Rais Magufuli amefanikiwa kwenye propaganda

Baadhi ya miradi hiyo siyo ya Magufuli. Barabara za juu ni za Kikwete. Yeye alikuja kumalizia tu. Lakini propaganda zake zinawadhalilisha watangulizi wake, eti hawakufanya kitu! Eti yeye kafanya mengi kuliko Nyerere+Mwinyi+Mkapa+Kikwete combined. Ndio propaganda hizo. Kikwete aliacha macho yaone yenyewe siyo kuimbwa kwenye kwaya na TBC.
Nadhani wewe una miwani ya mbao, hii miradi yote mikubwa huoni?
 
Aisee, huo mradi umefikia wapi? Mnasifia hadi mnakera, leta ulinganisho tuone.
Ulinganisho ndiyo huo niliokupa kama unapinga pinga kwa hoja, kwa mfano jumlisha gharama zote za miradi yote iliyotekelezwa awamu ya nne na uliganishe na gharama ya mradi huo mmoja wa bwawa la umeme la Rufiji.
 
Baadhi ya miradi hiyo siyo ya Magufuli. Barabara za juu ni za Kikwete. Yeye alikuja kumalizia tu. Lakini propaganda zake zinawadhalilisha watangulizi wake, eti hawakufanya kitu! Eti yeye kafanya mengi kuliko Nyerere+Mwinyi+Mkapa+Kikwete combined. Ndio propaganda hizo. Kikwete aliacha macho yaone yenyewe siyo kuimbwa kwenye kwaya na TBC.
Wewe ni mpuuzi kweli hutakuja kuelewa kitu
 
Hajui hata propaganda. Ni ubabe tu kuwaaminisha wananchi kuna maendeleo wakati kiuhalisia hali ni mbaya na umasikini umeongezeka kuliko hata kipindi Cha JK.
 
Kuna kipindi nilikuwa nafikiri rais Magufuli sio mwanasiasa, kumbe ni mwanasiasa tena aliyebobea anayejua kucheza vizuri katika siasa.

Uongozi wa miaka 5 mitano ya urais wa Magufuli umekamilika, ukijaribu kulinganisha maendeleo ya sasa na awamu zilizopita unagundua kuwa awamu zilizopita zilifanya maendeleo makubwa kuliko sasa. Mathalani Serikali ya awamu ya 4 ilijenga shule kila kata, barabara, ilisambaza umeme, maji toka ziwa Victoria, ajira, nyongeza ya mishahara kwa watumishi, ruzuku kwa wakulima, wafanyabiashara walifanya biashara bila bugudha. Lakini Serikali hiyo haikupewa sifa kama hii ya sasa.

Katika awamu hii hakuna ubunifu wowote uliofanywa kumkwamua mwananchi, shule zetu za msingi na sekondari zina hali mbaya, majengo hayatoshi na hata yaliyopo hayafai, walimu hawapo, vituo vya afya havina watumishi wa kutosha, maeneo mengi barabara ni zile zilizoachwa na awamu 4,ukosefu wa ajira ni mkubwa, awamu hii mkulima hajakumbukwa, maeneo mengi maji ni shida, rushwa na ukiritimba umekithiri.

Ukweli ni kwamba awamu hii haijamkumbuka mwananchi isipokuwa imewekeza kwenye propaganda kuaminisha watu kuwa imefanya makubwa wakati hali halisi hakuna kilichofanyika. Mbaya zaidi wanajua wanaongoza watu wa aina gani ndio maana Imekuwa rahisi kueneza propaganda zao.
Labda walichofanikiwa ni kuruhusu machinga kufanya biashara hata ikulu ili waonekane ni watetezi wa wanyonge. Magufuli ni mzigo mzito kwa taifa hili na watu wake ni vile tu propoganda zimewapumbaza akili
 
Ulinganisho ndiyo huo niliokupa kama unapinga pinga kwa hoja, kwa mfano jumlisha gharama zote za miradi yote iliyotekelezwa awamu ya nne na uliganishe na gharama ya mradi huo mmoja wa bwawa la umeme la Rufiji.
Fanya hivi chukua miradi yote ya awamu ya nne, gharama yake linganisha na huo mradi wa bwawa toa mkopo toa gharama ya mradi iliyotumika mpaka sasa.
Sijui mmesomea ujinga.
 
Labda walichofanikiwa ni kuruhusu machinga kufanya biashara hata ikulu ili waonekane ni watetezi wa wanyonge. Magufuli ni mzigo mzito kwa taifa hili na watu wake ni vile tu propoganda zimewapumbaza akili
Na deni la taifa kupaa.
 
Kuna kipindi nilikuwa nafikiri rais Magufuli sio mwanasiasa, kumbe ni mwanasiasa tena aliyebobea anayejua kucheza vizuri katika siasa.

Uongozi wa miaka 5 mitano ya urais wa Magufuli umekamilika, ukijaribu kulinganisha maendeleo ya sasa na awamu zilizopita unagundua kuwa awamu zilizopita zilifanya maendeleo makubwa kuliko sasa. Mathalani Serikali ya awamu ya 4 ilijenga shule kila kata, barabara, ilisambaza umeme, maji toka ziwa Victoria, ajira, nyongeza ya mishahara kwa watumishi, ruzuku kwa wakulima, wafanyabiashara walifanya biashara bila bugudha. Lakini Serikali hiyo haikupewa sifa kama hii ya sasa.

Katika awamu hii hakuna ubunifu wowote uliofanywa kumkwamua mwananchi, shule zetu za msingi na sekondari zina hali mbaya, majengo hayatoshi na hata yaliyopo hayafai, walimu hawapo, vituo vya afya havina watumishi wa kutosha, maeneo mengi barabara ni zile zilizoachwa na awamu 4,ukosefu wa ajira ni mkubwa, awamu hii mkulima hajakumbukwa, maeneo mengi maji ni shida, rushwa na ukiritimba umekithiri.

Ukweli ni kwamba awamu hii haijamkumbuka mwananchi isipokuwa imewekeza kwenye propaganda kuaminisha watu kuwa imefanya makubwa wakati hali halisi hakuna kilichofanyika. Mbaya zaidi wanajua wanaongoza watu wa aina gani ndio maana Imekuwa rahisi kueneza propaganda zao.
Sababu kubwa aliyebaki kuongea ni yeye tu wenzake wakiongea anadai wanamtukana.
 
Hii yake siyo propaganda ni ubabe.
bila mapolisi hamna kitu pale.
hastahili kupewa credit yoyote ya kuijua propaganda because hajui propaganda.
propaganda inahitaji mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja, which he doesn't have.

propaganda ni pale kunapokuwa na free expression (free media, political activities, independent parliament, independent courts, etc).

sasa hivi akihutubia yeye tv channels zote nchi nzima hadi za vichochoroni zinammulika yeye tu.

on the other side wamiliki wa radio, tv, nk hawana uhuru wa kuwapa wapinzani wake similar airtime/viewership kwa hofu ya kutembelewa na TRA/TAKOKURU the following morning.
Hili ndiyo kafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

Pamoja na mazuri kadhaa aliyofanya ukweli ni kwamba kawaminya sana wenzake kiasi cha kuonekana ni mtu katili na aisyefaa kuwa kiongozi.
 
CDM pingapinga mna matatizo sana, unajua gharama za mradi mmoja tu awamu hii, kwa mfano bwawa la kufua umeme la Rufiji ni sawa na gharama za miradi yote iliyotekelezwa awamu ya nne.
Hahahah mkuu tupe picha ya maendeleo ya bwawa Hilo.Barabara ya kimara Kibaha kilometer 17 Sasa miaka mitano na haijakamilika
 
CDM pingapinga mna matatizo sana, unajua gharama za mradi mmoja tu awamu hii, kwa mfano bwawa la kufua umeme la Rufiji ni sawa na gharama za miradi yote iliyotekelezwa awamu ya nne.
[emoji16] Leta takwimu mkuu propaganda za kupondeza kila ujinga tumezishtukia
 
Amefanikiwa ktk propaganda za bunduki na kufunga
 
Pamoja na ruzuku yote, kuwalazimisha wabunge michango kila mwezi, hela za wahisani BADO CDM HAKUNA HATA OFISI!
Duh....!
Kwa hiyo kazi zao wanafanyia sebuleni kwako kama hawana ofisi!.
 
Uongozi wa miaka 5 mitano ya urais wa Magufuli umekamilika, ukijaribu kulinganisha maendeleo ya sasa na awamu zilizopita unagundua kuwa awamu zilizopita zilifanya maendeleo makubwa kuliko sasa. Mathalani Serikali ya awamu ya 4 ilijenga shule kila kata, barabara, ilisambaza umeme, maji toka ziwa Victoria, ajira, nyongeza ya mishahara kwa watumishi, ruzuku kwa wakulima, wafanyabiashara walifanya biashara bila bugudha. Lakini Serikali hiyo haikupewa sifa kama hii ya sasa.
Kikwete alikuwa na mipango mizuri sana ya kimaendeleo ya nchi.

Tatizo lake ni hilo linalojulikana kwa kila mtu - "Kukubali Tanzania kuliwa zaidi kuliko ilivyokula." na kuwa na ulaji usiokuwa na breki.
 
Jiwe anadai Aliikuta sukari ni sh 5000 akaishusha

Kisha anatuaminisha kuwa katengeneza ajira milioni 6

Anadai Ubungo Interchange kajenga yeye, wakati kakuta mradi ushatafiutiwa fedha na kusainiwa

Kisha anakuja kusema hadi daraja la Kigamboni kajenga yeye.

Bila miradi ambayo Jiwe alikuta ishasainiwa na kutafutiwa fedha na serikali ya JK, Jiwe ana miradi michache mno!
 
Back
Top Bottom