Kuna kipindi nilikuwa nafikiri rais Magufuli sio Mwanasiasa, kumbe ni mwanasiasa tena aliyebobea anayejua kucheza vizuri katika siasa.
Uongozi wa miaka 5 mitano ya urais wa Magufuli umekamilika, ukijaribu kulinganisha maendeleo ya sasa na awamu zilizopita unagundua kuwa awamu zilizopita zilifanya maendeleo makubwa kuliko sasa. Mathalani Serikali ya awamu ya 4 ilijenga shule kila kata, barabara, ilisambaza umeme, maji toka ziwa Victoria, ajira, nyongeza ya mishahara kwa watumishi, ruzuku kwa wakulima, wafanyabiashara walifanya biashara bila bugudha. Lakini Serikali hiyo haikupewa sifa kama hii ya sasa.
Katika awamu hii hakuna ubunifu wowote uliofanywa kumkwamua Mwananchi, shule zetu za msingi na sekondari zina hali mbaya, majengo hayatoshi na hata yaliyopo hayafai, walimu hawapo, vituo vya afya havina watumishi wa kutosha, maeneo mengi barabara ni zile zilizoachwa na awamu 4,ukosefu wa ajira ni mkubwa, awamu hii mkulima hajakumbukwa, maeneo mengi maji ni shida, rushwa na ukiritimba umekithiri.
Ukweli ni kwamba awamu hii haijamkumbuka Mwananchi isipokuwa imewekeza kwenye propaganda kuaminisha watu kuwa imefanya makubwa wakati hali halisi hakuna kilichofanyika. Mbaya zaidi wanajua wanaongoza watu wa aina gani ndio maana Imekuwa rahisi kueneza propaganda zao.