Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Muhimbili

Hakuna kitufe cha 'like' ndio maana imebidi ni quote. Tatizo la huduma za afya halikuanzia hapo, limeanzia toka juu, na jambo hili ni katika idara zote za serikali. Inawezekana mkurugenzi akawa na uzembe, lakini uzembe huo pia inawezekana umechochewa na mambo mengine ambayo yako juu ya uwezo wake.

sasa ajieleze nini tena,ina maana hyo hospital haikusanyi mapato?na vipi kuhusu suala la usafi nalo?
 
Watu wanajua kupamba. KUMBE MAGUFULI KAVUNJA BODI YA HOSPITAL KWASABABU BODI IMEMALIZA MUDA WAKE..HAHAAA
Watu wa aina yako mmezivamia siasa za upinzani mpaka akili na fikra zetu zimejaa negative thinking and ill-wishing.

Wewe ni aina ya wapinzani mnaotaka Rais Magufuli asifanikiwe katika utendaji wake ili mpate hoja fupi za kisiasa.

Hoja na tatizo lako ni nini?

Jaribu kuangalia masuala kwa kutumia fikra pevu.
 
Nadhani ni busara kumuunga mkono Mhe Rais kwa kuonyeshwa kukerwa na aliyoyaona pale Muhimbili,sasa kinachofatia ni kushughulika na tatizo.
Kuna baadhi ya watu wanabeza kwa sababu hawataki Rais Magufuli afanikiwe katika kazi zake.

Tumekuwa taifa la evil eye
 
Fungu la matengenezo ya mashine hizo linapatikanaje?utaratibu wa kutengeneza hizo mashine zikiharibika ukoje?
 
Kuna baadhi ya watu wanabeza kwa sababu hawataki Rais Magufuli afanikiwe katika kazi zake.

Tumekuwa taifa la evil eye

Mimi nawaunga mkono watu ambao wana mtazamo unaouita "kutotaka Magufuli afanikiwe" kwa sababu ndio watakaompa changamoto ya kufanya vizuri zaidi.

Kiongozi lazima awe na kundi la watu katika jamii wanaom criticize ili ajue wapi kakosea. Hakuna haja ya kumsifu kiongozi pale alipofanya vizuri kwa sababu ni wajibu wake kufanya hivyo.

Na vilevile nichukue fursa hii kuwapongeza wale wote waliopiga kura kwa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwani unamfanya Magufuli kuelewa kwamba Watanzania wameichoka CCM ndio maana walimnyima kura na kumchagua Lowassa kama Rais wao. Hali hii itamfanya Magufuli awe na guilt concious kipindi chake chote cha miaka mitano kwani anajua kwamba kama si CCM kuiba kura asingekuwa pale Ikulu.

Hivyo. Shime Wananchi. Hata kama Magufuli akifanya vizuri namna gani. Ikifika uchaguzi mkuu ujao, endeleeni kuwapigia kura Wapinzani ili kuongeza uwajibikaji kwa chama kitakachoingia madarakani.
 
'...yaani mimi Magufuli niwe Raisi,mimi kabisaaa,halafu mtu anaharibu eti bado namchekea! Ahh(anatia kisukuma), nalala naye mbele kwa mbele... Hawa Watanzania maskini wanahitaji mtu wa kuwasaidi....' Kipindi cha kampeni,hapo JK alikuwa pembeni akicheka
 
Watu wanashindwa kuelewa kwamba Dr Kidanto anatokea wizarani hivyo raisi amemrudisha hukohuko wizarani si alikuwa mshauri wa wizara?

Ushauri na Utawala ni vitu viwili tofauti na utaalam wa dr Kidanto kwenye magonjwa ya watoto unafaa utumike zaidi akiwa Wizarani na sio Muhimbili ambako alikwenda kufanya ulaji tu badala ya kushughulika na Utalaam wake.
 
Kama itakuwa ni kweli, basi hata mimi nimejiuliza kama wewe.

Ukipata iona ile video alipokuwa anamuuliza maswali daktari, utaelewa kwanini amemsimamisha!
Pia hivi vitu haviwi ghafla tu, lazima kuna za chini chini zilipelekwa!
 
Machine za neurology mwaka wa 2 hazifanyi kazi chonde RAIS Magufuri tusaidie hapo Muhimbili
 
Habarini,naona watu wanachanganya mambo..Rais hajamfukuza Mkurugenzi,alichokifanya katibu mkuu kiongozi ni kumuhamisha aliyekuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi kwenda wizarani..ikumbukwe kaimu mkurugenzi sio mkurugenzi kamili..na wakati huo huo kateuliwa mtu mwingine kukaimu nafasi hiyo ya ukurugenzi..nadhani.ndo taarifa inavyosema..tuache kuzusha kuwa.Rais Kamfukuza mkurugenzi wa Muhimbili.
Hizi mashine za CT Scan na MRI ni muhimu sana..kimsingi zinatakiwa kufanya kazi masaa yote kama mitambo ya redio/Tv ambayo haitakiwi kukatika katika kwa muda mrefu..sasa miezi miwili ni mingi sana..tukubali..wanaoifanya serikali hii ionekane haifanyi kazi ni watendaji wake..watupishe tu kama kasi ya Rais hawaiwezi.
 
No one is condemned unheard! Je kama alitaarifu mamlaka za juu kuhusu tatizo hilo akaambiwa asubiri fedha hazipo kwa sasa Hazina? Katibu Mkuu hazina alipaswa kuulizwa kama ana taarifa juu ya jambo hilo na jee ombi la fedha kwa matengenezo na ununuzi wa vifaa lilifika kunakohusika? Sasa akitembelea hospital za Mikoani si atafukuza Madakatari wa kuu wa Mikoa yote kwa kosa hilo? Dr
Pombe ameanza vizuri sana ila asaidiwe ili akimuwajibisha mtu awe ni muhusika!

hayo maswala raisi hana muda wa kufuatilia na kusoma barua ,,,..... alipaswa kutoa taarifa kuonesh kafanya juhudi zipi???? ok nilipeleka taarifa wizarani ikakataa kutoa ushirikiano,,,,, enhe what next?? ukaamua kulala watu wafe?????
embu tumuache raisi afanye kazi
 
..kuna tatizo la UCHAFU.

..kwa kweli hapastahili kuitwa hospitali.

..aliyetelekeza hospitali mpaka ikawa chafu namna ile ilipaswa naye afukuzwe kazi.

..Raisi angefanya utaratibu wagonjwa wote waliolazwa chini wahamishiwe hospitali binafsi kwa gharama za serikali.

cc Nyani Ngabu, MsemajiUkweli
 
Last edited by a moderator:
MRI na CT SCAN za hospitali binafsi nzima kila siku,lakini za hospitali za umma hasa Muhimbili kila kukicha mbovu,hapa kuna hujuma Mh. Rais wangu,hongera kwa maamuzi uliyofanya!

..how about UCHAFU?

..hivi mmeona jinsi hospitali ya taifa ilivyo CHAFU?

..mbona kule Aga Khan alipotembelea kulikuwa kusafi?

..Raisi alipaswa kuwafuta kazi wahusika walisababisha hali ya uchafu Muhimbili.
 
..how about UCHAFU?

..hivi mmeona jinsi hospitali ya taifa ilivyo CHAFU?

..mbona kule Aga Khan alipotembelea kulikuwa kusafi?

..Raisi alipaswa kuwafuta kazi wahusika walisababisha hali ya uchafu Muhimbili.

Keshafukuzwa tayari
 
Back
Top Bottom