Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,886
- 6,883
Tukio la amani kuvurugia huko kisiwani Zanzibar na kusababisha mali za watu pamoja na baadhi ya makanisa kuchomwa serikali haiwezi kukwepa lawama kutokana na dalili za wazi watu kutaka mjadala wa Katiba mpya uende sambamba na kujadili Muungano wetu. Hakuna wenye kuchukia Muungano, ila kero mbalimbali zilizofumbiwa macho miaka nenda rudi ndizo zinazofanya watu wafikie hatu ya kuona sasa inatosha, tunataka tujadili Muungano wetu.
Kauli ya Rais Kikwete kabla na alipotangaza kamati ya kuratibu mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, alisema Suala la Muungano sisiguswe. Kauli hiyo inaweza kujenga maswali mengi na pengine kufikisha kwenye tukio la Zanzibar ukosekanaji wa amani kama ilivyotoke.
Ulimwengu wa leo utandawazi ndio unaofanya amani ipatikane, na pale wananchi wanaposhinikizwa kutogusa au kuongelea jambo linalowahusu hapo wanachukua njia nyingine ya kudai haki yao.
Busara kwa Rais wetu Kikwete kuruhusu Muungano ujadiliwe na wananchi katika mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya nchi, kwani kwa hali inavyoonekana sasa hivi jambo hilo halikwepeki kwa namna ye yote vinginevyo ni kukaribisha maafa zaidi ya yaliyotokea Zanzibar.