Rais Magufuli aanzishe chama kipya akiwa Ikulu ili apambane na Ufisadi, ndani ya CCM hataweza

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Napenda niweke kumbukumbu vizuri Rais Magufuli ana uchaguzi wa vitu viwili

Moja kuanzisha chama kipya akiwa Ikulu kama Bingu wa Mutharika wa malawi ili kupambana na ufisadi sawasawa. nje ya hapo hawezi fanya kitu hata kidogo anatudanganya tu. Angalia mambo yalivyo magumu mpaka unatumia hela ya maafa?

Pili kuungana na waliomtangulia katika kupiga madili na kuendeleza ufisadi na ndo mana lazima akwame kwa sababu walioharibu nchi ni CCM na mafisadi wako CCM na anafanya nao kazi na ndo watakaommaliza

Sasa ivi anahemea mipira ingawa mbishi ila ukweli siku zote haufukiwi angalia ajira hamna, watoto wamerudishwa nyumbani bodi ya mikopo imeshindwa kuwapa hela, stahiki za wafanyakazi kashindwa kuwapa anasingizia wafanyakazi hewa.

Angalia kila kitu kiko hoi ukiuliza eti hao wanaolia ni wapiga dili ngoja mjidangane muda unazidi kuyoyoma hakuna jipya aibu tupu kila kona

kwa hiyo rais hana jipya bila kufanya maamuzi nagumu ya kuanzisha chama kipya akiwa IKULU, hapo vita hii atashinda nje ya hapo awamu hii inaweza kuwa ya mwisho kwake.

Think Big Magufuli if you realy mean what you are trying to convice us as changes
 
Akianzisha chama kipya,atachafuka kuliko hapo alipo.
Na kuhusu maisha kuwa magumu,aache kung'ang'ania itikadi za ujamaa katika kuiongoza tanzania,awaache wawekezaji na wafanyabiasha wafanye kazi zao bila ya kuwatishia,wakati huohuo alegeze kidoogo kwenye kodi.
 
hawezi chafuka kwa sababu bado anaaminiwa sana watu wengi hsiba yake ndo inapanda zaidi
 
Mleta mada hoja yako ni nzuri..

Lakini nafikiri.. na huu ni mtazamo wangu.. JPM ameshachelewa kufanya hilo unalotaka alifanye. Kama angekuwa na guts za kufanya hivyo pale pale alipoingia Ikulu angefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Lakini kwa sasa ameshajipambanua na kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa namna gani.. Ana dalili zote za kupenda kuburuza wengine.. Ana dalili zote za kutaka analotaka yeye liwe ndio lazima liwe... Ana vimelea vya Udikteta.. Sio mtu wa kusikiliza ushauri (tunavyosikia sikia) Hata aanzishe chama now hatopata watu wa kumuunga mkono...

It's too late Brother.
 
Maamuzi magumu yalikuwa ni kumkata fisadi tu...na yalishafanyika.
Toka wamkate fisadi hakujawahi kuwepo ufisadi tena serikalini.
Hata kula hela za rambirambi walizochangishana mashetani kwa ajili ya Kagera haijatokea tena toka akatwe fisadi.
Ktk mahakama ya mafisadi ameenda mmoja tu(huyo aliyekatwa)
Kwa sababu fisadi alikatwa, JPM hataki kufukua makaburi .........
 
Mleta mada hoja yako ni nzuri..

Lakini nafikiri.. na huu ni mtazamo wangu.. JPM ameshachelewa kufanya hilo unalotaka alifanye. Kama angekuwa na guts za kufanya hivyo pale pale alipoingia Ikulu angefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Lakini kwa sasa ameshajipambanua na kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa namna gani.. Ana dalili zote za kupenda kuburuza wengine.. Ana dalili zote za kutaka analotaka yeye liwe ndio lazima liwe... Ana vimelea vya Udikteta.. Sio mtu wa kusikiliza ushauri (tunavyosikia sikia) Hata aanzishe chama now hatopata watu wa kumuunga mkono...

It's too late Brother.
Chezea magwiji wa ccm weweee,washa mmoderate faster
 
Cshangai kina jingalao na barbarosa wanavojibu hoja humu.. mmeishiwa nyinyi,nmeona picha za marehemu mawazo Leo nmeogopa sana.kwanini mlimuua jmn?mbona mmemfanya vile?kweli?Mungu mmoja ana endelea kujibu.
 
nakuambia hivi nyie mnaojificha kwenye mambo ya lowasa na kutumia kigezo cha kuhamia cdm hamuwezi kusafisha ccm dhidi ya ufisadi na umaskini wa nchi yetu hakuna mwingine dhsmbi iko na ccm tu
 
Toka wamkate fisadi hakujawahi kuwepo ufisadi tena serikalini.
Hata kula hela za rambirambi walizochangishana mashetani kwa ajili ya Kagera haijatokea tena toka akatwe fisadi.
Ktk mahakama ya mafisadi ameenda mmoja tu(huyo aliyekatwa)
Kwa sababu fisadi alikatwa, JPM hataki kufukua makaburi .........
Uzushi wa kuliwa kwa fedha za maafa ni jitihada za kuzima kashfa ya lwakatare kujifungulia akaunti binafsi ya kukusanya michango na hatimaye kuitafuna...tuelewane
 
Yeye ana usafi gani tofauti na wenzake?Mbona hata mali na madeni yake(kama anayo) ameshindwa kututangazia?
 
Uzushi wa kuliwa kwa fedha za maafa ni jitihada za kuzima kashfa ya lwakatare kujifungulia akaunti binafsi ya kukusanya michango na hatimaye kuitafuna...tuelewane
Ile taarifa hukuisikia kuwa sh.5.4 b imeelekezwa kwenye taasisi za serikali na kwamba wahanga wasitegemee fedha hizo?
Je, kuna sehemu ambapo serikali imeonesha pesa iliyochangwa (sio na UK) imekabidhiwa kwa nani ili iwafikie wahanga wanaotaabika hadi sasa?. Tuelewane mkuu
 
ufisadi,ujangili,rushwa,utapeli.........aisee nyie weny chama chenu Mungu anawaona
 
Mleta mada hoja yako ni nzuri..

Lakini nafikiri.. na huu ni mtazamo wangu.. JPM ameshachelewa kufanya hilo unalotaka alifanye. Kama angekuwa na guts za kufanya hivyo pale pale alipoingia Ikulu angefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Lakini kwa sasa ameshajipambanua na kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa namna gani.. Ana dalili zote za kupenda kuburuza wengine.. Ana dalili zote za kutaka analotaka yeye liwe ndio lazima liwe... Ana vimelea vya Udikteta.. Sio mtu wa kusikiliza ushauri (tunavyosikia sikia) Hata aanzishe chama now hatopata watu wa kumuunga mkono...

It's too late Brother.
kuna ukweli kidogo ila mbele ya safari atakwama vibaya sana na hakika atajuta sana mana hao ndugu zake wanammaliza tarayibu ka mgonjwa wa ukimwi
 
Uzushi wa kuliwa kwa fedha za maafa ni jitihada za kuzima kashfa ya lwakatare kujifungulia akaunti binafsi ya kukusanya michango na hatimaye kuitafuna...tuelewane
yaani akili yako ni sawa na id yako ila sishangai huko kwenu ili upate cheo inabid uwe chizi kidogo
 
Back
Top Bottom