Rais Magufuli afanya mazungumzo na Bilionea Dangote

Yule waziri alietuambia jamaa anataka Gas ya bure nimemuona jisura Lake nyuma anashindwa hata kutazama camera,
 
Wabongo bana juzi tu hapa kuna mtu alitoa taarifa ya utapeli wa dangote tena kutoka lumumba kupitia media na mawazir waka dhibitisha hilo watu wakasema ukosefu wa ajira vijana wa ccm wakasema ooh nendeni nyie wapiga dili nyie leo yamekua ya ukawa je muulizeni wazir wa ccm amekubali kutoa gesi bure au kwa bei ananayotaka yeye mana naona watu wamebadilika upande tena

Hapo ndipo wapiga dili walipotaka kuingia, nafikiri umesikia wameshindwa na kulegea
 
Mkuu hivi wapiga dili wanapata wapi jeuri ya kumzungusha mwekezaji wa maana kama Dangote! Ina maana Serikali (Wizara ya aridhi) ilikuwa haifatilii kwa karibu kinacho endelea nchini? Mbona Waziri Lukuvi aliwahi kutoa tamko kwamba mwekezaji yeyote akizungushwa au kulazimishwa kulipia/nunua aridhi kwa hela ndefu atawachukukia hatua kali wahusika wote, sasa imekuwaje mpaka Dangote atoe malalamiko yake kwa Dk.Magufuli is this normal?
Hii awamu hawana nanafasi watashindwa na watalegea siktk ili tuu hata kwa mengine pia wajue ukinusa unalambwa mkono
stay in.....!
 
Ungeweka na ushahidi jinsi wanavyohusika, otherwise suala maendeleo ikiwamo maendeleo yako binafsi hayana itikadi.
 
Why hawajaweka wazi kuhusu bei ya gasi? Why Dangote alazimishwe kununua malighafi Tanzania? Sheria ipi imetumika? Ile dollar 3 iliongezwa na nani kwa instructions za nani na zinaenda wapi?
Umeuliza maswali ya kitoto sana
 
Unafiki upo wapi sasa? Watu wengine bora muwe mnanyamaza tu.

Mnahangaika kuona nchi inarudi nyuma.

Kuweni na aibu.
Unafiki?...'double standard' katika ubora wake
...Je mawaziri wake waliopishana kauli kwa kumponda Dangote atawatumbua?
Mwingine alisema Dangote alikuwa anataka gesi ya bure

::IKULU, DAR: Rais Magufuli leo afanya mazungumzo na Bilionea Dangote::

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.

Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.

10 Desemba, 2016.
 
Why hawajaweka wazi kuhusu bei ya gasi? Why Dangote alazimishwe kununua malighafi Tanzania? Sheria ipi imetumika? Ile dollar 3 iliongezwa na nani kwa instructions za nani na zinaenda wapi?

Kama ulikuwa hujui pata shule hapa:

Sheria ya madini ya mwaka 2009 inazuia kuagiza malighafi endapo zinapatikana hapahapa kwetu (locally available), hivyo Dangote sheria hii inamzuia kuingiza malighafi hizo kwa kuwa zipo zinapatikana Tanzania!
 
Mwijage anaomba weekend isifike,si unajua weekend huwa ina tendency ya utumbuaji and he is likely to be the next victim
 
Nauliza tena, je nani amemfuata mwenzake kuomba yaishe? je wamempa discount aliyoitaka?
Inahusu nini! Halaf ukishajua? Nani kakwambia anataka discount. Tumeshawaahtukia nyinyi wapiga dili. Mmekosa ulaji basi. Mmetumika kijinga na wenye pesa sasa hivi hamna pa kukimbilia. Ulof.a na u.p.umb.a.f huo
 
Sana mkuu.. Wale ni mbweha sio watu!

Mm nlisema tangu huu mgogoro unaanza kwamba selikari haiwezi kumhujumu muwekezaji huo utakuwa wendawazimu!

Pale kulikuwa na watu wana maslahi yao! Alafu hivi chadema hiki kiwanda kikifungwa faida yenu ni nini? Maana urais hamtapata na bado wananchi watakuwa wamekosa ajira!
Sasa wewe huoni raisi mwenyewe amekili kuwa kulikua na tatizo ila ninyi ndio mlikuwa mnabisha kuwa mambo shwari LA aondoke. Bila kelele za chadema Ndangote angehujumiwa. Ahsante chadema kwa kuokoa hili
 
Mitandao na baadhi ya vyombo vya habari ni wazushi, wanapenda kukuza mambo. Pia kuna baadhi ya watu wana mtimanyongo walishangilia uzarishaji uliposimama, eti kisa upinzani.Acheni roho za korosho kuweni wazalendo tuiombee nchi yetu mema. Pia tumuombee raisi wetu mpendwa.
 
Back
Top Bottom