Rais Magufuli aagiza kiwanda cha Buko kuanza kazi ya kubangua korosho mara moja. Waziri aita wanasayansi wa UDSM haraka

Hivi ni nani anamdanganya Mh. Rais?

Mkuu wa Mkoa wa Lindi alimuambia waziri mkuu Mh. MKM kuwa kile kiwanda hakiwezi kubangua hata kg 5 za korosho kutokana mashine zake chakavu, nunueni mitambo na sio kulazimisha kubangua tu korosho.
hahahaja ht 5kgs?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘Š
 
Waziri wa biashara amesema ameagizwa na Rais Magufuli kuhakikisha kiwanda cha Buko kilichosimama kufanya kazi kinaanza kazi ya kubangua korosho mara moja.

Kufuatia agizo hilo waziri amewataka mafundi wabobezi na wanasayansi wenye ubunifu kutoka Udsm wafike haraka Mtwara na kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kazi ndani ya wiki moja.

Source ITV habari!
Naona watu wamechanganyikiwa!, hivi unaita mafundi toka Udsm! toka lini Udsm ikawa na mafundi wabobezi?. Hata enzi ya FoE, kule kwenye Mechanical Engineering hao watu hawakuwepo Udsm, Kilichokuwa kikifanyika waliomaliza Mechanics hapo walikuwa wakitafutwa kwenye maeneo yao ya kazi baada ya kupata uzoefu wa kutosha kwenye vitendo, ndiyo mnataka kufanya ya kina kina Profesa Msoro kuchunguza Makinikia wakati hawajawahi kukaa maabara ya uchunguzi wa madini hata mwaka mmoja mwishowe wanaleta ripoti ya kufikirika ambayo haijawahi kutokea duniani mradi wamfurahishe Jiwe. Tatizo la serikali hii ni mihemko mingi bila kutumia maarifa na ushauri wa wenye uzoefu wa kutatua matatizo
 
Hahahah jeshi limebangua kwa meno mpaka wakawa vibogoyo. Nimeiona hiyo habari muda mfupi.

Namshauri Jiwe wale wasomi wa Chuo cha UDSM badala ya kumsifia tuuu basi awakamate wote kuanzia Bashiri, Kalamaganda na Vibudu awafungie ndani ya maabara kama ilivyokuwa kwa Enrique Feki na washirika wake waliofungiwa na Hilter ndani ya maabara bila kupewa chakula kwa miezi kadhaa ndipo wakaweza kutengeneza Sythetic runner. Na walikuwa wanachanganya reagent ndipo wanakunywa ili wasife maana unachanganya sodium na naniliu unapata protein unakunywa unaishi. Sasa awakamate hao wasifiaji kisha awafungie ndani nakuambie kesho korosho yote inabanguliwa kama unapiga pili
Nahisi ni muda tu unasubiriwa. Usishangae kesho wakaita waganga wote wa kienyeji waje wapige ramli kinachokwamisha ubanguaji wa korosho. Yetu macho.
 
Watawala kuna kitu wanakosa.

Wanashindwa kujua nani anaweza kufanya nini kwa ufanisi. Wao wamelewa na titles za Dr au Prof., hata kama titles hizo hazina msaada wowote. Hivi ni nini cha maana kwa mfano Prof. Kabudi ameisadia nchi tangu aingizwe serikalini zaidi ya kuzidi kumpotosha zaidi Rais?

Kwa sababu serikali bado haijui who is the right person for a particular task, for sure it will continue failing to meet its expectations.

Walimu wa chuo kikuu siyo watu wa field. Hawana uzoefu wa kutengeneza mitambo. Hawa ni watu wa kufundisha principles lakini ukiwapeleka field, utashangaa. Wanaweza kuzidiwa na fundi wa darasa la saba.

Tunawaona wanapokuja kuwasimamia wanafunzi wakati wa field. Kitu kidogo ambacho mfanyakazi wa kawaida ambaye yupo kwenye field, unamwuliza mara moja, na anakupa jibu sahihi, mhadhiri wa chuo kikuu itamchukua hata mwezi kukupa jibu, na wakati mwingine anakupa jibu siyo sahihi.
Ninaapa kwamba wewe ulieandika haya huna PhD hata masters huna. Nasema hivyo kutokana na uelewa wako wa mtu mwenye title ya Dr au Prof!
 
Waziri wa biashara amesema ameagizwa na Rais Magufuli kuhakikisha kiwanda cha Buko kilichosimama kufanya kazi kinaanza kazi ya kubangua korosho mara moja.

Kufuatia agizo hilo waziri amewataka mafundi wabobezi na wanasayansi wenye ubunifu kutoka Udsm wafike haraka Mtwara na kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kazi ndani ya wiki moja.

Source ITV habari!
Huyo waziri aliyeita wanasayansi wa udsm ana akili timamu!? Yaani mwanasayansi wa Tanzania ni wa kwenda kufanya kazi ya ufundi wa mitambo iliyochakaa?
 
Walipeni wakulima hela zao.mnataka kubangua korosho za dhulma? Hamtafika mbali nawambia.jasho la mtu haliendi bure.
Mimi nashauri watetezi wa haki wafike Ntwara na Lindi na kuorodhesha watu wote ambao wamepeleka korosho lakini wameambiwa hawatalipwa. Inaonekana kuna dhuruma kubwa inafanyika kule
 
hivi kwa nini asiwaagize na psssf kuwalipa wastaafu mafao yao mara moja? au hili yeye halioni?tunateseka sana sisi tuliostaafu tulifanya kazi kwa uaminifu sana mpaka kufikia kstaafu,kwa nini mnatutesa?
 
Um
Watawala kuna kitu wanakosa.

Wanashindwa kujua nani anaweza kufanya nini kwa ufanisi. Wao wamelewa na titles za Dr au Prof., hata kama titles hizo hazina msaada wowote. Hivi ni nini cha maana kwa mfano Prof. Kabudi ameisadia nchi tangu aingizwe serikalini zaidi ya kuzidi kumpotosha zaidi Rais?

Kwa sababu serikali bado haijui who is the right person for a particular task, for sure it will continue failing to meet its expectations.

Walimu wa chuo kikuu siyo watu wa field. Hawana uzoefu wa kutengeneza mitambo. Hawa ni watu wa kufundisha principles lakini ukiwapeleka field, utashangaa. Wanaweza kuzidiwa na fundi wa darasa la saba.

Tunawaona wanapokuja kuwasimamia wanafunzi wakati wa field. Kitu kidogo ambacho mfanyakazi wa kawaida ambaye yupo kwenye field, unamwuliza mara moja, na anakupa jibu sahihi, mhadhiri wa chuo kikuu itamchukua hata mwezi kukupa jibu, na wakati mwingine anakupa jibu siyo sahihi.
Umeongea ukweli kiasi lakini nadhani kutakuwa na walimu ambao pengine wamekaa field kwa muda mrefu, pia nadhani watakuwa na matechnician kibao wenye uzoevu then wao watakuwa wakishusha principle zao na usimamizi, huwezi peleka technician site bila kuwa na supervisir.
 
Back
Top Bottom