Rais Magufuli aguswa na kifo cha Dkt. Reginald Mengi

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1086069

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma Salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi.

Kifo cha Dkt. Mengi kimetokea usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 2, 2019 huko Dubai katika falme za Kiarabu. Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika;

"Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara," ameeleza Rais Magufuli.
 
Rest in Peace Mzee. Utakumbukwa kwa mengi kama lilivyo jina lako. Kuanzia kwenye sekta ya mazingira, viwanda, vyombo vya habari hadi futari yake.😥
 
Tunatembea na kifo at our side. RIP mzee Mengi. Pole zake nyingi sana Miss Jacqueline Ntuyabaliwe

JM.png
 
Ukisikia ametuachia pengo ndiyo huyu sasa..
Mzee vp lkn usitegeme utaenda kupiga hela hpo huo ni msiba kamati yke ni special haina ujanjajanja kama wa wale
Maana we hukawahi kuvamia shuguli....

Ova
Hahahaa......... Nimekusoma mkuu ni imani yangu vikao vya msiba huu hamtafanyia Bar!
 
Kwani huyu ndiye yule wa Bongo movie?
Ukisikia ametuachia pengo ndiyo huyu sasa..
Mzee vp lkn usitegeme utaenda kupiga hela hpo huo ni msiba kamati yke ni special haina ujanjajanja kama wa wale
Maana we hukawahi kuvamia shuguli....

Ova
 
Mtu mhimu sana kwenye nchi yetu ni regnard mengi..R.I.P
 
Back
Top Bottom