Rais Magufuli amteua Mama Makinda kuwa M/kiti Bodi NHIF, Jaji Lila kuwa jaji Mahakama Rufani...

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology -DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro. Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

13308222_10154254102004345_3721840702264604012_o.jpg
 
Kutoka Ujaji Kiongozi ambae ni Msaidizi Mkuu wa Chief Justice hadi ujaji wa Mahkama ya Rufani Katumbuliwa kidizaini kama ile ya DPP Feleshi kupewa Ujaji wakati wa Baba Ridh, japokuwa kwny front page itaonekana kapanda kutoka Mahakama Kuu mpaka ya Rufaa
 
Hongera Mama Makinda kuongoza Bodi ya NHIF, Kazi inayofuata ni kumshauri Rais kuteua Mkurugenzi Mkuu NHIF nafasi ambayo inatolewa macho na Mmoja wa Vigogo wa juu NSSF ambae pia anajidai ni shabiki wa Simba alieshindwa kwny jaribio la kutaka kumrithi Dr. Dau baada ya kushiriki mbinu kadhaa chafu za kupata ulaji NHIF ikiwa ni pamoja na kutapeliwa zaidi ya Mamilioni na wajanja wa Mjini waliojifanya Wazee wa System pale Courtyard Hotel
 
Hii serekali maigizo hayaishi.. Mh Magufuli bado sina imani naye mawaziri kateuwa walewale wengine walevi wengine waliitwa mizigo.. Wakina Magembe.. Na hata hawa anao teuwa sasa ni wale wale.. Mizengo Pinda... Mama Makinda.. Hivi damu changa jamani hakuna.. Ni wale wale wa awamu ya nne anawarudisha kiaina
 

Mheshimiwa Rais na huyo uliyemtuma kuandika na kutuletea sisi hii HABARI ya TEUZI zako hizi ni lini na yeye UTAMPANDISHA kutoka katika kuwa KAIMU tu? Hofu yangu hiko Cheo cha UKAIMU kitamzoea hivyo hata ukija kumpandisha rasmi anaweza akawa ameshaathirika na kukaimu kaimu. Imetosha sasa Mheshimiwa Rais wangu Kipenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli hebu mpe sasa MADARAKA RASMI Bwana Gerson Msigwa.
 
Hvi teuzi kama ya Ane Makinda nayo ni makini? Hivi hakuna vijana wenye uwezo wakujaza nafasi kama hizo wakati wako mtaani wanazunguka na mavyeti yao tu.
Mkuuu tunavyosema kuwa CCM ni ileilee ile ndiyo tuna maanisha hayo ya kulindana, juzi kamteua pinda na kumkabidhi ulaji na jana kumteua makinda ni muendelezo tu wa kuwakumbuka wana CCM wenzake
 
Aah, Magu ameanza kuthibitisha CCM ni ile ile, yule Mama kimeo ndo ameona awe mwenyekit wa NHIF? unajua hapa bongo kamati hazinaga meno kabisa, mwenyekiti ndo kila kitu. Japokuwa sijasoma sheria iliyounda huo mfuko lakin najua Board role ya baadh ya mifuko.
Usishangae kusikia kuanzia sasaiv hakuna tena vibali vya kutibiwa hospitali kama regency, mwisho mwanamala and the like.
 
Back
Top Bottom