Rais Magufuli aagiza kiwanda cha Buko kuanza kazi ya kubangua korosho mara moja. Waziri aita wanasayansi wa UDSM haraka

Hahahah jeshi limebangua kwa meno mpaka wakawa vibogoyo. Nimeiona hiyo habari muda mfupi.

Namshauri Jiwe wale wasomi wa Chuo cha UDSM badala ya kumsifia tuuu basi awakamate wote kuanzia Bashiri, Kalamaganda na Vibudu awafungie ndani ya maabara kama ilivyokuwa kwa Enrique Feki na washirika wake waliofungiwa na Hilter ndani ya maabara bila kupewa chakula kwa miezi kadhaa ndipo wakaweza kutengeneza Sythetic runner. Na walikuwa wanachanganya reagent ndipo wanakunywa ili wasife maana unachanganya sodium na naniliu unapata protein unakunywa unaishi. Sasa awakamate hao wasifiaji kisha awafungie ndani nakuambie kesho korosho yote inabanguliwa kama unapiga pili
Hitler ndo alikuwa anafanya hayo? Duuh Jamaa hakuwa wakispot
 
Jeshini hakuna wahandisi mitambo na umeme?? Kazi ya maprofesa na madr ni kufanya tafiti na kuvumbua... Hii ni maintenance and repair inahitaji vijana wajanja wajanja wa site sio watu waliobobea kwenye theory na kukariri principle's..

Nina uhakika hicho kiwanda ukiwapa vijana wa gerezani chini ya wahandisi wanne wa mitambo na umeme wazoefu wa field na fungu kinaamka mwezi tu..

No automation pale ni gears, shafts, conveyors, motors na old teknolojia.. Inatakiwa misasa ya kutosha, penetrating oils, diesel na petrol ya kutosha, lathe machine, drilling machine, milling machine na shaping machine za kawaida tu, tool boxes za kutosha, vernier caliper, micrometer, TUACHE SIASA HII NI DUNIA YA MATOKEO..
 
Watawala kuna kitu wanakosa.

Wanashindwa kujua nani anaweza kufanya nini kwa ufanisi. Wao wamelewa na titles za Dr au Prof., hata kama titles hizo hazina msaada wowote. Hivi ni nini cha maana kwa mfano Prof. Kabudi ameisadia nchi tangu aingizwe serikalini zaidi ya kuzidi kumpotosha zaidi Rais?

Kwa sababu serikali bado haijui who is the right person for a particular task, for sure it will continue failing to meet its expectations.

Walimu wa chuo kikuu siyo watu wa field. Hawana uzoefu wa kutengeneza mitambo. Hawa ni watu wa kufundisha principles lakini ukiwapeleka field, utashangaa. Wanaweza kuzidiwa na fundi wa darasa la saba.

Tunawaona wanapokuja kuwasimamia wanafunzi wakati wa field. Kitu kidogo ambacho mfanyakazi wa kawaida ambaye yupo kwenye field, unamwuliza mara moja, na anakupa jibu sahihi, mhadhiri wa chuo kikuu itamchukua hata mwezi kukupa jibu, na wakati mwingine anakupa jibu siyo sahihi.
Tunaamini sana kwenye vyeti kuliko hali halisi uwezo wa MTU,we uoni wamefukuzwa wataalamu wazuri mabingwa Kwa vigezo vya cheti cha 4 ,wamechukuliwa nje ya nchi ukienda Kenya,Botswana, Namibia nk wanapiga Kazi package nzuri wengi wanashukuru kufukuzwa wasingepata mazuri wayapatayo sasa
 
Waziri wa biashara amesema ameagizwa na Rais Magufuli kuhakikisha kiwanda cha Buko kilichosimama kufanya kazi kinaanza kazi ya kubangua korosho mara moja.

Kufuatia agizo hilo waziri amewataka mafundi wabobezi na wanasayansi wenye ubunifu kutoka Udsm wafike haraka Mtwara na kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kazi ndani ya wiki moja.

Source ITV habari!

Kwenye jambo kama hili mimi sinalo tatizo kabisa, tena tumechelewa sana kulianza.

Pawekwe tu utaratibu mzuri wa kufanya mambo kama haya. Hatuwezi kuwa watu wamesomeshwa miaka yote hii toka tupate uhuru, halafu tusiwe hata na uwezo wa kubangua korosho?

Wasomi hao wapo wapi, watafutwe popote walipo, hata kama wamejificha ndani ya siasa kama akina Maprof. Kabugi Kalamaganda. Watafutwe popote walipo, hata kama wamestaafu waende wakabangue korosho.

Vyuo vyote vyenye wataalam hawa ni lazima vianze kufanya kazi kwa njia tofauti. Viache kufundisha nadharia tu na kuachia hapo. Huko Costec, wanafanya nini kusaidia nchi ijikwamue kwenye tope hili?

'Brutality' ya aina hii ntaiunga mkono.

Fanya hivyo hivyo na kwenye viwanda vya madawa, ngozi, pamba, n.k.

Haya yakifanyika, na kuacha ubabe, uonevu, kupotea na mengine mabaya kama hayo "Nitaunga Juhudi"
 
Back
Top Bottom