Rais Magufuli ampokea Rais wa Zambia, Edgar Lungu

Rais Magufuli ampokea Rais wa Zambia, Edgar Lungu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Rais wa Zambia amewasili kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambayo pamoja na mambo mengi, nchi mbili zitatiliana mikataba ya kiuchumi na kijamii.

Tanzania na Zambia zina uhusiano na historia ya muda mrefu iliyoasisiwa na viongozi wa awamu ya kwanza wa Tanzania na Zambia lakini pia nchi hizi mbili ni mwanachama wa Southern African Development Community (SADC) yenye nchi 15 wanachama.

CyRpCNxWQAACzlL.jpg

CyRo0vJWgAAN5ZF.jpg

Rais Magufuli akijiandaa kumpokea Rais wa Zambia, Edgar Lungu.
CyRo8mTXgAAd55R.jpg

Rais Magufuli akiongea na Rais wa Zambia, Lungu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege tayari kwa ziara ya siku mbili nchini.
 
Uhusiano wa Tanzania na Zambia ni wa muda mrefu sasa! Tuendelee kuudumisha!
 
Duh Kwa hiyo Leo rais kapokea wageni wawili MUHIMU maeneo ya kutiliana sign mikataba yawe pia kwenye sekta ya kilimo maana ni kama imesahaulika
 
Ila tukumbuke tu Uchaguzi uliofanyika Zambia siku za karibuni ulikumbwa na utata baada ya dalili zote kuonyesha Upinzani ulikuwa umeshinda.

Alichokifanya huyu Bw Edgar Lungu na Tume yake ya Uchaguzi wanajua wenyewe mpaka yeye akatangazwa ameshinda.

Ni vema tukamfahamu kidogo huyu mgeni wa serikali ya CCM.
 
Rais tunavutiwa sana na jitihada zako za kuimarisha diplomasia ya uchumi nje ya nchi mabarozi waendelee pale ulipoishia mikataba hiyo ina matokeo mazuri ikifuatiliwa kwa bidii.It is a clear landmark in foreign policy
 
Ila tukumbuke tu Uchaguzi uliofanyika Zambia siku za karibuni ulikumbwa na utata baada ya dalili zote kuonyesha Upinzani ulikuwa umeshinda.

Alichokifanya huyu Bw Edgar Lungu na Tume yake ya Uchaguzi wanajua wenyewe mpaka yeye akatangazwa ameshinda.

Ni vema tukamfahamu kidogo huyu mgeni wa serikali ya CCM.
Kwa hiyo tumfukuze? Au Wazambia wamekwambia sio Rais wao.

Shame on you boy!!
 
Back
Top Bottom