Kuna swali ambalo limekuwa likigonga kichwa changu kwa muda mrefu lakini kila nikijaribu kulitafutia jibu/majibu ninajikuta nikiwa njia panda kutokana na mazingira ya siasa za Tanzania.
Ikumbukwe kuwa, haijawahi kutokea kama sasa kabla ya utawala wa Rais Kikwete kwa wananchi kuwa na haki ya uhuru wa mawazo kama kama ilivyoainishwa katika Sura ya Kwanza, kifungu cha 18(2) cha Katiba yetu ya 1977.
Moja ya matatizo ya kuwepo kwa uhuru wa mawazo ni kuwepo kwa kundi la watu wanaotumia vibaya uhuru wa mawazo kwa manufaa ya ajenda zao za kishetani hasa ikichukuliwa kuwa, Uwongo hupanda lift kuwafikia walengwa wakati ukweli hutumia ngazi.
Miaka ya nyuma, Jamiiforums ilikuwa ni kisiwa cha kuchota majibu, lakini kwa sasa na kwa kiwango kikubwa, imekuwa ni kisiwa cha kuchota habari za uwongo na majungu.
Jamiiforums kwa sasa imejenga kitu kinachoitwa PRECEDENT na wataalam wa sheria.
Precedent is a legal case establishing a principle or rule that a court or other judicial body may utilize when deciding subsequent cases with similar issues or facts.
Kinachofanyika kwa sasa ndani ya Jamiiforums ni hii kitu inaitwa Persuasive precedent. Kwa sababu kuna baadhi ya watu hapo mwanzo walileta habari za ukweli kwa hiyo uaminifu huo umeendelea kukubalika kwa MODs hata kama kwa sasa wanaleta habari za kutunga na uwongo.
Pamoja na mapungufu ya Jamiiforums lakini hatutachoka kurudi na kuchota habari hata kama niza kutunga/uwongo kwa sababu kwa mtu mwenye fikra pana ana uwezo wa kuchuja na kuelewa ukweli wa habari/hoja.
Katika utawala wa Rais Kikwete, kuna mambo mengi mazuri na mabaya yametokea. Hii siyo mada ya kuyaangalia mazuri ya Rais Kikwete bali ni kutafuta ukweli kuhusiana na mabaya katika utawala wa Rais Kikwete katika eneo la ufisadi, udhaifu au chuki za kisiasa.
Niliwahi kumsikia Katibu Mkuu wa CCM, Mzee Kinana akijenga hoja na kusema Rais Kikwete anaangushwa na viongozi aliowateua. Hii sentensi unaweza ukadhani ni sentensi nyepesi lakini ukiichambua inatoa hoja nzito sana kwa kiongozi Mkuu wa nchi.
Neno anaangushwa na VIONGOZI na siyo anaangushwa na KIONGOZI linajenga akisi kama kuna udhaifu fulani ambao unamwangusha katika maamuzi yake.
Kuna madai mengi tu ya Ufisadi wa Rais Kikwete na familia yake ambayo yanatolewa watu mbali mbali kupitia vyombo vya kupashana habari na hasa ambavyo mkono wa serikali ya Tanzania unakuwa hauvigusi kwa urahisi (policing the internet) kama yalivyo magazeti na vitabu vinayouzwa mitaani.
Hakuna madai yanayotolewa kuhusu ufisadi wa Rais Kikwete yaliyowahi kubeba ushahidi hata wa kimazingira achilia mbali ushahidi dhahiri/wazi/hakika (tangible evidence) na kama upo ingefaa uletwe ili kujibu msingi wa hoja yangu.
Ni lazima tuelewe kuna tofauti kubwa kati ya individual corruption and institutional corruption.
Institutional corruption ni matokeo ya individual corruption ambayo yanajenga nguzo za uendeshaji ndani ya taasisi. Inahitaki kiongozi ambaye siyo mla rushwa au dhaifu ili kupambana na Institutional corruption.
Sifahamu kama Serikali ya Rais Kikwete kwa sasa ni Institutional corrupt lakini scandal kama za EPA zilikuwa zinaashiria hali kama hiyo.
Sitaki kuingia kwenye hoja za Institutional corruption katika mada hii kwa sababu siyo malengo ya hoja zangu.
Kwa mfano, Wakati wa kampeni ndogo za Ubunge wa Ridhiwani Kikwete katika jimbo la Chalinze, nilitegemea kama utakuwa ndiyo uwanja mpana wa kufahamu ufisadi wa familia ya Rais Kikwete, lakini kiu yangu haikuisha kwa sababu hakuna mtu/mwanasiasa aliyejitokeza kueleza ufisadi wake kwa njia ya tangible evidence.
Miaka tisa iliyopita, wananchi wengi wa Tanzania walikuwa na matumaini makubwa kwa ujio wa Rais Kikwete katika ofisi ya juu ya taifa letu. Takwimu zinaonyesha mwaka 2005 waliojiandikisha ni watu 11,875,000 na zaidi ya 72.4 waliweza kupiga kura, lakini mwaka 2010 imekuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kupata asilimia 42.8 kati ya jumla ya wapiga kura 19,694,055 waliyojiandikisha Tanzania Bara.
Takwimu kama hizi zinaakisi picha ya kufifia kwa matumaini ya wananchi katika utendaji wa serikali kupitia wanasiasa.
Kuna sababu nyingi, lakini moja ya sababu ya wananchi kujiandikisha kwa uwingi halafu wapiga kura wanakuwa ni wachache ni kukosa matumaini kutoka kwa wanasiasa wanaogombea.
Wananchi wanadhani hakuna mwanasiasa katika wale waliojitokeza atakaye wapa kile ambacho wanadhani hakipo kwa sababu wote ni wale wale bali wanatofautiana majina. Ikumbukwe uandikishaji wa wapiga kura huwa unatangulia kabla ya majina ya wagombea kuchaguliwa kwenye vyama.
Idadi ya watu wachache walijitokeza mwaka 2010 kwenda kupiga kura inaonyesha jinsi wananchi walivyokosa matumaini katika serikali ya Rais Kikwete ambayo ningependa pia kuelewa kama moja ya sababu ya kukosa matumaini ni ufisadi, udhaifu au chuki za kisiasa ambazo wananchi wamelishwa/wanalishwa na kuzimeza kutoka kwa wanasiasa wenye ajenda za kishetani kiasi kwamba wanadhani hakuna umuhimu wowote wa kupiga kura.[Cheo ni Thamana Jamani na si Umwinyi.) na (Ndio maana Cheo hicho kinagharamiwa na Walipa Kodi matarajio yakitegemewa kuwa ni Matunda Mema na sio Yaliyooza) Sasa wewe Kiongozi utuleteapo Uozo tukupigie makofi na Tubugie tuu...!:alien: Labda Uwe wewe ni Chizi na Mwendawazimu, maana umeadhirika Kiakili.:msela:QUOTE]