Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Candid ni kweli, kama hawa wanaodai kujadili Muungano kama mlango ungekuwa umefunguliwa wasingefikia hapa hadi kusababisha machafuko. Ndio maana kuwazuia wamefikia hatua ya kutaka kupiga kura ya kutokukubaliana na Muungano.
Binafsi naona njia mbadala ya kulinda amani ya nchi yetu ni uwazi katika kujadili mambo yanayotuhusu kwa uhuru. Lakini kutoruhusiwa baadhi ya kero za Muungano hapo moto hauwezi kuzimika, wanachofanya ni kutuliza kwa muda lakini utaibuka tu. Bora kuruhusu yaishe.
Tukio la amani kuvurugia huko kisiwani Zanzibar na kusababisha mali za watu pamoja na baadhi ya makanisa kuchomwa serikali haiwezi kukwepa lawama kutokana na dalili za wazi watu kutaka mjadala wa Katiba mpya uende sambamba na kujadili Muungano wetu. Hakuna wenye kuchukia Muungano, ila kero mbalimbali zilizofumbiwa macho miaka nenda rudi ndizo zinazofanya watu wafikie hatu ya kuona sasa inatosha, tunataka tujadili Muungano wetu.
Kauli ya Rais Kikwete kabla na alipotangaza kamati ya kuratibu mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, alisema Suala la Muungano sisiguswe. Kauli hiyo inaweza kujenga maswali mengi na pengine kufikisha kwenye tukio la Zanzibar ukosekanaji wa amani kama ilivyotoke.
Ulimwengu wa leo utandawazi ndio unaofanya amani ipatikane, na pale wananchi wanaposhinikizwa kutogusa au kuongelea jambo linalowahusu hapo wanachukua njia nyingine ya kudai haki yao.
Busara kwa Rais wetu Kikwete kuruhusu Muungano ujadiliwe na wananchi katika mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya nchi, kwani kwa hali inavyoonekana sasa hivi jambo hilo halikwepeki kwa namna ye yote vinginevyo ni kukaribisha maafa zaidi ya yaliyotokea Zanzibar.
Huu Muungano nini faida kwetu? Huenda unatuongezea gharama za serikali tu.
Au uvunjwe kusiwe na chakujadili
Binafsi naona njia mbadala ya kulinda amani ya nchi yetu ni uwazi katika kujadili mambo yanayotuhusu kwa uhuru. Lakini kutoruhusiwa baadhi ya kero za Muungano hapo moto hauwezi kuzimika, wanachofanya ni kutuliza kwa muda lakini utaibuka tu. Bora kuruhusu yaishe.
Viongozi wachache hawataki muungano ujadiliwe kwenye katiba inayojadiliwa, wakati huohuo watu wa muungano huo wanataka ujadiliwe...sijui nani atashinda ...yetu masikio na macho ambayo wao hawana
Off course intakuwa amesurrender kwa huu ugaidi?Na akifanya vibaya atakuwa amewapongeza na kuwazawadia thier wishes.
Tukio la amani kuvurugia huko kisiwani Zanzibar na kusababisha mali za watu pamoja na baadhi ya makanisa kuchomwa serikali haiwezi kukwepa lawama kutokana na dalili za wazi watu kutaka mjadala wa Katiba mpya uende sambamba na kujadili Muungano wetu. Hakuna wenye kuchukia Muungano, ila kero mbalimbali zilizofumbiwa macho miaka nenda rudi ndizo zinazofanya watu wafikie hatu ya kuona sasa inatosha, tunataka tujadili Muungano wetu.
Kauli ya Rais Kikwete kabla na alipotangaza kamati ya kuratibu mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, alisema Suala la Muungano sisiguswe. Kauli hiyo inaweza kujenga maswali mengi na pengine kufikisha kwenye tukio la Zanzibar ukosekanaji wa amani kama ilivyotoke.
Ulimwengu wa leo utandawazi ndio unaofanya amani ipatikane, na pale wananchi wanaposhinikizwa kutogusa au kuongelea jambo linalowahusu hapo wanachukua njia nyingine ya kudai haki yao.
Busara kwa Rais wetu Kikwete kuruhusu Muungano ujadiliwe na wananchi katika mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya nchi, kwani kwa hali inavyoonekana sasa hivi jambo hilo halikwepeki kwa namna ye yote vinginevyo ni kukaribisha maafa zaidi ya yaliyotokea Zanzibar.
Mambo yote yanakwenda kwa utaratibu ili kila mtu aepuke lawama mwisho wa siku ;kwa sasa kumeundwa tume ya kuriview katiba. Naomba tuiachie kazi na tuipe ushirikiano ili kutupati akatiba bora.n atuwaachie viongozi wetu wafanye kazi nyengine.hao wazanzibar wanahitaji maelekezo tu ya nini kazi ya tume wakioanisha na malalamiko yao