Rais Magufuli amepatia jambo moja kwenye makinikia, amekosea jingine

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,987
2,000
Ile picha Rais Magufuli akipokea magari mawili ya taka kutoka kwa balozi wa Kuwait ilieleza jambo.
The president is desperate for anything he can get.

Nchi haina cash ya kujiendesha.Busara inamwambia rais kama kuna 'fimbo ya Musa na lile jabali la Meriba' basi apige chochote chaweza kutokea.

Na njia ilikuwepo tayari.
2013 Kikwete alitumia hiyo fimbo ya Musa kupiga hilo jiwe la Meriba na $20 million zikatoka. Alifanyaje?
2013 tribunal iliyoongozwa na jaji wa mahakama kuu ilitoa hukumu dhidi ya 'ukwepaji kodi' wa Barrick. Hukumu iliitaka Barrick kulipa $41.25 million kama kodi ya serikali.
Barrick ilichokisema ni kuwa, wahusika kwenye hiyo tribunal hawakuwa na uelewa juu ya tax arrangements kati ya Barrick na Serikali.
Ila, kama alama ya nia njema Barrick ikatoa $20 million kama fedha ya utangulizi kwa malipo ya kodi miaka mitatu mbele.
Take Note; Barrick haikulipa ile $41.25 million kama ruling ya tribunal ilivyotaka na maisha yakaendelea.

Kwahivyo hakuna ajabu yeyote katika hizi kelele za sasa za makinikia kwa Barrick kutoa fedha kidogo na maisha yakaendelea.

Alichokifanya Magufuli basically ni kupiga kelele kubwa zaidi ili Barrick atoe fedha nyingi zaidi.

Barrick / Acacia ni wafanyabiashara, na management ya kampuni inapimwa kwa mambo mengi ila sio kwa kushinda kesi mahakamani.
Kwahivyo , kwenye kutafuta hela, Magufuli anaweza kupata japo kidogo,ila sio hizo wanazozitaja.

ANAPOKOSEA MAGUFULI
In every war, there is enough glory for everyone. It is only a foolish general who will want to take it all for himself.

Rais Magufuli anakosea kufanya siasa za kutafuta moral high ground kwenye hili suala la Makinikia. Hawezi kuipata, sio leo wala kesho. Na haiwezekani tu kwasababu, simply, hana hiyo moral high ground na haipo kwaajili yake.

Kitu kimoja tunataka kusahau, wote tunataka kuwa bendera fuata upepo kama wabunge wa CCM.
What the president is doing is not sustainable. It is good for Mfa maji approach but, not a long term strategy to be counted upon.

Barrick/ Acacia wamewekeza around $ 3 billion - dolla billion 3.
Fedha hizi zinachangia zaidi ya robo ya exports zetu kama nchi na wachumi wanajua multiplier effect zake.
Fedha hizi kwenye uchumi wa dunia ya leo hazipatikani kirahisi. Sio kwenye mabank wala masoko ya hisa.

Tayari bei ya dhahabu imekuwa kikwazo kwenye uwekezaji wa dhahabu duniani kote kwa muda sasa. Sasa hili tatizo la 'unstable government policies' tunalojiongezea, haliendi kufanya mambo rahisi zaidi.

Magufuli akunje 'ngudo' na kusali Barrick watoe fedha kidogo ili afanye tena siasa kidogo halafu baada ya hapo akafanye mambo mengine ya maana. Makinikia kwake, kisiasa, sio nyumba nzuri ya kukaa kwa muda mrefu. Masika itaingiza maji.

Magufuli sio Sauli aliyekuja kuwa Paulo kwenye biblia kwasababu Magufuli bado ana roho ya kukomoa wapinzani wake na anaendesha serikali isiyofuata misingi ya sheria.
Magufuli hajashukiwa na roho mtakatifu kuwa mzalendo uzeeni, Magufuli hajui ni wapi apate fedha ya kuendeshea serikali. Fullstop
 
Negan The Dead

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
340
1,000
Tatizo lake anafikiri hao Barrick au Acacia walivamia kwa nguvu.Ni serikali yake ya ccm ndio ilipitisha mikataba hii,isitoshe aliingizwa madarakani na pesa za kifisadi na ujanja ujanja wa kina Makamba jr.
Na haya yote wazungu wanayajua vizuri, lazima tukubali kua njaa zetu, chama kibovu cha ccm na viongozi walafi ndio wametufikisha hapa.Unaanzaje kujenga ghorofa kwenye msingi mbovu?
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,927
2,000
Barrick/ Acacia wamewekeza around $ 3 billion - dolla billion 3.
Unaijua dollar bilion 3 au unaiona kwenye namba tu wewe.
Dola bilioni tatu kwa ajili ya kununua malori na mashine za kuchimbia tu au kuna nini zaidi?
Leta justification ya hiyo dola bilioni 3 hapa
 
Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,987
2,000
Unaijua dollar bilion 3 au unaiona kwenye namba tu wewe.
Dola bilioni tatu kwa ajili ya kununua malori na mashine za kuchimbia tu au kuna nini zaidi?
Leta justification ya hiyo dola bilioni 3 hapa
Dollar billion 3 kwenye hela ya madafu inaonekana kama 6,600,000,000,000/=tshs
But actually there investment is more than this!

Kama unajua uchumi nijulishe nitiririke multiplier effect yake kwenye uchumi .
Kama hujui tulia kimya ukaungane na viongozi wa bunge kutumia pombe zisizopikwa.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,927
2,000
Dollar billion 3 kwenye hela ya madafu inaonekana kama 6,600,000,000,000/=tshs
But actually there investment is more than this!

Kama unajua uchumi nijulishe nitiririke multiplier effect yake kwenye uchumi .
Kama hujui tulia kimya ukaungane na viongozi wa bunge kutumia pombe zisizopikwa.
Wacha kelele na mikwara.tiririka tuoneshe breakdown ya hiyo dola bilioni tatu imefanya nini.
 
Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,987
2,000
Wacha kelele na mikwara.tiririka tuoneshe breakdown ya hiyo dola bilioni tatu imefanya nini.
Kuongelea multiplier effect ya investment sio Kuongelea break down ya figures. Ni Kuongelea spill over effect ya investment kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo.
Hapa tu nimehisi unataka kunichosha na hata nikielezea hautanielewa.

Anyway, kujua multiplier effect ya investment ya level ya Barrick unapaswa kujua economics of mining kwanza .
Hii itakusaidia kujua trickle down effect of the figure.

Tanzania tunasema tuna utajiri wa madini .
Hii statement inaongelewa zaidi kwa layman language .
Utajiri wa chochote ni mpaka ukufanye wewe kuwa tajiri kwanza.
Hapa namaanisha for gold deposit in Tanzania to be regarded as a fortune it must be profitably located,developed,extracted,processed, and sold .

Unanipatapata niendelee au nikuruhusu ukashiriki pombe zisizopikwa na Mh. Speaker?
 
Blah blah nyingi tu,umetaja dola B3,unashindwa kuonesha zimefanya nini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom