voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Pengine Rais haelewi ukweli kwamba anachokihangaikia yeye kusaini kila siku huko sio kinachotusumbua wananchi huku mtaani.
Unazidi kusaini mikataba,huku hata ile michache ya awali hatujaona impact yake kwa maendeleo chanya,wala ufumbuzi wa kero yoyote.
Unazidi kutafuta wawekezaji,wakati hata Umeme ambao ni nguzo kuu ya uwekezaji ukiwa unahujumiwa mbele yako?
Huu ni ukweli,ingawa "Asali Gang"na wapambe wao humu JF kina Mwashambwa na wengineo,wako busy kutetea vitumbua vyao.hawataacha kutukana hoja kama hizi.
Kuzunguka nje ukisaini mikataba,bila kudhibiti matumizi mabaya na mabovu ya serikali.l hii ya CCM.
Bado tija ya hizo ziara haitaonekana kamwe!
Unazunguka nje kuomba Omba,wakati Unashindwa kutulia Ofisini kudhibiti Ufisadi ulioibuka kwa kasi,sekta zote nchini. Hii ni sawa na kujaza maji kwenye Gunia!
Unazunguka nje kusaini mikataba,badala ya wao kuja kuisaini ndani ya nchi yetu.
Ili mikataba hiyo itekelezwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Hii ni kwa maslahi mapana ya kina nani?
Unazunguka nje bila kutulia nchini mwako na kuzifanyia kazi changamoto lukuki zinazowakumba wananchi kwa sasa!
Badala yake Wewe ni Rais wa safari, Makongamano, warsha, mipango kazi, vikosi kazi.....huku ukiacha "Asali Gang" kuwa wasimamizi?
Rais kubali na uwasikilize wananchi.
Unayoyahangaikia wewe,sio yanayotusumbua sisi huku mtaani!
Huenda kama Mh, Rais wetu akifanikiwa kuongoza kwa miaka 10,akawa na rekodi ya pekee Duniani,kama Rais aliyesafiri na kutia saini mikataba Duniani kuliko Rais yeyote wa Afrika huko Awali.