Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Muhimbili

Bado ni mapema sana kumsifia Rais.Tunataka huu moto usiwe wa nyasi.Hivyo tutaendelea kupinga kama njia ya kuchochea moto ili tupate maendeleo.Wananchi tuendeleeeee kukosoa hasa mpaka hawa jamaa wabadililike.
 
Tatizo letu Watz ni kufurahia mwingine kuguswa na misukosuko. Kamwachisha kazi, yeye ndiye kamwajiri?? Mkurugenzi huyo ana haki zake chungu nzima, unamwachisha tu ka Hg!!! Haya tungojee. Alisimamisha Makandarasi wangapi wa barabara bila mjadala. Wakamshinda mahakamani ka mtoto. Akalipa mihela ya kufa mtu. Hasara kwa taifa. Aliizuia meli ya Mvietnam, na samaki zake akagawa bure watu wale. Ati nitawashinda mahakamani. Amelipa meli mpya na samaki wapya kwa Dollar mpya za kimarekani. Hasara kuu kwa taifa.
Haya yoote, mlimsifia. Sitamsema vibaya rais wangu ila, Uongozi bora si hivyo. Yeye ni kiongozi, awaongoze wanaoongoza wafanye kazi ya viwango si kutimuana bila mpangilio. Ila kwa vile huwa hatuambiwi, mngekuja kutujuvya atakacho lipwa huyu mhusika baada ya kumbwaga mahakamani.

Naomba kujua kama ataweza kumshtaki raisi kwakumfukuza kazi.
 
..how about UCHAFU?

..hivi mmeona jinsi hospitali ya taifa ilivyo CHAFU?

..mbona kule Aga Khan alipotembelea kulikuwa kusafi?

..Raisi alipaswa kuwafuta kazi wahusika walisababisha hali ya uchafu Muhimbili.
Mkuu hawa jamaa wamemwachia Magufuli shughuli pevu ila imepata mwenyewe.

Kitendo cha kufuta safari na sasa aanze kuangalia ruzuku kama hospitali zina hali ile. Kusimamishwa kwa bodi kwanza kumechelewa hawa jamaa walikuwa wanatupa viuongo vya operation, sindano zilizotumika kwenye takataka as if hospitali aina incinerator clearly management ya kizembe in the first place isiyofikiria health hazards za matendo yao sasa wakiwa ndio viongozi wenyewe ni kasheshe.

Lakini kuna sehemu zingine aisee hapana ni vigumu kutekeleza majukumu na maraisi waliotangulia wamekosea sana kama muhimbili waliikuta katika hali hii na wameiacha mpaka imefikia hatua hizi tunazoona. Kwa pale unaweza piga deki saa ngapi wakati kuna wagonjwa wametupwa vile kama second class citizens 24/7 si unataka kuwaongezea risk zingine za magonjwa ya mlipuko tu, au rangi unapaka saa ngapi ndani kwa mlundikano ule si unataka uwape na mafua kama nyongeza watu ambao tayari wana maradhi na wengine wapo mwezi awana hela ya matibabu (shame tanzania).

Kuna vitu vingine ni impossible unajiuliza kwa shift kila nesi anatakiwa aangalie wagonjwa wangapi kwa mlundikano ule na kazi yenyewe stressful you can see why there are scores of unnecessary death watakosa tu morale ya kazi kwa mazingira yale a lot of people need to be fired wizarani na kwakweli aiwezi kuwa business as usual kuna wizara lazima aweke watu wenye weledi na wenye vision tu kama anataka changes na priorities za budget spending ziongezwe kwenye social policies.

Nimesikitika sana kuona kama viongozi wanaweza kuangalia raia wanapata treatment hizo for ages that is appalling what happened to humanity in Tanzania.
 
utawala wa sheria upewe nafasi yake, tofautisha kati ya kuswaga ngombo kwenda joshoni na kuongoza watu kwenda hali bora zaidi ya maisha

Hii nchi watu wanapiga pesa sana, then wanakuwa wajanja wajanja wa kucheza na sharia ili kukwepa adhabu nguvu yaziada inahitajika ilikuwaokoa wanyonge kama haotunaowaona huko muhimbili, shiria iwekwe pembeni kidogo kwa faida ya wanyonge.

Nampongeza japo sikumchagua.
 
Bodi ilishamaliza muda wake unaaenda kuovunja ili iweje?
Sifa za kijinga, ni sawa na mwaka jana kina zito wakakomaa bodi ya tanesco ivunjwe wakati ilikua imemaliza muda wake. Ni aibu kwa hili taifa.

Kaka sasa hapo sifa ziko wapi? Kama muda ulishaisha si wangeondoka wenyewe mpaka waje kuvuliwa nguo?
 
Lugha ya Rais kukasirishwa na hali/matendo fulani na kuchukua hatua ilitumika miaka ya nyuma 1985 kurudi nyuma - Enzi za Mwalimu. Baada ya hapo sikusikia tena Rais akikasirika na kuchukua hatua. Tumezoea kusikia Rais ametengua uteuzi (sio kuachisha kazi) amembadilisha kazi (sio kuvua madaraka), na kadhalika.
Jana nimesikia Rais Amesikitishwa, Kukasirishwa na kuchukua hatua hapo Muhimbili. Binafsi hii imenikumbusha Enzi za Mwalimu na Binafsi nimefarijika sana kupata kiongozi anayekasikia utendaji mbovu, na kusikitishwa na mateso ya wananchi. Wengine wanaweza kuwa na mawazo tofauti. Tujadili - Rais kukasirika ni sawa?
 
..kuna tatizo la UCHAFU.

..kwa kweli hapastahili kuitwa hospitali.

..aliyetelekeza hospitali mpaka ikawa chafu namna ile ilipaswa naye afukuzwe kazi.

..Raisi angefanya utaratibu wagonjwa wote waliolazwa chini wahamishiwe hospitali binafsi kwa gharama za serikali.

cc Nyani Ngabu, MsemajiUkweli

The thing is...hayo yote yametokea chini ya serikali za chama chake.
 
Back
Top Bottom