Kiongozi acha akili za kimagumashi. Ni wangapi ambao wamemaliza CHUO, wafanya biashara wazuri na wengine wameajiriwa ila hawalipi mikopo yao. Pia unasema ajira zimekaliwa unataka kusema miaka yote hiyo ajira zimekaliwa. Kuwa na logic kidogo. Watanzania wengi hatupendi kulipa mikopo shida iko hapo. Wengine wanashughuli za maana tu lakini hawalipi.Ukusanyaji wa mikopo utakuwaje rahisi wakati ajira za mliowakopesha mmezikalia?
Kuweka record sawa, mikopo imeanza kutolewa mwaka 1994 ila kwa mfumo wa unapewa kila kitu na wengine hata ada ya chuo hujui ni shilingi ngapi maana wewe ni kusoma tu unachojua ni stationery allowance pamoja na food and accomodation allowance mpaka pale bodi ya mkopo ilipoanzishwa 2004 ndipo huu utaratibu wa sasa ukaanzishwa ambapo pamoja na kwamba unapewa mkopo lakini gharama ya course yako unapewa na unachangia kiasi kadhaa kulingana na asilimia ulizopewa. Na ndio maana wanapotusaka wanufaika wa mikopo husema wale wote ambao wamesoma elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 na kuendeleaFedha za kusomesha wanafunzi chuo kikuu zilikuwa zinatolewa na wafadhili mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000! Wafadhili walipojitoa kutusomesha ndio yakaanza haya mambo ya mikopo...
Zamani lini???Wewe Bawacha hivi hujui kama zamani wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa wanasoma bure ,siyo mkopo ni bure.
PointKinachokulazimsha ni Masharti ya Mkopo uliosaini sio Magufuli
Hakuna bure siku hizi,peleka stress zako mbeleWakuu
Nimeangalia CV ya Rais nimeona amesema chuo degree ya kwanza mwaka 1985 -1988.
Je, alipataje elimu yake ?
Je, alisomeshwa na nani?
Je, kama alisomeshwa na serikali amelipa pesa ya serikali iliyomsomesha?
Je, kama hakulipa kwanini anawakazia wanafunzi waliokuwa chini ya bodi walipe madeni?
Kama hakulipa maana bodi ilikuwa aijaundwa kwanini hataki wenzake wasome bure?
Kwanini imekuwa ngumu sana kwa mtu aliyepewa elimu bure yeye kuwanyima wenzie elimu?
Basi hata hizo za kurudisha wapeni basi wadogo zetu masikini ziwasadie.
Ukweli mchungu ni kuwa hakuna viongozi wowote waliojilipia ada ya chuo kikuu.
Magufuli
Lowassa
Kikwete
Ndalichako .
Na wengine mulisoma bure udsm na wala hamkudaiwa pesa baada ya masomo yenu.
Nyerere kawapa elimu bure na Mungu anawaona .
Magufuli toa elimu bure mpaka chuo kikuu au jiuzulu.
Hiyo moral authority haimfanyi ashindwe kusomesha wenzieWakati yeye anasoma yaani kuanzia waliosoma 1993 kwenda nyuma ilikuwa unasoma bure alafu unatakiwa kufanya kazi serikalini kwa muda wa miaka 5 lakini kwa waliosoma kuanzia 1994 na kuendelea ndio utaratibu wa mikopo ulipoanzishwa na lengo lilikuwa kupata idadi kubwa ya wanafunzi kwa kigezo kwamba wanaporudisha walengwa wa mikopo zinapatikana za kulipia wengine. Kutokana na kutokuwepo utaratibu mzuri wa ukusanyaji madeni ndipo 2004 bodi ya mikopo ilipoanzishwa japokuwa bado changamoto ya ukusanyaji madeni haukuwa mzuri mpaka ilipofika 2009 angalau makusanyo yalianza kukusanywa japo kwa kasi ndogo
Kwahiyo Rais na kundi lake na wazee wetu wote wao sheria hahiwataki kulipa mikopo
zamani walikuwa wachache kweli pamoja na hilo vitega uchumi vilikuwa vichache pia. Inakuwaje kwa sasa pamoja na migodi, gesi nk vipo ila hata uo mkopo wenyewe unakosekanaZamani wasomaji walikuwa wachache so ilikuwa ni rahisi kuwasomesha. Now wasomaji wamekuwa wengi so inakuwa ni mzigo mkubwa kwa taifa... Hili suala lingekuwa rahisi Zaidi kama ukusanyaji wa mikopo kwa wakopaji waliomaliza lingekuwa effective...
Sasa hivi wafadhili mnawatukana wana uwezo wa kuzitoa ndio maana tumepoteza 1.6 trions za MCCFedha za kusomesha wanafunzi chuo kikuu zilikuwa zinatolewa na wafadhili mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000! Wafadhili walipojitoa kutusomesha ndio yakaanza haya mambo ya mikopo...
Swali gumu majibu mepesiZamani wasomaji walikuwa wachache so ilikuwa ni rahisi kuwasomesha. Now wasomaji wamekuwa wengi so inakuwa ni mzigo mkubwa kwa taifa... Hili suala lingekuwa rahisi Zaidi kama ukusanyaji wa mikopo kwa wakopaji waliomaliza lingekuwa effective...
Daaah hii nchi ngumu kweli alafu mtu anakwambia niombee..mimi sikupata mkopo lakini kama ningekuwa nimekopeshwa nisingelipa huo mkopo kwanini nilipe niyekopeshwa wakatiwale waliochukua kwa nguvu hela za mboga,vijisenti zile za harusi na nyingine nyingi tu wala hawaulizwi na hili sio uchochezi ila ni halihalisi
Tujenge utamaduni wa kuwajenga watoto wetu kwamba jukumu la kumsomesha mtoto ni la mzazi mwenyewe hivyo tutakuwa na kizazi ambacho tayari kimejiandaa kisaikolojia kuliko hivi sasa kila siku tunawaza bure na kila awamu inakuja na mkakati wake yaani maisha yanakuwa mashakani kila siku yaani huyu elimu bure akiingia mwingine lazima tulipe. (kwa mapato gani ya serikali mpaka tusome bure, na huu mkopo sema wengi wameutafsiri vibaya hasa wale ambao hawajaanza kulipa na vichwani siasa ndio kila kitu katika mfumo wa maisha).Hiyo moral authority haimfanyi ashindwe kusomesha wenzie
Kidogo nimekusoma lakini shida ya maamzi yao yana effect kubwa sana katika maisha yetuKupambana na Wanasiasa ni Kupoteza Muda!
Mkuu we hutaki kumuombea mkulu[emoji3]Daaah hii nchi ngumu kweli alafu mtu anakwambia niombee..
Unapoongea angalia maisha ya watanzania 80% ni bora mtu umpe elimu iliyo bora hivyo vingine atatfuta mwenyewe...Tujenge utamaduni wa kuwajenga watoto wetu kwamba jukumu la kumsomesha mtoto ni la mzazi mwenyewe hivyo tutakuwa na kizazi ambacho tayari kimejiandaa kisaikolojia kuliko hivi sasa kila siku tunawaza bure na kila awamu inakuja na mkakati wake yaani maisha yanakuwa mashakani kila siku yaani huyu elimu bure akiingia mwingine lazima tulipe. (kwa mapato gani ya serikali mpaka tusome bure, na huu mkopo sema wengi wameutafsiri vibaya hasa wale ambao hawajaanza kulipa na vichwani siasa ndio kila kitu katika mfumo wa maisha).
Kwa mfano walivyoanza kukusanya walikuwa wanamwomba mwajiri aonyeshe ushirikiano kwa kuwataja wanafunzi waliosoma kipindi cha kuanzia 1994 kisha bodi inaleta deni ofisini kila mtu aliangalie na kukubali kama ni kweli na yupo tayari kisha unaandaliwa utaratibu wa kulipa na wengi walikuwa wanalipa kati ya 30,000 mpaka 50,000 haijalishi unadaiwa shilingi ngapi, uzembe wa serikali kwa miaka iliyopita na wanufaika wenyewe kukimbiakimbia wakidhani watalipishwa laki kadhaa ndio umetufikisha hapa mpaka Bodi ikaweka kiwango cha marejesho kisipungue 8% ya mshahara wa mnufaika