Rais Magufuli afuta shamrashamra za miaka 52 ya Muungano, fedha zikajenge barabara Mwanza

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Lakini mapumziko yapo palepale
bb796336-6397-4c2f-b159-63f217b01029.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.

Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya "Mwanza Airport' katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULUChato04 April, 2016

Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yafana sana Mjini Dodoma Aprili 26, 2017

Pesa za sherehe ya Muungano iliyoahirishwa zigawiwe sawa Tanzania bara na Zanzibar

Rais Magufuli aadhimisha sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Jiji la Dodoma
 
Hii ni style ya kupunguza mzigo wa utekelezaji wa majukumu/ahadi

Hata hivyo itakuwa ni vizuri wakatutajia na kiasi kilichokuwa kimetengwa mwaka jana kwa sherehe hizi ili tuweze kulinganisha maana hatutarajii ongezeko kubwa.

Otherwise sio uamuzi mbaya.
 
Uamuzi mzuri kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya taifa.

Hata wanaopata Vinywaji na vyakula katika sherehe hiyo ni watanzania ambao mapato yao kwa mwezi ni zaidi ya Tsh millions. It's high society and elite flock.

Hii dhana ya alichonacho ataongezewa lazima tuondoe kama tunataka taifa lenye misingi ya usawa.
 
Hii ni style ya kupunguza mzigo wa utekelezaji wa majukumu/ahadi

Hata hivyo itakuwa ni vizuri wakatutajia na kiasi vha fedha kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya mwaka huu na pia watutajie na kiasi kilichotumika kwa mwaka jana kwa sherehe hizi ili tuweze kulinganisha maana hatutarajii ongezeko kubwa.

Otherwise sio uamuzi mbaya.


Ukisoma vizuri kiasi kimetajwa kwamba ni Bilioni 2!
 
Back
Top Bottom