Rais Magufuli amepatia jambo moja kwenye makinikia, amekosea jingine

Ile picha Rais Magufuli akipokea magari mawili ya taka kutoka kwa balozi wa Kuwait ilieleza jambo.
The president is desperate for anything he can get.

Nchi haina cash ya kujiendesha.Busara inamwambia rais kama kuna 'fimbo ya Musa na lile jabali la Meriba' basi apige chochote chaweza kutokea.

Na njia ilikuwepo tayari.
2013 Kikwete alitumia hiyo fimbo ya Musa kupiga hilo jiwe la Meriba na $20 million zikatoka. Alifanyaje?
2013 tribunal iliyoongozwa na jaji wa mahakama kuu ilitoa hukumu dhidi ya 'ukwepaji kodi' wa Barrick. Hukumu iliitaka Barrick kulipa $41.25 million kama kodi ya serikali.
Barrick ilichokisema ni kuwa, wahusika kwenye hiyo tribunal hawakuwa na uelewa juu ya tax arrangements kati ya Barrick na Serikali.
Ila, kama alama ya nia njema Barrick ikatoa $20 million kama fedha ya utangulizi kwa malipo ya kodi miaka mitatu mbele.
Take Note; Barrick haikulipa ile $41.25 million kama ruling ya tribunal ilivyotaka na maisha yakaendelea.

Kwahivyo hakuna ajabu yeyote katika hizi kelele za sasa za makinikia kwa Barrick kutoa fedha kidogo na maisha yakaendelea.

Alichokifanya Magufuli basically ni kupiga kelele kubwa zaidi ili Barrick atoe fedha nyingi zaidi.

Barrick / Acacia ni wafanyabiashara, na management ya kampuni inapimwa kwa mambo mengi ila sio kwa kushinda kesi mahakamani.
Kwahivyo , kwenye kutafuta hela, Magufuli anaweza kupata japo kidogo,ila sio hizo wanazozitaja.

ANAPOKOSEA MAGUFULI
In every war, there is enough glory for everyone. It is only a foolish general who will want to take it all for himself.

Rais Magufuli anakosea kufanya siasa za kutafuta moral high ground kwenye hili suala la Makinikia. Hawezi kuipata, sio leo wala kesho. Na haiwezekani tu kwasababu, simply, hana hiyo moral high ground na haipo kwaajili yake.

Kitu kimoja tunataka kusahau, wote tunataka kuwa bendera fuata upepo kama wabunge wa CCM.
What the president is doing is not sustainable. It is good for Mfa maji approach but, not a long term strategy to be counted upon.

Barrick/ Acacia wamewekeza around $ 3 billion - dolla billion 3.
Fedha hizi zinachangia zaidi ya robo ya exports zetu kama nchi na wachumi wanajua multiplier effect zake.
Fedha hizi kwenye uchumi wa dunia ya leo hazipatikani kirahisi. Sio kwenye mabank wala masoko ya hisa.

Tayari bei ya dhahabu imekuwa kikwazo kwenye uwekezaji wa dhahabu duniani kote kwa muda sasa. Sasa hili tatizo la 'unstable government policies' tunalojiongezea, haliendi kufanya mambo rahisi zaidi.

Magufuli akunje 'ngudo' na kusali Barrick watoe fedha kidogo ili afanye tena siasa kidogo halafu baada ya hapo akafanye mambo mengine ya maana. Makinikia kwake, kisiasa, sio nyumba nzuri ya kukaa kwa muda mrefu. Masika itaingiza maji.

Magufuli sio Sauli aliyekuja kuwa Paulo kwenye biblia kwasababu Magufuli bado ana roho ya kukomoa wapinzani wake na anaendesha serikali isiyofuata misingi ya sheria.
Magufuli hajashukiwa na roho mtakatifu kuwa mzalendo uzeeni, Magufuli hajui ni wapi apate fedha ya kuendeshea serikali. Fullstop
Viroba vipo au vimepigwa marufuku?? Kwenye suara la makinikia kukomoa upinzani kumeingiaje?? Hv watu kila kitu siasa.hivi watanzania hatuna masuala ya kitaifa yanayotuunganisha km nchi???!!! Kila kitu kinapimwa kw misingi ya kisiasa.
 
kumwita mtu "Lofa" haigharimu chochote. lakini kujenga hoja kwa nini unamwita lofa, inaweza kugharimu angalau kidogo. onesha u-GT wako kwa kujenga hoja. matusi siyo ishu. hata wale wadada wa uwanja wa fisi wanaweza kutoa matusi "bora zaidi" ya hili lako
Sijaona hoja inayofanana na GT zaidi upuuzi mtupu!
 
Nilidhani mheshimiwa ataomba hela kidogo, kumbe yeye anataka budget ya miaka 10. Hatari hii.
 
Tukumbushane tu maana nauona mwisho wetu vizuri kuliko mwanzo!
 
Kama rsis sna nia njema tumsaidieni kufikia lengo tuliokoe taifa

Sio kumtazama kama mechi ya yaifa stars na algeria
 
Back
Top Bottom