Rais Kikwete "NAKUSHAURI UJIUZULU"

Ya gesi tu au kuna mengine? Wenzio bado tunamtaka.


Wanaotumia madawa ya kulevya wanaweza kusaidiwa matibabu, lakini ni Ray C tu siyo wengine; huyu anamtaka mimi simtaki sina matatizo ya kujitakia au kutakiwa
 
Sijui kama anajitambua yeye anaona ametuletea maisha karaha badala ya maisha bora lakini kwake si kitu
 
hawezi achia ngazi kirahisi hivyo huyu rais wetu, japokuwa yuko kwenye hard time. anajuaga kujikaza kisabuni.
jamani big show yuko wapi mbona yuko kimya hivyo! kuna uzima huko ndugu yangu?
 
Wakati unaingia watu walikuwa na imani sana na wewe lakini huenda ukaondoka
wakati watu (Watanzania) wamejenga chuki kubwa sana kwako. Yanayojitokeza
ni mengi na hayajawahi kutokea awamu yoyote ya uongozi katika nchi hii, huenda
washauri wako hawana nia nzuri na wewe kwa kukutumbukiza katika majanga mabaya
ambayo mwisho wa siku yameifanya nchi yetu kuondoka katika sifa ya kuwa kisiwa
cha amani.

Huenda CHADEMA Wanakuhujumu ili usitawale vizuri.

Huenda WAPINZANI wanakufitini kwa kukitaka kiti chako.

Huenda ni MAADUI ZAKO NDANI YA CHAMA wanakufanyia yote haya.

Huenda wananchi umeshindwa kuwatekelezea ahadi yako ya maisha bora

Umeleta kaulimbiu ya kujivua gamba nafikiri ni muda muafaka sasa kama mwenyekiti
wa Chama kuonyesha mfano kwa wenzako. JIVUE GAMBA mkuu yasijekutokea yale
ya misri kwani kuna kitu kina fukuta chini kwa chini.

Mimi sipendi utoke, napenda kukuona ukiwa ikulu lakini kwa hali jinsi ilivyo
ni Bora umkabidhi nchi Magufuli, Mwakyembe au hata NAPE sio mbaya kwa
muda tu wakati tunasubiri katiba mpya na uchaguzi mwingine.

Watanzania naona kama wanavuta Bangi siku hizi wasije kukung'oa kwenye
kiti kwa upuuzi wao wanaouita nguvu ya Umma.

Ni hayo tu.


Wako mdau wa gesi.
(NAUNGA MKONO MATUMIZI YA GESI KWA WATANZANIA WOTE)

Joseph A Chinamkalava
box........
Mnyambe
Newala

sio bangi maisha magumu wkt anaingia walikuwa wamepinda na sasa wamejikunja kabisa,hii nchi ukipata post ya kukimbia usigeuke
 
Back
Top Bottom