Rais Magufuli ameirudisha nchi kwa wananchi

Rais Magufuli ameirudisha nchi kwa wananchi

November 5, 2017 na Azam TV
Azam TV - Miaka miwili ya Rais Magufuli madarakani, yachambuliwa
Azam TV imewakaribisha Elijah Mwandumbya -Kamishna wa kodi za ndani TRA, Dr. Benson Bana - Mhadhiri Mwanandamizi -UDSM na Dr. Albina Chuwa - Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Taifa-NBS. Maudhui ni kujadili yaliyotokea ktk miaka miwili ya utawala wa John Magufuli ikiwemo ''nidhamu'' ya kazi, kauli mbiu Hapa Kazi, asilimia 71% ya watanzani muda wa kazi watu walikuwa wanapiga soga hawazalishi mali n.k

Source: Azam TV
Wateuliwa wanatumia nguvu nyingi kusifu mtu hakuna sehemu wataalamu wameonesha ''mfumo'' mpya kuwekwa kuendesha nchi kwa mafanikio makubwa ili kuinua ufanisi sekta ya umma au viwanda vikubwa kujengwa, kukarabati/ujenzi wa reli, kilimo cha kisasa, uvuvi wa kisasa na biashara
 
November 6, 2017
AZAM TWO - 'MIZANI YA WIKI': Mjadala mkali miaka miwli ya JPM madarakani
Kanali Mstaafu Ngemela Esrom Lubinga, katibu wa NEC - CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa azungumzia sera za serikali ya awamu ya tano kuvutia wawekezaji toka nje ya nchi katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais. John Pombe Magufuli. Mahusiano ya CCM na chama cha LABOUR cha Uingereza. Nidhamu au woga wa watendaji serikalini . Heshima kwa CCM maana Mwenyekiti wao, Rais John Magufuli ''anaombwa'' na watu wa nje akatawale nchi zingine za kiafrika kwa angalau miaka miwili warudishe ''uwajibikaji'' wa viongozi ktk nchi zao n.k

Mchambuzi Edgar anaangalia minongono kuwa Mh. John Magufuli ni ''One Man Show'' maana inaonekana hakuna mfumo kila kitu Magufuli aende kutatua baada ya kuona ''mabango''. Kanali Mstaafu Lubinga Katibu wa NEC -CCM anasema Magufuli apewe muda kidogo kuendelea kuwa ''One Man Show''..... Kuzuiwa mikutano ya hadhara ya kisiasa demokrasia imedumazwa wakati mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais anatumia kofia zake mbili za kichama na kiserikali kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima...


Source: Azam TV
 
Yeye mwenyewe mwizi, fisadi na mpiga madili mkubwa halafu airudishe nchi kwa Wananchi!!! Ingekuwa hivyo basi angeruhusu katiba mpya ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi ili Watanzania wafanye kweli kwa kupiga kichwa cha nyoka mwenye sumu kali ili tuondokane na hili jinamizi lenye chuki za kutisha.


Kwani si kuna sheria inayoongoza upatikanaji wa katiba? Aruhusu vipi kabla ya kubadilisha sheria?
 
Tume Huru ya Uchaguzi

Katiba ya Warioba

Uhuru wa Maoni ili wananchi wawe huru kusema ya moyoni

Na wananchi wangethibitisha hili kwa kumpa Mheshimiwa Magufuli kura nyingi za kishindo, kura za haki
Uhuru mbona upo unaongelea Uhuru gani wa kutukana? Kama ni huo hauwezi kutokea kamwe!
 
A Rioba Huyuhuyu Ninayemfahamu Anajitoa Ufahamu Kabisa Kabisa?Kuirudisha Nchi Ni Kuruhusu Katiba Mpya,yy Ataondoka Katiba Itabaki Km Dira Yakutuongoza,kurudisha Nch Kwa Wananch Nipamoja Kufanya Kazi Km Timu Bila Mihimili Mengne Kuingiliwa,hyo Ndyo Tumesema Nch Imerudi Kwa Wananch
Kuiruhusu katiba gani? Kwani katiba so tunayo au unamaanisha rasimu pendekezwa? Kama ni hiyo si kuna sheria ya kufuata kabla ya kuwa katiba sasa aruhusu vipi bila kufuata sheria?
 
Na Judith Mhina – MAELEZO ( Rais Magufuli Ameirudisha Nchi Kwa Wananchi | MPEKUZI)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha nchi kwa wananchi na kwamba hayo ni mapinduzi ya ajabu ambayo hayajawahi kutokea katika nchi zetu hususan Afrika.

Maneno hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba alipofanya mahojiano na redio Uhuru mwishoni mwa wiki iliyopita katika ofisi zao zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar-es-salaam.

Dkt.Rioba amesema Mhe. Rais ameirudisha nchi kwa wananchi kwa kuwa anatekeleza “kile anachoambiwa na wananchi, na ahadi alizowaahidi wakati akiwaomba kura” anaeleza Dkt. Rioba na kuongeza kuwa yeye binafsi anamshukuru Mhe. Rais kwa “kuirudishia heshima Tanzania“.

Katika mahojiano hayo, Dkt. Rioba alieleza kuwa tangu kushika madaraka miaka miwili sasa Rais Magufuli amekuwa ‘busy’ kuhakikisha nchi inakaa sawa kimfumo ndio maana hajashughulika sana na safari za kwenda nje ya nchi.

Rais anataka kutengeneza “mfumo wa kimkataba au kibiashara na hawa mabwana wakubwa (wawekezaji toka nje) utakaowezesha kugawana nusu kwa nusu katika kile kinachopatikana katika uendelezaji wa rasilimali zetu badala ya mifumo ya zamani ya kukubali kila mfumo unaoletwa na nchi zilizoendelea” alisema Dkt. Rioba.

Mkurugezi Mkuu huyo alikieleza kituo hicho cha redio kuwa yeye binafsi anadhani kilichosababisha Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Barrick kumsikiliza Mhe Rais ni umakini wa kiongozi huyo kwa “hanunuliki, hahongwi hongwi maana Afrika ina viongozi wengi ambao wananunuliwa na kuhongwa” lakini sasa wanajua huyu ni tofauti.

Dkt. Rioba anamuona Rais Magufuli kuwa kiongozi anayesimamia mambo yanayo wanufaisha wananchi wake na “hakimbii kimbii kwenda huku na kule kuomba” na kuifananisha nchi yetu na zile zinazotoa misaada katika nchi nyingine. Kwa kuwa fedha wanazozipata zinatokana na rasilimali zetu na kueendeleza nchi zao.

Mhe Magufuli alisema; “Nchi yetu ilitakiwa kuwa Donor Country, yaani nchi inayotoa misaada kwa nchi nyingine”.

Ninachoweza kuwaambia Watanzania wenzangu miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano madarakani, hakika viongozi wetu wameonesha nia nzuri na wanatakiwa kuunga mkono kwa hili analolifanya Rais Magufuli wakati huu wa mpito.

Nchi yoyote inapopita katika mpito ni lazima kuna mambo yalikuwa hayaendi sawa na mengine yamekwenda sawa. Mpito ukitokea kuna mabadiliko yatakayojitokeza. Mfano Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipendekeza mfumo wa vyama vingi japo wananchi wengi, bado waliutaka mfumo wa chama kimoja. Aidha kutokana na kubadilishana uongozi hapa Tanzania, mabadiliko mengi yalijitokeza ambayo yalikuwa mazuri na mengine sio mazuri kwa kuwa ni kipindi cha mpito.

Dkt. Rioba amesema ujio wa Rais Magufuli ulikuwa ujio muhimu sana kwa wakati huu, kwa ajili ya kurekebisha yale yote yaliyojitokeza ambayo hayakuwa sawa. Akitoa mfano wa mwana falsafa mmoja anayeitwa Fans Fanon wakati wa vita vya ukombozi nchini Algeria alisema:

“Kila kizazi kinakutana na majukumu yake ya msingi ya kutekeleza au kuyatelekeza na kusubiri matokeo yake”

Mkurugezi Mkuu huyo wa TBC alieleza kuwa kwa maoni yake Rais Magufuli amekuwa kiongozi sahihi aliyekuja kwa wakati sahihi, ili kurekebisha mambo kwa namna moja au nyingine ambapo hapa na pale tulijikwaa kwa sababu tulitoka nje ya misingi iliyojengwa na Taifa letu.

Kuhusu suala la kuwa na uchumi mzuri katika nchi Rioba amesema tafiti zinafanyika kwa mrengo wa kimagharibi zaidi ambapo, wanahalalisha mifumo ya uchumi wanayoitaka wao. Wachumi walio wengi wanasema ili uchumi uwe mzuri na nchi kuendelea ni lazima kuwa na Ardhi, tekinolojia, rasilimali ziwe nyingi nk , lakini sio kweli.

Mfano nchi ya Singapore hawana rasilimali zaidi ya bahari na samaki lakini uchumi wao ni mzuri sababu moja kubwa ni uongozi bora ambao unasimamia matumizi sahihi ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi wa nchi husika. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi ya 4 duniani kwa wingi wa madini lakini haijaendelea, mpaka leo kuna watu wanaomiliki madini katika nchi hiyo wako nje hivyo faida yote inayopatikana kutokana na madini hayo inazinufaisha nchi za nje.

Jambo la msingi Rais Magufuli anataka rasilimali zilizopo, hata kama kidogo kitumike kwa manufaa ya wananchi wanyonge wa Tanzania. Tanzania ya Rais Magufuli amesema hapana haya madini yanayopatikana hapa Tanzania ni lazima tugawane nusu kwa nusu.

Dkt. Rioba anasema Rais ameonesha mfano kwa nchi nyingine za Afrika zenye rasilimali kama zetu, kuwa hili la kugawana faida nusu kwa nusu, hata kama hatuna tekinolojia na mitaji linawezekana.

Zipo nchi nyingi za Afrika ambazo zilitumia rasilimali zao vibaya mfano, Siera Leoni, Liberia wakawa wanachimba almasi kwa ajili ya kuendesha vita na kununua silaha kutoka nchi zilizoendelea. Afrika ifike mahali ioneshe ukomavu na kuacha mambo ya kipumbavu kama hayo ioneshe kuwa Afrika ina watu wanaweza kufikiri na kuweza kugawana rasilimali kama alivyofanya Rais Magufuli.

Ukiangalia nchi ya Nigeria asilimia 80 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda nje ni asilimia 1 tu ya mafuta hayo ndio yanarudi Nigeria, lakini Tanzana ya Magufuli amesema hapana

Akitoa mfano Dkt Rioba alisema Baba wa Taifa mara baada ya Uhuru wa Tanganyika, wasomi walikuwa wachache sana wasingeweza kutosheleza katika masuala ya utaalam na kuleta maendeleo kupitia rasilimali tulizonazo. leo hii nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika suala la taaluma na elimu ambapo hatukuwa na Chuo Kikuu hata kimoja. Leo Tanzania ina vyuo vikuu takriban 50, na wataalamu wako wengi, tunachokosa ni Wataalamu wanaoipenda nchi yao wazalendo wenye nia ya kusukuma gurudumu la maendeleo.

Dkt. Rioba anaeleza kuwa ni vizuri kuwa na waaalam vijana wenye moyo wa kujituma na uzalendo na kuwa tayari kuwa watumishi wa wananchi na kusaidia kutimiza ndoto ya Tanzania ya viwanda na ndivyo anavyotaka Rais Magufuli.

Akizungumzia suala la kuondoa dhana ya kuwa na matabaka ya watu katika Taifa, Rioba amesema kwa sababu Tanzania iko katika mpito, ambapo ilitoka katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea (Azimio la Arusha) na sasa ni kama kutengeneza Azimio la Arusha jipya lakini katika muktadha wa zama za sasa. Kwa wale watanzania ambao ni wazalendo kabisa kabisa, Dkt. Rioba anasema watakubaliana nae kuwa anayoyafanya Rais Magufuli ni lazima aungwe mkono kwa kuwa anaipeleka nchi panapostahili.

Dkt. Rioba katika mahojiano hayo amesema ni wakati sasa kwa kila Mtanzania kuona uchungu kwa kila aina ya wizi wa rasilimali za nchi na kwamba dhambi kubwa ambayo watanzania wanaweza kuifanya ni kudhani kuwa jukumu la kulinda rasilimali za nchi ni la Rais Magufuli pekee.

“Haijawahi tokea kiongozi yeyote barani Afirika kusema wananchi tumeibiwa mno na mbali zaidi, kutafuta suluhisho la kuibiwa huko. Hongera Rais Magufuli jitihada zako ni ukombozi kwa rasilimali zote Barani Afrika na mwisho wa Bara la Afrika kuwa Shamba la Bibi (akimaanisha kila mtu anakuja kujichukulia na kundoka)” Dkt. Rioba alimazilia mahojiano hayo.

Kulikuwepo Na Misukule na Mabufoon waliokuwa wanawashangilia Akina Mobutu, Id Amin, Bokassa etc. Hata wewe sikushangai.

1) Kununua Madiwani wa Upinzani kwa fedha za Walipakodi ni Uzalendo?

2) Kukamata Watu wanaotoa Maoni yao Kikatiba Ni Uzalendo?

3) Kuiba 2.7 Bil Kuhonga Wabunge wa CCM ili kupitisha sheria ya habari ni Uzalendo?

4) Kumwambia Aliyeingia Kwa jinai Piga Kazi ni Uzalendo?

5) Kumpandisha Cheo aliyetoa na kukiri kutoa Rushwa ni Uzalendo

6) Kumyanyapaa Nyalandu kwa kwenda Kumsalimia Tundu Lissu ni Uzalendo? ( Jiulize ni Kwanini ni Usaliti Kumwona?)

7) Kumpiga Tundu Lissu Risasi ni Uzalendo? (Kwanini maombi yazuiwe? kwanini isiwe sawa wanaccm kumwona?)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Limbukeni? Miaka zaidi ya 20 anaongoza!!!
As God Live That will Never, Never, Never happen Mark my words! Magufuli will not Even rule Tanzania for 5 years if he keep Acting the way he is Doing, Mbanu! God Forbid, It will never happen oooooh! God will not Allow it!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mfano mzuri ni Chato International Airport itakuwa ni ya wanambuzi na wanang'ombe kupata malisho.
 
Jinga kweli, milioni 50 za kila kijiji ziko wapi? mikopo kwa wanafunzi, masilahi kwa wafanyakazi, bei kwa vifaa vya ujenzi n.k
Mjinga nani kati ya ww mzururaji na yeye anayeishi maisha bora
 
Mimi sikubaliani na wote wanaompongeza rais kwa sababu tangu aingie madarakani umaskini ndo umeingia.Wafanyakazi na watu waishio mijini hawana hela,watu wa vijijini nao vilevile hali ni mbaya zaidi.Watu wa mikoa ya kusini ambao mahindi ndo tegemeo yamezuiliwa kuuzwa nje.Wananchi wamebaki na mazao yao yanawaozea nyumbani.Watawapeleka vipi watoto shule?wataanzaje msimu mwingine wa kilimo?
Inawezekana mheshimiwa alikuwa anawaza kuwa kwa kuyazuia yatapata soko zaidi lkn haijawa hivyo.
Kilio cha wafanyabiashara ndo usiseme
Biashara kila siku ndo zinafungwa.Hii ndo serikali ya wananchi tunayoitaka?
Uhuru wa habari upo wapi? magazeti yanafungiwa,Mikutano ya hadhara no,sasa hiyo ndo serikali ya wananchi?anaogopa nini?
Rioba na wenzio mlioajiriwa kuupigia debe utawala huu mnajisumbua bure.Waswahili husema "Chema chajiuza,Kibaya chajitembeza! nyie akina Rioba ndo mnafanya hiyo kazi! hongereni lkn hamtafanikiwa.Kila mtu mpk vijijini wanajua machungu na magumu wanayopata mara baada ya huyu mheshimiwa kuingia ikulu.
Watu kama ninyi awamu zote huwa mnalalamika, hata akija rais mwingine bado mtalalamika. Kazi hamfanyi mnategemea maisha yatakuwa rahisi
 
Amerudisha nchi au amerudisha umasikini kwa wananchi?![emoji30][emoji30]
 
Jinga kweli, milioni 50 za kila kijiji ziko wapi? mikopo kwa wanafunzi, masilahi kwa wafanyakazi, bei kwa vifaa vya ujenzi n.k
Ulitaka Ryoba amsifie mboowe kwa kutaka kumuua Lissu ndio furaha yako?
 
Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
Nchi imekwisha kweli hii ni kauli ya Rioba jamaniii duu shame Rioba
Toa maoni yako na wewe. Sio kulalamika eti Rioba jamani. Au wewe ni kati ya makundi yale mafisadi.vyeti feki. Mishahara hewa n.k. wasafi wanaona maendeleo yanakuja
 
I nawezekana...ila wakati yeye anakimbia na Bing'ola,kuna mtanzania wa hali ya chini hali milo miwili kwa siku ila majgambo ni uchumi kupanda...
 
Back
Top Bottom