ndogo,hivi kwa mawazo yenu mnadhani jpm anaweza kumfanyia ubaya jk?.??

Huo utamaduni haupo na utakapoanza hakuna rais atakubali kuachia madaraka kamwe
 
Mkuu wa chuo hana kazi ya maana, Mkandala ni Makamu mkuu wa chuo, ndiye mtendaji wa kazi za kila siku za chuo. Ukuu wa chuo ni nafasi za kisiasa zaidi hazina cha maana labda wakati wa graduation, kama sio mgeni rasmi aliyealikwa, basi mkuu wa chuo ndiye mgawa zawadi na vyeti
Yaah...ila anahitajika mtu makini zaidi. Kwa mtazamo wangu, JK sio mtu serious hivyo sio chaguo sahihi kwa nafasi kama hii.
 
Nijuavyo mkuu wa chuo kikuu cha taifa(udsm) miaka yote anakuwaga Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania!Imekuwaje sasa?au utaratibu ulishabadilika kitambo?
Ilibadilishwa nadhani kitambo, maana alikuwa Paul Bomani (sina uhakika), Rwezaura na sasa huyu J. K.
 
Back
Top Bottom