KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Walimu wa chuo kikuu siyo watu wa field. Hawana uzoefu wa kutengeneza mitambo. Hawa ni watu wa kufundisha principles lakini ukiwapeleka field, utashangaa. Wanaweza kuzidiwa na fundi wa darasa la saba.
Tunawaona wanapokuja kuwasimamia wanafunzi wakati wa field. Kitu kidogo ambacho mfanyakazi wa kawaida ambaye yupo kwenye field, unamwuliza mara moja, na anakupa jibu sahihi, mhadhiri wa chuo kikuu itamchukua hata mwezi kukupa jibu, na wakati mwingine anakupa jibu siyo sahihi.
Aiseee!! Bams?
"----kitu kidogo ambacho mfanyakazi wa kawaida anaweza kukifanya mara moja, kinamchukua mhadhiri inamchukua mwezi?"
Wacha bhwana!. nakubali, mhadhiri anaweza asikupe jibu la kiwandani kwako papo kwa papo, kwa sababu ya mazingira ya kiwandani kwako hana uzoefu nayo, lakini akae mwezi hata wiki?
WaTanzania tuache utani huu Bhwana.