Rais Magufuli ahudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu, aelezea kusitishwa ajira za serikali

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Rais Magufuli katika hotuba yake kwenye maadhimisho haya ambayo yamehuduriwa na Magavana na Naibu Magavana wa Benki Kuu, Rais Magufuli pia amesema baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili Benki Kuu ni usimamizi wa huduma za kifedha ili kuwafikia watanzania hadi vijijini.

Aidha Rais Magufuli amesema Benki Kuu inatakiwa kudhibiti matumizi ya dola ili kulinda thamani ya shilingi, kulinda ubora na usalama wa matumizi ya kielekroniki pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.

Wakati huo huo Rais Magufuli amesema uamuzi wa serikali kusitisha ajira mpya pamoja na kupandisha vyeo watumishi wa serikali ni wa muda mfupi ili kudhibiti tatizo la watumishi hewa. Amesema zoezi hilo halitazidi miezi miwili ili kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.

Awali akielezea historia ya Benki Kuu tangu kuanzishwa kwake June 14 mwaka 1966, Gavana Beno Ndulu amesema Benki Kuu imeweza kujiendesha yenyewe bila ya kutegemea serikali.

Katika maadhimisho hayo Rais Magufuli pia amezindua Sarafu ya Shilingi Elfu hamsini kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na kupokea Hundi ya Shilingi Bilioni nne ikiwa ni mchango wa ajili ya madawati.

Magavana na Naibu Magavana kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa wamehudhuria maadhimisho haya.

VIDEO:


89565df8-8e47-4882-8d40-84f20b96bf3c.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
DSC_6435.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam
p14.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam
DSC_6573.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania
DSC_6649-1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Magavana na Manaibu Magavana na menejimenti ya BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania.


 
Najaribu kuwaza hivi B.O.T wana generate income kama kama taasisi zingine za serikali na kama ndivyo mishahara ya watumishi inatokana na hayo mapato au ni budget kutoka serikalini?????

Na je mwaka wa fedha haujaiisha hizo billion 4 kama mchango wa madawati zimetoka wapi na sidhani kama wali bajetia kwenye budget ya mwaka 2015/2016
 
Sasa anawakumbusha BOT majukumu yao ya kila siku? Si angesalimia tu na kukaa badala ya kuingilia fani za watu kama hakua na jipya? Kwanza naona amejitahidi maana asingesita kuamrisha wachape manoti mengi kumaliza tatizo la fedha.Maana kule Uganda miaka hiyo Rais Idd alimuamuru gavana afanye hivyo
 
Kuna watu kuwapata ni rahisi.Nilitaka kuwatoa povu.Kama kawaida umekuja kwa hasira kweli maana uliweka thread kwa kumpamba kwelikweli.

Nimecheka sana Response
 
Kweli siasa kitu cha hovyo sana leo ktk kupiga picha mtu kama makonda anakaa front huku watu na elimu zao wanasimama nyuma
Acha wivu wa kinyama. Hao wote wa mbele unawajua kwa majina na nyadhifa zao ndiomaana umeweza kumtaja Mh Makonda. Hao wa nyuma huwajui pengine majina na nyadhifa zao. Hilo la kufahamika latosha kutambua hadhi yake kuwa mbele na ndicho kigezo muhimu. Kataa kubali ndivyo ilivyo.
 
Kweli siasa kitu cha hovyo sana leo ktk kupiga picha mtu kama makonda anakaa front huku watu na elimu zao wanasimama nyuma

Hapa ni suala la protocol na si kingine...elimu haingii kwenye protocol...Makonda ni RC wa Dar es Salaam, na shughuli hizi zimefanyika mkoani mwake...ndivyo siasa ilivyo, sasa whether siasa ni 'hovyo' (kama unavyosema wewe) hilo ni suala jingine...lakini kikubwa kingine ni kuwa everything in this world is politics, iwe ni kwenye uchumi, biashara na kila kitu ni politics...wengine wanasema politics is a dirty game ....
 
Na wale watumishi hewa wa BOT aliosema ana orodha waondolewe ndani ya siku 14 kasemaje...jamani
 
Kweli siasa kitu cha hovyo sana leo ktk kupiga picha mtu kama makonda anakaa front huku watu na elimu zao wanasimama nyuma
Kila aliyoko pale angeweza kukaa ila walipeana nafasi kulingana na heshima/cheo lakni tushangae mh.alikuwa anawapiga kikumbo wenzake.
 
Back
Top Bottom