Kwani kujulikana mpaka aende kutembelea nchi nyingine? Kazi zake na ubunifu wake umemtangaza vya kutosha mpaka wengine wanataka kutunyima misaada. Alipoingia tu ikulu alianza na ukwepaji Kodi bandarini, akafuta safari za nje zisizo za lazima, akaanzisha kampeni ya usafi wa mazingira kwa kushika fagio mwenyewe, sheria mpya ya madini na kuzuia makinikia za Acacia, pia kule kutosafiri hata baada kualikwa na mataifa makubwa pekee ni kujulikana. Kutotembea na bakuli kwa kiongozi ni heshima ya pekee ambayo rais wetu amejipatia. Au wewe ulitaka awe anakwenda kunywa divai huko baada ya vikao visivyo na tija?
Mbona unageuza mada? Umesema anakubalika sasa hivi unasema tena wananyima misaada, huko ndo kukubalika au kukataliwa?
Vitu vizuri vingi kafanya hata mi nakubali, ila hilo halimaanishi anakubalika dunia nzima, unajua dunia nzima wewe? Umezunguka hata kufika Kenya tu tusiende mbali? Hakuna mtu anamjua magufuli nje ya afrika mashariki zaidi ya viongozi wachache ambao wamepewa kazi ya kushughulika na ukanda huu.
Mi sio pingapinga kila kitu, napinga vitu ambavyo ni vya kijinga na sio vya kweli, napenda kua neutral kwenye mambo kama haya na kutumia akili sio kama matahira wengi mnakubaliana na kila jambo hata kama ni la kijinga.
Vizuri alivyofanya Magufuli
1. Bandari
2. Kukataa kuingia mikataba ya kijinga na wachina
3. Safari za nje za ovyo kajitahidi sana kuzizuia
4. Wakwepa kodi wengi sasa wanakamatwa
5. Kajitahidi kubana matumizi
6. Anapenda vya nyumbani kwanza, kama juzijuzi swala la TTCL, ni vizuri sana TTCL ifanikiwe maana inamilikiwa na watanzania, kampuni nyingine hizi ni hela tunawapa wanabeba wanapeleka kwao hela yetu inashuka thamani, hakuna hela kwenye mzunguko zote tunabeba tunawapa foreigners wanaondoka nazo.
Vibaya alivyofanya
1. Bashite anakumbatiwa mno na ujinga wote anaoufanya
2. Anajiona mungu, akisema kitu kasema kifanywe anavyotaka yeye bila kuquestion, ukiquestion tu jela
3. Uhuru hakuna, waandishi wa habari wanalijua hilo, ukipata data ukapublish serikali inataka upublish data wanayokupa wao hata kama ni ya uongo, ukipublish ukweli jela au kufungiwa na fine juu
4. Hela zinapotea hazijulikani zimeenda wapi na hataki kua questioned, taarifa ya CAG inajieleza vizuri
5. Priority za kijinga, hela anajipangia anavyotaka
6. Decisions zinatolewa juu juu tu bila kukaa na kufanya analysis ya kutosha, akiamua kitu ndani ya sekunde ashatangaza, hajakaa kufikiria side effects zake huko mbeleni ni nini
7. Ubabe wake wa kijinga unapelekea kuharibu uchumi, mfano mzuri kua na youtube channel dunia nzima tanzania pekee ndiyo sehemu wanayohitaji ulipe leseni ya 1mil kwa mwaka kabla hujaanzisha, huu ni upuuzi wa hali ya juu, badala ya iwe bure watu wajitahidi wengi waone kama watafanikiwa wakifanikiwa waregister biashara yao walipe kodi, mtu anazuiliwa kabla hata hajaanza, hivi unategemea mtanzania gani atatoa 1m kabla ya kufungua channel? Hii yote sababu ya ubabe wake kushindana na watu wanaompinga youtube, alivyo mjinga kichwani hajui wanaompinga wengi wapo nje ya nchi zile channel hawafungi, kitu kinachofanywa na mtu moja kinaua biashara za watu zaidi ya elfu moja? Kalio kabisa
8. Hajui kujicontrol, ana hasira za kijinga sana huyu mzee, unaweza hata simama kwenye mkutano wake akakuangalia kwa jicho baya ukasikia funga huyo analeta usumbufu, ndiyo dalili za udikteta huo kama hamjui, hana compassion mzee mzima anaishi kama yupo jeshini
9. Anapenda sana misifa kitu kinachopelekea anaongea ujinga ili kufurahisha watu, mfano anavyoita wanafunzi vilaza, rais mzima na akili zake badala ya kuwapa watu moyo wakae wasome anawavunja moyo kabisa, tunakaa na failures tu hawana mbele wala nyuma wanalala siku nzima wamekata tamaa. Ni vizuri kua na utu sometimes na kuangalia ukisema nini kitakua na faida, kufurahisha watu wakacheka kwa muda ila unaleta permanent damage sio kitu kizuri. Nalaumu ushamba wake kwa hili.
Magufuli ni binadamu kama wengine, ana mazuri yake na mabaya yake pia. Nyie mnaojifanya kutetea kila kitu hua mnanishangaza sana, na wanaopinga kila kitu wote group moja tu, matahira. Tumieni akili acheni ukilaza