Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
- Thread starter
- #21
Mkuu Julius Kaizari umeongea hoja fikirishi.Ng'wamapalala,
Kikwete ni Rais dhaifu,mnafiki,na Fisadi.Hayo mawili ya mwanzo yapo wazi. Hili la pili huwa ni vigumu kwa Rais akiwa madarakani kugundulika ushezi wake,kwakuwa analindwa na Vyombo vya dola. Kwa hali halisi,subiri amalize muda wake,utaona uozo. Yote au mengi yanayosemwa yanakweli au chembe chembe za kweli ndani yake.Mwanae Ridhiwan anautajiri wa kufa mtu,bila shaka Baba yake anamkono katika hili. Mimi niliwahi fanya Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko,kuna Waturuki fulani walipata favor ya serikali hii,kwa mgongo wa kikwete,worth billions of Money,huo ni mfano mdogo kati ya mingi.
Tuombe amalize salama atuachie skeleton ya nchi yetu.
Unadhani vyombo vya dola vinamlinda vipi Rais Kikwete na ufisadi wake ili wananchi wenye mapenzi mema na taifa wasiweze kupata ushahidi kamilifu kuhusiana na Ufisadi wake.
Kuna wengine wameanza kujenga hoja wakisema, udhaifu kwa kiongozi ni kichocheo cha ufisadi katika nchi ambayo haina misingi imara ya utawala.