Rais Magufuli akubalika duniani kote

Rais Magufuli akubalika duniani kote

Joined
Sep 14, 2011
Posts
8
Reaction score
45
RAIS Magufuli kushangiliwa kwa Nguvu Afrika kusini Ina Maana gani kwa Wapinzani wake??

Marais wengi wameenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini 25 May 2019 , lakini mara baada ya jina la Rais wa Tanzania John Magufuli kutajwa kwamba anaingia uwanjani ,Raia wa Afrika kusini walisimama na kushangilia kwa nguvu sana.

Umati mkubwa wa wananchi umelipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuaishwa kwa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa leo Jumamosi Mei 25, 2019

Kwa Mtazamo Wa kawaida hii inaashiria Rais Magufuli Kukubalika KITAIFA NA KIMATAIFA,

Kwa upande wa upinzani Utaendelea Kubeza na kukejeli Hatua Ambazo anafanya Rais Magufuli ila Kwa upande Wangu wapinzani Kufanya hivyo ni Sahihi kwao kwasababu Hauwezi Kutafuta Serikali kwa kusifia Serikali Iliyopo.

Wananchi Wanatakiwa kufahamu Wapinzani wanatekeleza Majukumu Yao,ila Ukweli wanaufahamu na Ukweli siku zote Haufichiki.

Kwa Wapinzani Kwasababu ya Kupinga hata yale Mazuri yanayofanywa Na Rais Hawachelewi Kusema .

"Waliomshangilia Rais Magufuli Afrika kusini Ni wanaCCM Walisombwa na Magari"

Ndugu Kwa sasa Hatuhitaji Kukosoa kila Kitu Tunahitaji kusema pale Panapohitaji Kusema,
Tuna Vijana wengi Ambao wana uwezo Mkubwa wa kulisemea Taifa hili na Sio Kushambulia Viongozi kwa Matusi Mitandano.

Agenda ya vijana wa Upinzani kwa sasa ni

1.MAGUFULI KUMPIGA PICHA DK Kikwete na Rais wa A.Kusini Ramaphosa.

2. Rais Magufuli kaongea Lugha gani A.kusini.

Hatuwezi Kuendelea kuwa Na vijana wa upinzani Wenye Maono Madogo Kiasi Hicho, Wanawaza PICHA NA LUGHA, Tunahitaji kuwa na Vijana ambao wanakuja na Mikakati ya Kuendeleza Uchumi, Umoja wetu Kitaifa na Uzalendo.

Hakika Magufuli Anakubalika kidunia.

KWA STYLE AMBAYO VIJANA WA UPINZANI WANAENDA NAYO, HATA KAMATI KUU YA CHADEMA NDIO IKIWA TUME YA UCHAGUZI CCM INASHINDA KWA KISHINDO.

ASANTE.

Road To 2020.
Florian Musumi
Mwanza.
 
Siko upinzani mkuu but to be honest hivi vi thread uchwara vya kusifia daily mnaboa mkuu,mnafanya wote tuonekane bogus.
Ni, kweli mkuu. Yaani huyu mleta mada hajui Walichoshangilia ni Tanzania na hawajamshangilia mtu. Ni kumfahamisha tu, kwamba hata angekwenda yeye, walipotaja tu jina la Tanzania wangeshangilia. Hii ni kwa sababu ya jitigada za Tanzania kumuunga Mkono kwa hali na Mali Marehemu Nelson Mandela ktk kupigania uhuru wa South Africa . Ila humu JF bahati mbaya pia kuna Mabumunda ambayo pia yanajiita great think
 
True mkuu jili lipo wazi kabisa kiasi kwamba kumkubusha mtu hua naona hata uvivu,sasa inafika kipindi vi thread km hivi naona labda anasaka uteuzi au kitu kingne
 
Acheni uongo nyie vipofu. aliyeshangiliwa sana ni Mnangwanga wa Zimbabwe.....

Hawa wengine mliona kama walikuwa wanashangiliwa ni kwa sababu gwaride lilishaanza kuingia uwanjani hivyo walikuwa wanashangilia gwaride na sio mtu
 
Masifa ya kijinga kabisa, kushangiliwa au kukubalika huko kunaongeza kitu gani ktk mfuko wako? Umeandika kishabiki sana japo kuna mahala umeongea fact juu ya vijana wa upinzani lkn hata hivyo ningekushauri uandike kuhusu vijana kwa ujumla maana sio Upinzani tu hata upande wa pili vijana wengi ni watu wa kusifia ujinga kwa lengo ama la kutafuta vyeo au kulinda madaraka waliopewa, hakuna tena critical thinkers miongoni mwa vijana wengi zaidi ya ama kupinga ukweli au kusifia ujinga na wengi wetu tumekua wapiga debe wa wanasiasa.
 
Ni, kweli mkuu. Yaani huyu mleta mada hajui Walichoshangilia ni Tanzania na hawajamshangilia mtu. Ni kumfahamisha tu, kwamba hata angekwenda yeye, walipotaja tu jina la Tanzania wangeshangilia. Hii ni kwa sababu ya jitigada za Tanzania kumuunga Mkono kwa hali na Mali Marehemu Nelson Mandela ktk kupigania uhuru wa South Africa . Ila humu JF bahati mbaya pia kuna Mabumunda ambayo pia yanajiita great think
Anajua sana kisa cha wasauzi kushangilia anajichetua akili mzee wa buku 7 huyo.
 
Huenda mko sawa wote shida ni kwamba hamuelewi rais yoyote mwalikwa lazima kitokee hicho kitu.utofauti upo lakini Si kigezo cha kumbeza MTU.
 
Ni, kweli mkuu. Yaani huyu mleta mada hajui Walichoshangilia ni Tanzania na hawajamshangilia mtu. Ni kumfahamisha tu, kwamba hata angekwenda yeye, walipotaja tu jina la Tanzania wangeshangilia. Hii ni kwa sababu ya jitigada za Tanzania kumuunga Mkono kwa hali na Mali Marehemu Nelson Mandela ktk kupigania uhuru wa South Africa . Ila humu JF bahati mbaya pia kuna Mabumunda ambayo pia yanajiita great think
Kama hawakumshangilia mtu mbona na Kikwete alitajwa lakini alipotajwa Magufuli ndo alishangiliwa?
 
Kwani kushangiliwa kuna tatizo gani? Pale uwanjani kulikuwa na watu wa mataifa tofauti na watanzania walikuwepo sasa kuna ubaya gani kwa watanzania kumshangilia rais wao?
 
Wewe ndiye unaewabeza Wapinzani wa Magu. Unaposema Dunia nzima wanamkubali unamaanisha Mh Lissu kushambuliwa kwa risasi huku akikaa kimya ama kushangilia upuuzi ule, Dunia wanaunga mkono??
 
Back
Top Bottom